SoC01 Uraibu wa Ngono

Stories of Change - 2021 Competition

Jade_

Senior Member
Apr 19, 2015
122
214
Uraibu upo wa aina nyingi. Kuna uraibu wa pombe, sigara, madawa ya kulevya, na uraibu wa chakula. Leo nitajikita kwenye uraibu wa ngono.

Tofauti na uraibu wa pombe, sigara na madawa ya kulevya ambazo hazimpati yeyote, (sio kila mtu atangukia kwenye raibu hizi) uraibu wa chakula na ngono ni rahisi kumpata mtu yeyote, kwa sababu miili yetu kibayolojia imeumbwa kuhitaji vitu hivi. Uraibu huu ukiongezea na uraibu wa video za ngono za mtandaoni (nitaongelea siku nyingine) inawaharibu kabisa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa na kuhatarisha mustakabali wetu.

Dalili za uraibu huu ni kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengi kwa wakati mmoja. Iwe mwanaume au mwanamke, kama muda wote unawaza kufanya ngono na huwezi kujizuia basi jua kwamba una shida mahali. Kama unatumia muda mwingi sana kupita na kuzunguka kwenye maeneo ambayo unajua utakutana na watu wa kulala nao au unatumia pesa nyingi kupita uwezo wako ili upate ngono basi una shida.

Kama upo tayari kufanya chochote na lolote ili kukidhi kiu yako ya ngono, bila kujali kama unavunja sheria, unaumiza watu au unajiweka katika mazingira hatarishi una shida. Kama huoni binadamu wana utu ila ni wakulala nao tu basi kuna shida. Kama upo tayari kuvumilia kudhalilishwa na kujidhalilisha ili upate ngono, kuna shida.

Je, nini kinasababisha uraibu wa ngono? Kuna sababu nyingi lakini wataalamu wengi wanakubaliana kwamba haya ni matokeo ya kudhalilishwa kingono utotoni. Kuna wanaopapaswa sehemu za siri na wafanyakazi wa ndani. Kuna wanaoambiwa na wafanyakazi wa ndani wawapapase sehemu zao za siri. Wengine wanadai walifanya mapenzi na watu wazima walivyokuwa watoto (kwa wanaume hii ni sifa). Kuna wengine wanabakwa na ndugu jamaa, marafiki na watu wa dini. Kuna wanaoadhibiwa kwa kupigwa sehemu za siri.

Kuna wanao angalia picha na video za ngono tangia wakiwa wadogo. Chochote unachomfanyia mtoto akiwa mdogo ndicho kitakaa naye mpaka atakapoingia kaburini. Rejea uzi wangu kuhusu elimu kwa watoto wadogo . Unapomzoesha mtoto mambo ya ngono unamwekea akilini kwamba upendo na mahusiano ni ngono. Binadamu tunahitaji kuwa na mahusiano mazuri na binadamu wenzetu kusaidiana na kupeana moyo. Watu wengi ni wapweke na wanafikiri kwamba ngono ndio namna ya kuondokana na upweke.

Sababu nyingine ni jamii yetu. Tangia tukiwa wadogo tunaambiwa kwamba mwanaume kazi yake ni kutafuta ngono na mwanamke kazi yake ni kuwa chombo cha ngono. Kama wewe ni mwanaume na hufanyi mapenzi muda wote au haupo mawindoni muda wote basi unaonekana una walakini kwenye maumbile yako. Kama huna wanawake wengi kwa wakati mmoja au kama haupo tayari kufanya mapenzi na mwanamke yeyote atakayekutaka basi unakuwa kituko. Utaambiwa ndio bayolojia ya mwanaume ilivyo na muda wote anahitaji kutulizwa hamu.

Kitu ambacho siyo kweli na mara nyingi mwanaume huyu anahitaji mtu wa kumsikiliza na mtu atakayeweza kumwamini ili amtegemee. Mwanamke kama hujakaa kimvuto wa kingono unaowatamanisha wanaume basi wewe thamani yako inashuka kwenye jamii. Kama ukimtega mwanaume na hajategeka basi kama mwanamke umefeli. Kama hutamaniki huna mantiki ya kuishi. Hapa inaonyesha ya kwamba hata kama mtu alikuwa asiwe mraibu wa ngono atakuwa tu kwa sababu ndivyo jamii inavyomtaka awe.

Lakini cha kuchekesha ni kwamba jamii hiyohiyo inayokutaka uwe kiumbe cha ngono muda wote inataka pia usifanye ngono. Hizi ni jumbe mbili kinzani. Ngono inafanywa kama vile ni dhambi kubwa mno na hata hisia za kufanya ni udhaifu wako wakutenda dhambi. Hii ni sababu inayopelekea watu wa dini mara nyingi kuwa waraibu wa ngono. Wanafahamu kwamba wana shida na katika harakati za kutatua shida hiyo wanafikiri kwamba wakishika sana dini na wakijinyima kabisa kufanya ngono watakuwa amejitibu.

Wanafikiri kwamba uraibu wa ngono ni udhaifu wao na wanatakiwa kuushinda kwa namna yeyote ile, kitu ambacho si kweli. Ukijinyima sana kufanya kitu basi ndio utakuwa unakiwaza muda wote. Mtu ambaye yupo kwenye diet atawaza chakula muda wote. Hii inapelekea kusikia kesi za mapadre kulawiti watoto au viongozi wa dini kuishi maisha ya aina mbili. Mchana anahubiri, usiku ananunua machangudoa au anatembea na waumini.

Madhara ya uraibu wa ngono ni mkubwa mno. Achilia mambo ya magonjwa ya zinaa yasiyo na tiba kama UKIMWI na Kaswende (haya pia ni majanga). Mzazi ambaye ana uraibu wa kutembea na watoto atawaambukiza na wao wawe na uraibu wa kutembea na watoto wao. Na kuna uwezekano mkubwa huyo mzazi alifanyiwa hivyo na wazazi wake. Hata kama mzazi hatembei na mtoto lakini kuna uwezekano mkubwa mtoto huyo akarithi tabia hizo, yaani na yeye akawa mraibu wa ngono. Kiufupi vizazi vinaharibika.

Uraibu wa ngono unasababisha watu wabake, watembee na watoto wachanga, wanyama na tabia nyinginezo ambazo zinatisha. Watu hawa wanahatarisha maisha ya watu wanaowazunguka. Pia uraibu huu unakulevya kama madawa, muda wote unakuwa kama ndio umetoka kuamka. Huwazi kufanya chochote cha maana na unawaza ngono tu. Mahusiano ya familia na wanaokuzunguka yanazorota, unakuwa mtu wa siri sana. Kibaya pia ni matatizo ya kisaikolojia. Ngono haiwezi kutatua maumivu tuliyoyapata tukiwa wadogo na kuendelea kufanya ngono kupita kiasi kunazidisha matatizo.

Watu hawa hufanya binadamu wenzio kama vyombo vya starehe na wapo tayari kuwafanyisha vitendo vya kiudhalilishaji ili kutimiza haja zao, kama vile kulazimisha kuingia au kuingiliwa kinyume cha maumbile. Au matendo ambayo sio za kawaida. Kifo cha mende kwake ni ushamba.

Je, nini kifanyike? Kutibu uraibu wa ngono sio kitu kirahisi. Kuna mwanamke anafikiri kufanya mapenzi muda wote na mumewe kutamsaidia aridhike na asichepuke. Hii ni imani potofu. Huwezi kumsaidia mraibu wa madawa kwa kumpa madawa kila anapotaka. Au kwamba kujinyima kabisa ndio suluhisho hapana. Pia kutunza siri ya uraibu huu hasa kwenye familia hakumsaidii mraibu na wanaomzunguka. Kutunza siri kunaendeleza hii laana na kuangamiza vizazi hadi vizazi. Ni bora afungwe jela asidhuru mtu tena. Na akiwa huko apate tiba.

Mtu mwenye uraibu wa ngono anatakiwa apate ushauri wa kisaikolojia. Kwa hapa Tanzania ni ngumu kidogo kwa sababu hospitali iliyobobea kwenye mambo ya akili ni moja tu ambayo ni Mirembe. Kwa sababu hiyo basi inabidi watu wenye haya matatizo watengeneze makundi yakupeana moyo. Makundi ya kuongea na kusikilizana.

Hii ni tiba inayotoa unafuu mkubwa sana na kuwapa waraibu matumaini. Hata asasi zinazoshughulika na uraibu wa madawa na pombe zinaweza kupokea pia waraibu wa ngono (hatua za kutibu raibu zote zinafanana). Inabidi muhathirika atambue sababu ya uraibu wake. Atafanya hivi kwa kupata tiba ya muda mrefu ya ushauri nasaa. Serikali iwekeze sana kwenye miundombinu ya magonjwa ya akili hasa katika kuongeza wataalamu wa saikolojia ili waweze kutibu watu ambao kwa nje wanaonekana wapo sawa na si mpaka wawehuke ndio wapate msaada.

Wazazi na walezi jamani, tunzeni watoto wenu. Usimuache mtoto akalale kwa ndugu au jamaa, usiogope kuambiwa unadekeza mtoto, au unamficha mwanao. Tuwapende watoto na tuwasikilize ili waweze kuwatengeneza mawazo mazuri ya mahusiano na binadamu wenzio waepukane na upweke. Watu wengi ni wapweke na upweke hata siku moja hautatatuliwa kwa kufanya ngono. Mwisho kila mtu kwa imani yake na kwa Mungu wake asali sana, na amini kwamba Mungu anampenda na atamsamehe kwa makosa yake hata kama ni makubwa kiasi gani.

Kitabu cha Out of the Shadows: Understanding Sexual Addiction kilichoandikwa na Patrick Carnes Ph.D kinatoa maelezo ya undani na ya ziada kuhusu uraibu wa ngono.
 
Mkuu
Mawazo mazuri na ya muhimu sana.
Ila sina hakika kama wajumbe wanaweza kukuelewa vizuri ama kutilia maanani.

maada za aina hii humu naona hazitiliwi sana maanani,ingawaje zina mguso mkubwa kwa jamii ya sasa.
Ahsante.
Ni kweli watu wengi hawataona umuhimu wake kwasababu jamii yetu inaona ni jambo la kawaida.
Kuna shida lakini watu wanakataa.
 
Hili tatizo linanitesa sana natamani nipate mwanasaikolojia wa kuniwezesha kuacha haya mambo
 
Yaani nilikuwa Na nyege za ajabu Sana ambazo zilikua zinanipush nifanye mapenzi muda woote

Oga maji yabaridi yanasaidia Sana kupunguza mihemuko
Ndio hili ni suluhisho zuri la harakaharaka.
Tatizo lako ulikaa nalo kwa muda gani?
 
Hili tatizo linanitesa sana natamani nipate mwanasaikolojia wa kuniwezesha kuacha haya mambo
Pole sana mkuu. Wanasaikolojia Tanzania wapo wachache. Labda upate matibabu hospitali ya Mirembe.

Kama kufika Mirembr ni shida, mtafute hata kiongozi wa dini yako (kama unayo). Lakini uwe makini kwa sababu hawa watu wanaweza kukuongezea ugonjwa. Tafuta mtu yeyote ambaye ni muelewa ambaye hatokuhukumu.

Na pia lazima utambue tatizo lako lilaanza lini.
Je maisha yako ya utotoni yalikuwaje?
 
Pole sana mkuu. Wanasaikolojia Tanzania wapo wachache. Labda upate matibabu hospitali ya Mirembe.
Kama kufika Mirembr ni shida, mtafute hata kiongozi wa dini yako (kama unayo). Lakini uwe makini kwa sababu hawa watu wanaweza kukuongezea ugonjwa. Tafuta mtu yeyote ambaye ni muelewa ambaye hatokuhukumu.
Na pia lazima utambue tatizo lako lilaanza lini.
Je maisha yako ya utotoni yalikuwaje?

kufika dodoma ni mtihani
na amna ninayemuamini wa kumueleza mambo yangu.

Lilianza nilipoanza sex tuu hadi leo naona ni mzigo ninaoshindwa kuutua

Maisha yangu ya utotoni sidhani kama yalikuwa na shida yoyote.
 
kufika dodoma ni mtihani
na amna ninayemuamini wa kumueleza mambo yangu.

Lilianza nilipoanza sex tuu hadi leo naona ni mzigo ninaoshindwa kuutua

Maisha yangu ya utotoni sidhani kama yalikuwa na shida yoyote.
Pole sana. Naomba niulize, uraibu wako ukoje? Mf unawaza kufanya mapenzi muda wote, au unapiga punyeto sana nk.
 
Pole sana. Naomba niulize, uraibu wako ukoje? Mf unawaza kufanya mapenzi muda wote, au unapiga punyeto sana nk.
punyeto sijawahi kufanya
nikimaliza wiki nzima bila kusex zaidi ya mara moja huwa nashukuru Mungu tena ukizingatia niko kwenye early 20s hata kuoa sijafikiria sasa inapotokea nimekosa mtu wa kusex nae kwa wiki nzima nakosa amani kabisa.
 
punyeto sijawahi kufanya
nikimaliza wiki nzima bila kusex zaidi ya mara moja huwa nashukuru Mungu tena ukizingatia niko kwenye early 20s hata kuoa sijafikiria sasa inapotokea nimekosa mtu wa kusex nae kwa wiki nzima nakosa amani kabisa.
Ahaaa. Kwahiyo usiposex wiki nzima unaona kama umekosa au umepungukiwa kitu?
Je una mahusiano? Familia yako ikoje? Unaishi na nani?
 
Ahaaa. Kwahiyo usiposex wiki nzima unaona kama umekosa au umepungukiwa kitu?
Je una mahusiano? Familia yako ikoje? Unaishi na nani?
kabisa yani

ninayo mahusiano

Familia ipi?
kama ni ndugu zangu ipo vizuri tuu

Naishi mwenyewe
 
kabisa yani

ninayo mahusiano

Familia ipi?
kama ni ndugu zangu ipo vizuri tuu

Naishi mwenyewe
Upo kwenye mahusiano na unatafuta watu wengine wakulala nao au sijakuelewa?
Na kwanini usiposex unaona unapungukiwa? Kwasababu unakuwa una hamu sana au?
 
Nilijikuta nimeangukia shimoni mkuu na iliniaharibu hata kimuonekano
Duu pole sana. Nahisi ulionekana kama mraibu wa madawa.
Enzi hizo uraibu umeshamiri, ulikuwa unataka kufanya mapenzi masaa 24 au? Na kazini je?
 
Back
Top Bottom