Urafiki na huyu brother umekuwa ni changamoto sana kiuchumi

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,508
99,303
Naombeni ushauri wakuu,

Ni Hivi,
Nakumbuka Kuna kipind niliwahi kuleta humu kesi ya Brother yetu mmoja (mkubwa kiumri) kumuoa mchumba wa miaka mingi wa rafiki yetu (mdg kiumri) Kama MKE mdogo.
Sasa hii ya leo, rafiki nnaemzungumzia Ni uyo uyo jamaa.

1. KESI YA KWANZA,
Nikiwa dukan KWANGU nauza, brother uyu kanipigia Simu anaitaka bidhaa flani. Nikampa Bei kwamba atanipa laki 9 Maana sokoni kuiuza Ni mil 1 net.
Akalalamika Bei ni kubwa namuuzia,kwamba sio ya mteja, nakwenda kutumia yy mwnyw Tena dukani kwake.
Kwakua ni mfanyabiashara mwenzangu afu rafiki yangu, Tena anakwenda kutumia mwnyw basi sikuona haja ya kumuuzia kwa faida.
Nikamwambia Basi utanirudishia laki 7 yangu Maana ww mwnyw Bei ya kuagizia unaifahamu.
Akasema "sawa"
Akatuma mtu akaja kuichukua, MDA si mrefu Akanambia inachangamoto kdg Kwny kuiset ikae vizur.
Nikamwambia kaka leo Niko mwnyw ofsni, Sina wa kumuachia.
ila usiwe na shaka, nkifunga ntapitia ofsn kwako jion nikusetie mwyw ikae sawa. Akasema POA.
Jion nmempitia dukn kwake kwenda kuiset, ananambia
"Dah! Kaka samahan kwa usumbuf, unajua ule mda Niko nahangaika kuiset nikapata mteja wa mil moja nikaiuza pale pale"
Nikamwambia, "Basi Jambo la heri"
Tukaagana maisha mengine yakaendelea.

Basi baada aya siku 2 yake Nikiwa ofsn nikiwa naangalia baadhi ya wateja walioweka Oda zao, niwakumbushe waje kuchukua mizigo.
Nikampigia mteja mmoja akanambia,
"Kaka ule mzgo nilishapata mbona, ulikataa kuniuzia kwa laki 9, nmeshachukua tayar siku ile ile kwa flan (uyo brother niliemuuzia) kwa sh.laki 8"

Dah! Nilipatwa na mshangao Sana maana Iyo Siku anayosema ndo siku nmemuuzia uyo jamaa yangu, afu jamaa anauzaje Bei ambayo hata sokoni haipo?
Nilipompigia akanambia uyo mteja muongo, huenda akakulaghai ili uwe unamuuzia Bei pungufu. Uku kwangu kalipa mil. 1 cash. Basi nikamuelewa ikawa imeisha hivyo.

KESI YA PILI,
Kuna chombo nilikua Nini miezi miwili TU tangu nikinunue alikuja kuazima kwangu kwamba anaenda shambani kwake mkoani kwa wiki 2, nikampatia.
Ile Kurudi ananirudishia ila akanambia Kaka Kuna sehem kiliharibika anaomba sana radhi. Basi nikamwita fund Wang akague kujiridhisha.
Fund akanambia kwa jins kilivyo haribika, Ni changamoto sana kukitengeneza maana spea yake itabidi iwe ya kuchongea, orijino huwez KUPATA kwa Sasa hapa bongo na hali Hii ya Corona.

Nikaona huu utakua usumbufu Sasa.
Basi nikamwambia jamaa kwakua yeye bado shughuli zake Ni endelevu uko shamban, na.mimi sikitumii mara kwa mara kwann asinirudishie nusu gharama yake yake ya sokoni,akakitengeneze mwnyw ili akimiliki moja kwa moja.
Jamaa akafurah na kweli baada ya wiki moja akaniletea ile pesa cash , nikamkabidhi nyaraka zake na maisha yakaendelea.

Miez miwili baadae, nmehudhuria harusi fulani parking. Nikakiona kile chombo anacho jamaa mmoja tunafahamiana tuliwahi kufanya biashara flani miaka ya nyuma sana. Basi nikamsifia chombo chake kizur, akambia kanunua Hapa Hapa bongo tena Kias kadhaa (robo tatu ya Bei ya kipya) . Nikamwambia bei ya kutupa kabisa hii ebu nikitest kidg. Kutest kimekaa vizur Lile tatzo la mwanzo hamna tena na kimeboreshwa Sana ndani na nje yake.

Nikamuuliza kakinunua hivyo hivyo au kakiongezea manjonjo?. akasema kakinunua hivyo hivyo. Basi ikawa imeisha hivyo. Ila nikajiuliza inakuaje rafki yangu anauza haraka Hivi na afu hata hajanambia? Hii sio fair.

Basi Siku Moja mkewe mkubwa kaja ofsin kwangu kuchukua bidhaa flan, bas ktk kunisimulia habar za maendeleo ya shamban kwao nikachomekea stori ya kile chombo kua vipi mlifanikiwa kukirekebisha Lile tatizo.

Akanambia Mbona fundi flani (yule yule fundi wangu) alirekebisha, akakarabati Tena na kikaa vizur sana na ikauzwa wiki ile ile pesa nzur sana Kia's flani na pesa waliopata ndio wamenunulia mashamba mengine ya kulima Tena mwakani. Basi nikamsifia afu Nikabakiwa na maswali.
Inamaana nilipewa USHAUR wa uongo na fundi wangu kwamba hakirekebishiki kirahisi au?
Sasa uyu Mbona kauza kwa faida kubwa kuliko niliyomuuzia na hakunambia?

Anyway, nikamtafuta fundi kumuuliza imekuaje kuaje, fundi akanambia kwamba yeye aliitwa kufunga tu spea maana jamaa tayar spea alikua nayo pale pale kwake.
afu akapewa kazi nyingine ya kuibadilisha muonekano ivutie zaidi maana ashapatikana mteja tayar anaitaka.
Kwaiyo yeye alifanya TU kazi yake. Basi nikaachana na fundi .

Nikamcheki brother,
akanambia nimsamehe Sana alikua na mkopo benki anadaiwa kwaiyo aliiuza haraka kulipa Deni la mkopo.
Nikamtafuta mkewe mkubwa nikamuuliza khs Deni, akakataa kata kata kua hakukua na Deni Wala Nini.
Basi nikajua jamaa kanifanyia uhuni, nikampigia tena akanipa MAELEZO hayaridhishi anang'ang'ana nimwambie aliesema Hana Deni kwanza Ni Nani uyo.

Nikasema yaishe nmekuelewa maana kwa jinsi alivopanic nikaona nikisema Ni mkewe mkubwa ntawaingiza Kwny mgogoro.
Ikabidi niliache Kama lilivyo ila akili yangu ikanambia uyu Kuna namna kanihujumu au Kama Ni Deni kweli POA TU, Haina shida.
Ikawa imeisha hivyo.

KESI YA 3,
Brother yangu uyu alikua na saiti yake haijakamilika anajenga lodge ya vyumba 12.
Basi uku kwangu kuna material zangu za ujenzi zilibaki (nondo, square pipes, na bati geti, welding sticks na black pipes) Akaniomba nimuazime akimbize ujenzi wake aanze kupiga Ela haraka ila siku nikizihitaji MDA wowote atanipatia. Nikasema sawa, nikampatia.

Baada ya MDA tukaenda site kwake tukakuta kasimamisha ujenz,nkamuuliza tatizo nn akasema biashara zimeyumba kiasi. Basi nikamshaur akomae kwnz na biashara maana huu ujenz upo mdg mdg atamaliza. Akasema sawa.

Sasa kuna kipind nikaja kuibiwa dukan KWANGU, baada ya ule wizi ikanilazimu kukarabati na kuimarisha ofisi yangu. Basi nikamuomba material zangu zile nilizomuazimisha anirudishie nikarabati ofisi yangu.

Akanambia zile material hazipo ameshaziuza, nikamwambia Mbona unakosea Kaka unauzaje kitu ulichoazimisha ukatumie mwnyw Hii tabia sio nzuri na Sipendi. Akaomba radhi ila akasema hakijaaribika kitu atanipatia pesa nikanunue nyngn. Nikasema sawa.

Kweli akaingiza pesa, ila changamoto akanirudishia pesa ya thaman ile ya mwanzoni vinauzwa kabla Bei hazipanda. Nikamuuliza inakuaje akasema Kaka iyo ndio pesa niliyouzia vitu ukinicharge zaidi unakua Kama Unanikomoa. Kwa Sasa Sina pesa kabisa.

Anyway, nikapotezea
Ila kiukweli nilichukia Sana maana niliongezea Zaid ya laki 4 juu kwenda kununua vipya kwa wakati ule ikiwa Ni nje kabisa ya Bajeti yangu. Ikawa imeisha hivyo.

KESI YA NNE,
Nilikuja kusafiri kwa wiki 2 kupakia mzgo wa ofisi, niliporudi breki ya kwanza ni kukagua hesabu za mauzo dukan kipind chote nilichokua sipo.

Kuna mahali nikakuta wameuza vitu kwa Bei ya hasara mno, Nikauliza imekuaje. Kijana ananambia Hivi vitu alikuja kuchukua rafiki yako flani mfanya biashara mwenzio (uyu jamaa angu) alisema yeye huwa unamuuzia Bei iyo na kwakua ulkua upatikani tukamuuzia hivyo hivyo TU.

Dah! Nilichoka maana Iyo bei hata kwa mzalishaji haipo na nimeingiliwa Sana.
Ikabd kumfata jamaa. Akajitetea kua alkua hajui Kama Bei zimepanda. Nikamwambia sio kweli maana Bei ulochukulia mzgo hata tunakoagiza hawauzi hivyo.

Akajitetea kua labda alikua na mawazo MDA ule ananunua.
Nikamwambia iyo pesa ilopelea nitakudai, akasema POA nitailipa.

Sasa deni lile likakaa MDA mrefu sana halijalipwa, kuna siku ikapelea bidhaa Moja kwangu, nikampigia akasema anayo. Nikamwambia Basi mpe wa kirikuu ailete kuna mteja anaisubiri Hapa. Akafanya hivyo.

Mteja alivonilipa pesa, nikaitia Kwny droo yangu na kumlipa kirikuu elfu 10 yake ya usafiri na kumwambia aende zake.

Jamaa akanipigia Mbona sijampa Ela yule wa kirikuu, nikamwambia nmeikata kwny Lile Deni letu la siku ile na nmebaki nakudai elfu 70.
Jamaa alilalamika Sana kua sijamtendea fair,
nikamwabia , brother ilo deni MDA ulkua mrefu. Afu umekausha unahisi nmesahau. Akalalamika Sana hata sikujali na maisha yakaendelea.

KESI YA TANO,
Kuna mzee flani Ni dreva kirikuu anapaki mitaa Hii hi ya dukan kwangu. tunamtumia Mara kwa Mara kupeleka mizigo ya wateja wetu,

Basi kuna bidhaa Moja anaipenda sana pale dukan na kila akiiona mate yanamtoka Sana anataka ampelekee mkewe nyumbani ila anabaki kulalamika akisema namkazia mno kumpatia kwa 270,000.
Namwambia kua Bei yake halisi Ni 350,000 ila yeye nmeshamwambia ntamuuzia kwa 300,000. anaishia kulalamika kua ana 270,000 haiongezeki hata Mia. Nikamwambia wee iache cha muhimu haiozi basi watanunua wengine. Basi ikawa hivyo.

Kuna siku brother angu uyu akaja dukan kwangu kua anaihitaji iyo bidhaa, nikamwambia wewe nipe 300,000 wewe kauze 350,000 au zaidi ya hapo utajua mwenyewe.

Akanambia hapana sio ya kuuza, niuzie kwa 200,000 Bei tunayonunulia wote kwa JUMLA maana nampelekea wife wangu mdg nae akafurahi nyumbani. Nikasema hapana wee Ni muongo unaweza sema unampelekea wife kumbe unaenda kuiuza kwa faida. Ndo tabia yako.

Akasema namfikiria ndivyo sivyo,
Nikamwambia Hapa mpk nipate uthibitisho wa shemej mwnyw ndo ntakuuzia Bei hii.
Basi nikampigia shemej, akasema kweli taarifa anayo. Basi akanipa laki 2 cash nikampatia bidhaa akaenda nayo.

Sasa baada ya siku Kama 5 mkewe mdg kapitia dukan kwangu kunisalimia Kuna duka la jiran alkikuja kununua mahitaji yake.
katika kusalimiana akanambia kwamba alichomfanyia uyu ndugu yangu hajakipenda, nikamuuliza Kipi. Akasema ile bidhaa alomnunulia kipind kile ilikaa siku mbili TU pale nyumbani Kisha akaiuza tena.
Nikamuuliza ya kweli Ayo, akasema ndio Ni serious. Nikamwambia Basi nitaonana na anambie tatizo nn.

Sasa ktk Yale maongez kijana wangu wa dukan akawa anayasikia, alivotoka tu yule mwanamke kijana akanambia analosema uyu mama Ni kweli kabisa 100% na ile bidhaa kamuuzia yule mzeee flan dreva kirikuu.
Kijana akasema kua Yule mzee alimwambia kua sisi tulikataa kumuuzia kwa 270,000 kaenda kwa jamaa kauziwa kwa 250,000.

Baha nzur mzee Hakua mbali,
Nikamwita yule mzee kumuuliza, akakiri kweli alinunua kwa jamaa kwa 250,000.

Dah! Kusikia Yale Maneno nilichoka sana, ikabidi kumpigia jamaa jioni tuonane baa flani nna maongezi nae.

Nikawapigia marafiki zangu wengine wanne nikawawaleza matukio yote ya mwanzo, Basi wakaashaur jion iyo nao wawepo ili tuambizane mbivu na mbichi. Uyu mwenzetu Anachofanya sio kizur

Jioni imefika tumekutana baa,
Katikati ya kilaji tukaingia kwny mada, nikaeleza kesi zote kuanzia Namba 1 mpaka Namba 5.

Wao wakashaur yaishe ila jamaa awe TU muungwana, aweke wazi maana anachokifanya Ni kuwagawa wateja.

Yaan ionekane kwangu nauza Bei kubwa, ila wakienda kwa jamaa wanauziwa Bei ndogo sana wkt mzgo huo huo umetoka kwangu kwa kigezo cha urafiki na anakwenda kutumia mwnyw. Huku Ni kurudishana nyuma kibiashara maana Bei tunazouziana sisi hazina faida. Tunalindana TU kila mmoja wetu apate.

Ile kesi ya chombo, ikaonekana kweli jamaa alikiharibu kusudi akiboreshe ili akiuze kwa Bei ya faida kwa kunizunguka pamoja na fundi wangu, hakua na Nia yakukitumia Kama alivyokua mwanzo na kushukuru.

Kwenye vifaa vya ujenzi ikaonekana kumbe hakua na kazi navyo wkt ule, tayar alishapata mtu anavihitaji kwaiyo alipovichukua tu kwangu alienda kuviuza kwa mtu Moja kwa Moja na sio kuvitumia Kama alivyoomba. Ikaonekaa huo Ni uhuni. Ni Bora TU angesema kapata mteja wore tujue tunafaidika vipi. Na sio achukue kwa mgongo wa kutumia kumbe Lengo Ni kuuza.

Basi jamaa yote akaomba radhi yakawa yameisha. Hivyo. Tukagonga bia tukaenda majumbani kwetu.

KESI YA 6,
Kuna siku Uyu jamaa yangu kaja anashida ya pesa Kias kadhaa anaazima akarejeshe mkopo wa benki mambo yameyumba kabisa, nyumba ya bimdg wake itapigwa mnada MDA wowote.

Sasa kutokana na kwamba mzigo ulikua mkubwa nikamwambia MDA ulobaki Ni mchache Sana afu mambo ya uchumi sio mazur Ni Bora tukachangia na jamaa zangu wengine tujue tunakutoaje hapo mwenzetu. Akasema sawa.
Basi tukapanga jion yake tukutane bar na jamaa zangu 5 JUMLA 6 tujue tunamkwamuaje uyu.

Sasa kabla hatujaenda bar, baadhi ya jamaa wakawa wanaonyesha mashaka yao khs ukweli wa Hilo suala. Akapigiwa bi mdg, kweli akakiri kulijua Hilo suala anatusihi tumsaidie mme wake.
Basi jamaa wakakubali.

Ila Pale pale Kuna jamaa wakawa wanakiri kua jamaa Ni msumbufu kwny suala zima la ulipaji wa madeni , Kuna mtu na akakiri hajawai mrejeshea mil. 5 inamiaka Zaid ya 6 aliazima, amekausha anahisi kasahau. Tutamuaminije kwa kesi Kama Hii?
Basi tukaona haina haha ya kurudisha ya nyuma, hebu tukamsikilize.

Basi tukakubaliana, twende tukakonane nae ila haya mapungufu yote yanayosemwa hapa Ni lazima tumwambie ajue na Kama ni maisha ya ujanja ujanja basi hayatomsaidia chochote.

Jion kweli tukafika na tukakubaliana tutamsaidia, ila Sasa baada ya hapo kila mtu akaonesha bado anamashaka na yeye.

Zile ahadi za kutoa mchango zikawa zinasua sua mpk siku ya tuliposikia tangazo la mnada wa ile nyumba. Basi jamaa wakagundua kumbe issueile ilkua serious.

Basi wakashauri iyo nyumba kwakua ishatangazwa inauzwa.
Tufanye chini juu, tuinunue sisi wenyewe Kisha tumrudishie jamaa ili bimdg wake aendelee kuishi mle mle ndani maana akinunua mwngn. mkewe atafukuzwa arud kupanga afu itakua aibu Tena kwa jamaa yetu uyu.

Basi kweli siku ya mnada, Pesa ikachangwa na kulipwa cash nyumba ikanunuliwa na sisi wenyewe. Baada ya mnada tukakutana tena bar kula kilaji na tukampa nasaha zetu wapi alikwama ajirekebishe na kumkabidhi documents zote za nyumba yake tulizopewa na bank ili akaendelee kuishi salama na bimdg wake. Ila apambane sana ile pesa atairudisha kidg kidg akishatengamaa kiuchumi.
Akasema sawa.

Sasa ikiwa bado anastruggle kiuchumi zile pesa anazodaiwa hajarudisha hata Mia mbovu,
Mwez wa 12 mwaka jana brother yetu uyu uyu akafanya Tena Lile tukio la kwenda kumuoa mchumba wa mwenzetu mmoja (Dogo) kama mke wa tatu.
Ambapo Dogo uyu uyu alishiriki pia kwny kumlipia pesa ya nyumba yake kwny mnada wa benki.
(Kisa chake nilishakileta hapa tayar)

Sasa Jana asbh
jamaa angu wa karibu sana (yule wa sheli) ni mmoja wapo wa wale tuliolipia ile nyumba ya mnada wa benki kanipigia akinieleza kwamba MKE mdg wa brother kamfata kazin kwake akimueleza kwamba jamaa yetu ile nyumba kaiuza na sahv kahamishiwaa nyumba ya kupanga mtaa flani.

Dah! Taarifa zile zilipotufikia, wote tukabaki na mshangao. Ikabidi Jana asbh Iyo Iyo na uyu jamaa yangu Ikabidi twende kule kule kwnyw nyumba tukashuhudie asimayo uyu mwanamke. Isije ikawa Ni uongo.

Kufika Ni kweli,
Kuna Watu wengine wanaishi pale, ikabidi tuwataarifu wenzetu wote tuloshiriki kuilipia iyo nyumba. Tukakubaliana kwamba jion yake tukutane na uyu jamaa yetu tumuulize kinaga ubaga Nini kafanya aiuze.

Basi jion tumefika bar, tukasubiri mtu hatokei. Tumepiga bia mpk tukaondoka mtu hatokei. Mara Yuko bize tupange siku nyingine. Ikabidi tuazimie kwamba uyu jamaa Ni mjeuri. Na sisi tumfanyie ujeuri.

Leo hii asbh tumemfungulia mashtaka polisi ya kauza nyumba isiyokua Mali yake kihuni na kamatwa kawekwa ndani.

Ule mda anakamtwa,
Katulaani Sana na kutukana matusi ya kila Aina,

MDA SI mrefu tukiwa polisi maaskali wakasema kwa maana wote Ni marafiki sio vema tukimfunga mwenzetu.
Stori ilivyo Uyu jamaa yetu huenda anamatatizo sana anahitaji kusaidiwa kisaikolojia . Ni vema Tukakae nae tuongee nae vizur arudishe hizo pesa alizouza Iyo nyumba maana tayar sio Mali yake Tena Japokua documents tulimrudishia kimakosa.
Jamaa akatolewa akakiri asiwekwe ndani yanazungumzika tukaongee nje ya polisi. Basi tukasema sawa.

Tumetoka polisi, tumerudi baa kujadiliana inakuaje. Jamaa yeye kaja na ndugu zake wakiume na wakike.

Kiukweli hali ya hewa ikawa imechafuka pale, Mwafaka ukashindikana maana ndugu zake wanaongea kwa mihemko zaidi.

Tukaona hiki kikao Bora kife, tukaondoka pale.

Ile tukaondoka,
Jamaa na ndugu zake wakaanza kuporomosha matusi, lugha zisizofaa na malalamishi kibao

Wanasema tulichokifanya sio undugu.
Kwamba tumekua tunaingilia mgogoro wake na mkewe kisa mke wa pili na watatu hawaelewani.
Eti sisi tumechagua kua upande wa MKE wa pili
Wanasema tulichokifanya kwake Ni kumdhalilisha,
Wanasema Kama urafiki ni Bora ufe,
Wanasema tunamnyanyasa kusudi kisa alioa mchumba wa rafiki yetu, eti tuna nongwa
Wanasema tulishindwa Nini kuwaona wao kama ndugu Kama ndugu yao alikua hatoi ushirikiano, Tukawaambia Mbona akiwa na matatizo yake nyie hatuwaoni mkishiriki. Nyumba mpk inauzwa hamjatokea Leo mnajifaya mnampenda Sana ndugu yenu.

Jamaa kaondoka na ndugu zake Ila kasema Yuko tayar kwenda jela sisi ni wanafiki, wenye wivu natunamuonea kijicho kisa kamuoa mchumba wa uyu Dogo
Wanarudisha nyuma kwamba ndo maana wote pale ile harusi yake na mchumba yule wa Dogo wote tuligoma kushiriki.
Hii tunamtafutia TU sababu.

Eti kisa Dogo nae alikuepo pale

Wkt kiuhalisia suala Lile la ugomvi wao na dogo Wala halikua ajenda yetu,
suala lililokuja mezani Ni nyumba TU. Dogo Yuko pale maana nae amechagia kwenye ile nyumba siku ya mnada wa benki.

Yaani
Ni kana kwamba Hawa ndugu pamoja na uyu brother wanajaribu kuhamisha mjadala wa nyumba, kuhusianisha na mgogoro wa kimahusiano na dogo

ila Sisi hayo yote tumeyapokea.

Ila tulichoazimia Ni kumfungulia mashtaka kwa kuuza Mali isiyokua ya kwake.

Na tushaongea na polisi kua muafaka umeshindikana, uyu kesho tunaazimia akamtwe awekwe ndani kesi iende mpk mahakamani nyumba ile irudi.

Sijajua tutakua tumekosea sana au Kama Kuna mahali pa kushaur pia tunaomba kwa dhati USHAUR wenu khs uyu mwenzetu maana tumembeba sana ila HABEBEKI

Nnachokiona
Kuzidi kumbeba uyu jamaa Ni Kama kubeba furushi la misumari mgongoni, yaani tunazidi kuumia sisi wenyewe

Natanguliza shukran wakuu
 
KESI NI NYINGI Mpaka zinatia uchovu kusoma ila mtoa mada unaonekana wewe ni mpuuzi sana kwahiyo mtu anakufanyia matukio yote hayo wewe bado umemkumbatia tu?? Takataka kabisaa wahenga wanasema KIKULACHO KINGUONI MWAKO .....Endelea kumkumbatia huyo bulaza akupige matukio mpaka siku akili itapokukaa sawa
 
Ndefu mno, nimesoma tu hadi kisa cha nne na nikapata tu conclusion kwamba piga chini rafiki mzigo huyo...

Huwezi kuwa na rafiki ambaye wewe ndiye mwenye kupata hasara muda wote...
 
Yaani mnamchangisha mtu Bado anaenda kuoa mademu zenu

Mm ningekuwa mmoja wa marafiki zenu hata mia siwezi changia acha nyumba hiuuzwe akili ikae sawa

Huyo ujinga wa kuchangia muhuni Kama huyo siwez fanya ktk serekali hii ya mam SSH
 
Uyu Jamaa kwa usaliti ule aliotufanyia tuliamua TU kumchunia Kama hatuoni.

Ila Sasa naona suala la nyumba analitumia Kama kichaka Cha upuuzi wake ule Ili kutuhamisha kwny mada
 
Woi sasa rafiki kama huyo mnamurndekeza wa nini, awekwe ndani akajifunze ndo aome kama hao ndugu zake watamsaidia.
Kinachonisikitisha,
Uyu jamaa tumeishi nae miaka mingi Sana hapa mjini. Kwenye shida na Raha.

Matatizo yake yote,Anakimbilia kwetu.

Ila linapotokea hili la kumuweka ndani, Hawa Hawa ndugu zake wanajifanya wao ndo wanauchungu nae Sana.wanakuja front kutushambulia sisi.

Upuuzi wa wapi huu
 
aisee watu tumetofautiana viwango vya kuvumilia ujinga. mkuu ww una kiwango kikubwa sana cha kuvumilia upuuzi me nisingeweza aisee.

ni snitch huyo rafikiyo.
Uyu jamaa ni mzigo Sana kiukweli,
Na usipomsaidia analalama kwamba hatumsaidii wkt tumetoka nae mbali na yeye ndo katufundisha biashara.

Yaan ni mlalamishi na Hana jema hata kidogo.
 
Naombeni ushauri wakuu,

Ni Hivi,
Nakumbuka Kuna kipind niliwahi kuleta humu kesi ya Brother yetu mmoja (mkubwa kiumri) kumuoa mchumba wa miaka mingi wa rafiki yetu (mdg kiumri) Kama MKE mdogo.
Sasa hii ya leo, rafiki nnaemzungumzia Ni uyo uyo jamaa.

1. KESI YA KWANZA,
Nikiwa dukan KWANGU nauza, brother uyu kanipigia Simu anaitaka bidhaa flani. Nikampa Bei kwamba atanipa laki 9 Maana sokoni kuiuza Ni mil 1 net.
Akalalamika Bei ni kubwa namuuzia,kwamba sio ya mteja, nakwenda kutumia yy mwnyw Tena dukani kwake.
Kwakua ni mfanyabiashara mwenzangu afu rafiki yangu, Tena anakwenda kutumia mwnyw basi sikuona haja ya kumuuzia kwa faida.
Nikamwambia Basi utanirudishia laki 7 yangu Maana ww mwnyw Bei ya kuagizia unaifahamu.
Akasema "sawa"
Akatuma mtu akaja kuichukua, MDA si mrefu Akanambia inachangamoto kdg Kwny kuiset ikae vizur.
Nikamwambia kaka leo Niko mwnyw ofsni, Sina wa kumuachia.
ila usiwe na shaka, nkifunga ntapitia ofsn kwako jion nikusetie mwyw ikae sawa. Akasema POA.
Jion nmempitia dukn kwake kwenda kuiset, ananambia
"Dah! Kaka samahan kwa usumbuf, unajua ule mda Niko nahangaika kuiset nikapata mteja wa mil moja nikaiuza pale pale"
Nikamwambia, "Basi Jambo la heri"
Tukaagana maisha mengine yakaendelea.

Basi baada aya siku 2 yake Nikiwa ofsn nikiwa naangalia baadhi ya wateja walioweka Oda zao, niwakumbushe waje kuchukua mizigo.
Nikampigia mteja mmoja akanambia,
"Kaka ule mzgo nilishapata mbona, ulikataa kuniuzia kwa laki 9, nmeshachukua tayar siku ile ile kwa flan (uyo brother niliemuuzia) kwa sh.laki 8"

Dah! Nilipatwa na mshangao Sana maana Iyo Siku anayosema ndo siku nmemuuzia uyo jamaa yangu, afu jamaa anauzaje Bei ambayo hata sokoni haipo?
Nilipompigia akanambia uyo mteja muongo, huenda akakulaghai ili uwe unamuuzia Bei pungufu. Uku kwangu kalipa mil. 1 cash. Basi nikamuelewa ikawa imeisha hivyo.

KESI YA PILI,
Kuna chombo nilikua Nini miezi miwili TU tangu nikinunue alikuja kuazima kwangu kwamba anaenda shambani kwake mkoani kwa wiki 2, nikampatia.
Ile Kurudi ananirudishia ila akanambia Kaka Kuna sehem kiliharibika anaomba sana radhi. Basi nikamwita fund Wang akague kujiridhisha.
Fund akanambia kwa jins kilivyo haribika, Ni changamoto sana kukitengeneza maana spea yake itabidi iwe ya kuchongea, orijino huwez KUPATA kwa Sasa hapa bongo na hali Hii ya Corona.

Nikaona huu utakua usumbufu Sasa.
Basi nikamwambia jamaa kwakua yeye bado shughuli zake Ni endelevu uko shamban, na.mimi sikitumii mara kwa mara kwann asinirudishie nusu gharama yake yake ya sokoni,akakitengeneze mwnyw ili akimiliki moja kwa moja.
Jamaa akafurah na kweli baada ya wiki moja akaniletea ile pesa cash , nikamkabidhi nyaraka zake na maisha yakaendelea.

Miez miwili baadae, nmehudhuria harusi fulani parking. Nikakiona kile chombo anacho jamaa mmoja tunafahamiana tuliwahi kufanya biashara flani miaka ya nyuma sana. Basi nikamsifia chombo chake kizur, akambia kanunua Hapa Hapa bongo tena Kias kadhaa (robo tatu ya Bei ya kipya) . Nikamwambia bei ya kutupa kabisa hii ebu nikitest kidg. Kutest kimekaa vizur Lile tatzo la mwanzo hamna tena na kimeboreshwa Sana ndani na nje yake.

Nikamuuliza kakinunua hivyo hivyo au kakiongezea manjonjo?. akasema kakinunua hivyo hivyo. Basi ikawa imeisha hivyo. Ila nikajiuliza inakuaje rafki yangu anauza haraka Hivi na afu hata hajanambia? Hii sio fair.

Basi Siku Moja mkewe mkubwa kaja ofsin kwangu kuchukua bidhaa flan, bas ktk kunisimulia habar za maendeleo ya shamban kwao nikachomekea stori ya kile chombo kua vipi mlifanikiwa kukirekebisha Lile tatizo.

Akanambia Mbona fundi flani (yule yule fundi wangu) alirekebisha, akakarabati Tena na kikaa vizur sana na ikauzwa wiki ile ile pesa nzur sana Kia's flani na pesa waliopata ndio wamenunulia mashamba mengine ya kulima Tena mwakani. Basi nikamsifia afu Nikabakiwa na maswali.
Inamaana nilipewa USHAUR wa uongo na fundi wangu kwamba hakirekebishiki kirahisi au?
Sasa uyu Mbona kauza kwa faida kubwa kuliko niliyomuuzia na hakunambia?

Anyway, nikamtafuta fundi kumuuliza imekuaje kuaje, fundi akanambia kwamba yeye aliitwa kufunga tu spea maana jamaa tayar spea alikua nayo pale pale kwake.
afu akapewa kazi nyingine ya kuibadilisha muonekano ivutie zaidi maana ashapatikana mteja tayar anaitaka.
Kwaiyo yeye alifanya TU kazi yake. Basi nikaachana na fundi .

Nikamcheki brother,
akanambia nimsamehe Sana alikua na mkopo benki anadaiwa kwaiyo aliiuza haraka kulipa Deni la mkopo.
Nikamtafuta mkewe mkubwa nikamuuliza khs Deni, akakataa kata kata kua hakukua na Deni Wala Nini.
Basi nikajua jamaa kanifanyia uhuni, nikampigia tena akanipa MAELEZO hayaridhishi anang'ang'ana nimwambie aliesema Hana Deni kwanza Ni Nani uyo.

Nikasema yaishe nmekuelewa maana kwa jinsi alivopanic nikaona nikisema Ni mkewe mkubwa ntawaingiza Kwny mgogoro.
Ikabidi niliache Kama lilivyo ila akili yangu ikanambia uyu Kuna namna kanihujumu au Kama Ni Deni kweli POA TU, Haina shida.
Ikawa imeisha hivyo.

KESI YA 3,
Brother yangu uyu alikua na saiti yake haijakamilika anajenga lodge ya vyumba 12.
Basi uku kwangu kuna material zangu za ujenzi zilibaki (nondo, square pipes, na bati geti, welding sticks na black pipes) Akaniomba nimuazime akimbize ujenzi wake aanze kupiga Ela haraka ila siku nikizihitaji MDA wowote atanipatia. Nikasema sawa, nikampatia.

Baada ya MDA tukaenda site kwake tukakuta kasimamisha ujenz,nkamuuliza tatizo nn akasema biashara zimeyumba kiasi. Basi nikamshaur akomae kwnz na biashara maana huu ujenz upo mdg mdg atamaliza. Akasema sawa.

Sasa kuna kipind nikaja kuibiwa dukan KWANGU, baada ya ule wizi ikanilazimu kukarabati na kuimarisha ofisi yangu. Basi nikamuomba material zangu zile nilizomuazimisha anirudishie nikarabati ofisi yangu.

Akanambia zile material hazipo ameshaziuza, nikamwambia Mbona unakosea Kaka unauzaje kitu ulichoazimisha ukatumie mwnyw Hii tabia sio nzuri na Sipendi. Akaomba radhi ila akasema hakijaaribika kitu atanipatia pesa nikanunue nyngn. Nikasema sawa.

Kweli akaingiza pesa, ila changamoto akanirudishia pesa ya thaman ile ya mwanzoni vinauzwa kabla Bei hazipanda. Nikamuuliza inakuaje akasema Kaka iyo ndio pesa niliyouzia vitu ukinicharge zaidi unakua Kama Unanikomoa. Kwa Sasa Sina pesa kabisa.

Anyway, nikapotezea
Ila kiukweli nilichukia Sana maana niliongezea Zaid ya laki 4 juu kwenda kununua vipya kwa wakati ule ikiwa Ni nje kabisa ya Bajeti yangu. Ikawa imeisha hivyo.

KESI YA NNE,
Nilikuja kusafiri kwa wiki 2 kupakia mzgo wa ofisi, niliporudi breki ya kwanza ni kukagua hesabu za mauzo dukan kipind chote nilichokua sipo.

Kuna mahali nikakuta wameuza vitu kwa Bei ya hasara mno, Nikauliza imekuaje. Kijana ananambia Hivi vitu alikuja kuchukua rafiki yako flani mfanya biashara mwenzio (uyu jamaa angu) alisema yeye huwa unamuuzia Bei iyo na kwakua ulkua upatikani tukamuuzia hivyo hivyo TU.

Dah! Nilichoka maana Iyo bei hata kwa mzalishaji haipo na nimeingiliwa Sana.
Ikabd kumfata jamaa. Akajitetea kua alkua hajui Kama Bei zimepanda. Nikamwambia sio kweli maana Bei ulochukulia mzgo hata tunakoagiza hawauzi hivyo.

Akajitetea kua labda alikua na mawazo MDA ule ananunua.
Nikamwambia iyo pesa ilopelea nitakudai, akasema POA nitailipa.

Sasa deni lile likakaa MDA mrefu sana halijalipwa, kuna siku ikapelea bidhaa Moja kwangu, nikampigia akasema anayo. Nikamwambia Basi mpe wa kirikuu ailete kuna mteja anaisubiri Hapa. Akafanya hivyo.

Mteja alivonilipa pesa, nikaitia Kwny droo yangu na kumlipa kirikuu elfu 10 yake ya usafiri na kumwambia aende zake.

Jamaa akanipigia Mbona sijampa Ela yule wa kirikuu, nikamwambia nmeikata kwny Lile Deni letu la siku ile na nmebaki nakudai elfu 70.
Jamaa alilalamika Sana kua sijamtendea fair,
nikamwabia , brother ilo deni MDA ulkua mrefu. Afu umekausha unahisi nmesahau. Akalalamika Sana hata sikujali na maisha yakaendelea.

KESI YA TANO,
Kuna mzee flani Ni dreva kirikuu anapaki mitaa Hii hi ya dukan kwangu. tunamtumia Mara kwa Mara kupeleka mizigo ya wateja wetu,

Basi kuna bidhaa Moja anaipenda sana pale dukan na kila akiiona mate yanamtoka Sana anataka ampelekee mkewe nyumbani ila anabaki kulalamika akisema namkazia mno kumpatia kwa 270,000.
Namwambia kua Bei yake halisi Ni 350,000 ila yeye nmeshamwambia ntamuuzia kwa 300,000. anaishia kulalamika kua ana 270,000 haiongezeki hata Mia. Nikamwambia wee iache cha muhimu haiozi basi watanunua wengine. Basi ikawa hivyo.

Kuna siku brother angu uyu akaja dukan kwangu kua anaihitaji iyo bidhaa, nikamwambia wewe nipe 300,000 wewe kauze 350,000 au zaidi ya hapo utajua mwenyewe.

Akanambia hapana sio ya kuuza, niuzie kwa 200,000 Bei tunayonunulia wote kwa JUMLA maana nampelekea wife wangu mdg nae akafurahi nyumbani. Nikasema hapana wee Ni muongo unaweza sema unampelekea wife kumbe unaenda kuiuza kwa faida. Ndo tabia yako.

Akasema namfikiria ndivyo sivyo,
Nikamwambia Hapa mpk nipate uthibitisho wa shemej mwnyw ndo ntakuuzia Bei hii.
Basi nikampigia shemej, akasema kweli taarifa anayo. Basi akanipa laki 2 cash nikampatia bidhaa akaenda nayo.

Sasa baada ya siku Kama 5 mkewe mdg kapitia dukan kwangu kunisalimia Kuna duka la jiran alkikuja kununua mahitaji yake.
katika kusalimiana akanambia kwamba alichomfanyia uyu ndugu yangu hajakipenda, nikamuuliza Kipi. Akasema ile bidhaa alomnunulia kipind kile ilikaa siku mbili TU pale nyumbani Kisha akaiuza tena.
Nikamuuliza ya kweli Ayo, akasema ndio Ni serious. Nikamwambia Basi nitaonana na anambie tatizo nn.

Sasa ktk Yale maongez kijana wangu wa dukan akawa anayasikia, alivotoka tu yule mwanamke kijana akanambia analosema uyu mama Ni kweli kabisa 100% na ile bidhaa kamuuzia yule mzeee flan dreva kirikuu.
Kijana akasema kua Yule mzee alimwambia kua sisi tulikataa kumuuzia kwa 270,000 kaenda kwa jamaa kauziwa kwa 250,000.

Baha nzur mzee Hakua mbali,
Nikamwita yule mzee kumuuliza, akakiri kweli alinunua kwa jamaa kwa 250,000.

Dah! Kusikia Yale Maneno nilichoka sana, ikabidi kumpigia jamaa jioni tuonane baa flani nna maongezi nae.

Nikawapigia marafiki zangu wengine wanne nikawawaleza matukio yote ya mwanzo, Basi wakaashaur jion iyo nao wawepo ili tuambizane mbivu na mbichi. Uyu mwenzetu Anachofanya sio kizur

Jioni imefika tumekutana baa,
Katikati ya kilaji tukaingia kwny mada, nikaeleza kesi zote kuanzia Namba 1 mpaka Namba 5.

Wao wakashaur yaishe ila jamaa awe TU muungwana, aweke wazi maana anachokifanya Ni kuwagawa wateja.

Yaan ionekane kwangu nauza Bei kubwa, ila wakienda kwa jamaa wanauziwa Bei ndogo sana wkt mzgo huo huo umetoka kwangu kwa kigezo cha urafiki na anakwenda kutumia mwnyw. Huku Ni kurudishana nyuma kibiashara maana Bei tunazouziana sisi hazina faida. Tunalindana TU kila mmoja wetu apate.

Ile kesi ya chombo, ikaonekana kweli jamaa alikiharibu kusudi akiboreshe ili akiuze kwa Bei ya faida kwa kunizunguka pamoja na fundi wangu, hakua na Nia yakukitumia Kama alivyokua mwanzo na kushukuru.

Kwenye vifaa vya ujenzi ikaonekana kumbe hakua na kazi navyo wkt ule, tayar alishapata mtu anavihitaji kwaiyo alipovichukua tu kwangu alienda kuviuza kwa mtu Moja kwa Moja na sio kuvitumia Kama alivyoomba. Ikaonekaa huo Ni uhuni. Ni Bora TU angesema kapata mteja wore tujue tunafaidika vipi. Na sio achukue kwa mgongo wa kutumia kumbe Lengo Ni kuuza.

Basi jamaa yote akaomba radhi yakawa yameisha. Hivyo. Tukagonga bia tukaenda majumbani kwetu.

KESI YA 6,
Kuna siku Uyu jamaa yangu kaja anashida ya pesa Kias kadhaa anaazima akarejeshe mkopo wa benki mambo yameyumba kabisa, nyumba ya bimdg wake itapigwa mnada MDA wowote.

Sasa kutokana na kwamba mzigo ulikua mkubwa nikamwambia MDA ulobaki Ni mchache Sana afu mambo ya uchumi sio mazur Ni Bora tukachangia na jamaa zangu wengine tujue tunakutoaje hapo mwenzetu. Akasema sawa.
Basi tukapanga jion yake tukutane bar na jamaa zangu 5 JUMLA 6 tujue tunamkwamuaje uyu.

Sasa kabla hatujaenda bar, baadhi ya jamaa wakawa wanaonyesha mashaka yao khs ukweli wa Hilo suala. Akapigiwa bi mdg, kweli akakiri kulijua Hilo suala anatusihi tumsaidie mme wake.
Basi jamaa wakakubali.

Ila Pale pale Kuna jamaa wakawa wanakiri kua jamaa Ni msumbufu kwny suala zima la ulipaji wa madeni , Kuna mtu na akakiri hajawai mrejeshea mil. 5 inamiaka Zaid ya 6 aliazima, amekausha anahisi kasahau. Tutamuaminije kwa kesi Kama Hii?
Basi tukaona haina haha ya kurudisha ya nyuma, hebu tukamsikilize.

Basi tukakubaliana, twende tukakonane nae ila haya mapungufu yote yanayosemwa hapa Ni lazima tumwambie ajue na Kama ni maisha ya ujanja ujanja basi hayatomsaidia chochote.

Jion kweli tukafika na tukakubaliana tutamsaidia, ila Sasa baada ya hapo kila mtu akaonesha bado anamashaka na yeye.

Zile ahadi za kutoa mchango zikawa zinasua sua mpk siku ya tuliposikia tangazo la mnada wa ile nyumba. Basi jamaa wakagundua kumbe issueile ilkua serious.

Basi wakashauri iyo nyumba kwakua ishatangazwa inauzwa.
Tufanye chini juu, tuinunue sisi wenyewe Kisha tumrudishie jamaa ili bimdg wake aendelee kuishi mle mle ndani maana akinunua mwngn. mkewe atafukuzwa arud kupanga afu itakua aibu Tena kwa jamaa yetu uyu.

Basi kweli siku ya mnada, Pesa ikachangwa na kulipwa cash nyumba ikanunuliwa na sisi wenyewe. Baada ya mnada tukakutana tena bar kula kilaji na tukampa nasaha zetu wapi alikwama ajirekebishe na kumkabidhi documents zote za nyumba yake tulizopewa na bank ili akaendelee kuishi salama na bimdg wake. Ila apambane sana ile pesa atairudisha kidg kidg akishatengamaa kiuchumi.
Akasema sawa.

Sasa ikiwa bado anastruggle kiuchumi zile pesa anazodaiwa hajarudisha hata Mia mbovu,
Mwez wa 12 mwaka jana brother yetu uyu uyu akafanya Tena Lile tukio la kwenda kumuoa mchumba wa mwenzetu mmoja (Dogo) kama mke wa tatu.
Ambapo Dogo uyu uyu alishiriki pia kwny kumlipia pesa ya nyumba yake kwny mnada wa benki.
(Kisa chake nilishakileta hapa tayar)

Sasa Jana asbh
jamaa angu wa karibu sana (yule wa sheli) ni mmoja wapo wa wale tuliolipia ile nyumba ya mnada wa benki kanipigia akinieleza kwamba MKE mdg wa brother kamfata kazin kwake akimueleza kwamba jamaa yetu ile nyumba kaiuza na sahv kahamishiwaa nyumba ya kupanga mtaa flani.

Dah! Taarifa zile zilipotufikia, wote tukabaki na mshangao. Ikabidi Jana asbh Iyo Iyo na uyu jamaa yangu Ikabidi twende kule kule kwnyw nyumba tukashuhudie asimayo uyu mwanamke. Isije ikawa Ni uongo.

Kufika Ni kweli,
Kuna Watu wengine wanaishi pale, ikabidi tuwataarifu wenzetu wote tuloshiriki kuilipia iyo nyumba. Tukakubaliana kwamba jion yake tukutane na uyu jamaa yetu tumuulize kinaga ubaga Nini kafanya aiuze.

Basi jion tumefika bar, tukasubiri mtu hatokei. Tumepiga bia mpk tukaondoka mtu hatokei. Mara Yuko bize tupange siku nyingine. Ikabidi tuazimie kwamba uyu jamaa Ni mjeuri. Na sisi tumfanyie ujeuri.

Leo hii asbh tumemfungulia mashtaka polisi ya kauza nyumba isiyokua Mali yake kihuni na kamatwa kawekwa ndani.

Ule mda anakamtwa,
Katulaani Sana na kutukana matusi ya kila Aina,

MDA SI mrefu tukiwa polisi maaskali wakasema kwa maana wote Ni marafiki sio vema tukimfunga mwenzetu.
Stori ilivyo Uyu jamaa yetu huenda anamatatizo sana anahitaji kusaidiwa kisaikolojia . Ni vema Tukakae nae tuongee nae vizur arudishe hizo pesa alizouza Iyo nyumba maana tayar sio Mali yake Tena Japokua documents tulimrudishia kimakosa.
Jamaa akatolewa akakiri asiwekwe ndani yanazungumzika tukaongee nje ya polisi. Basi tukasema sawa.

Tumetoka polisi, tumerudi baa kujadiliana inakuaje. Jamaa yeye kaja na ndugu zake wakiume na wakike.

Kiukweli hali ya hewa ikawa imechafuka pale, Mwafaka ukashindikana maana ndugu zake wanaongea kwa mihemko zaidi.

Tukaona hiki kikao Bora kife, tukaondoka pale.

Ile tukaondoka,
Jamaa na ndugu zake wakaanza kuporomosha matusi, lugha zisizofaa na malalamishi kibao

Wanasema tulichokifanya sio undugu.
Kwamba tumekua tunaingilia mgogoro wake na mkewe kisa mke wa pili na watatu hawaelewani.
Eti sisi tumechagua kua upande wa MKE wa pili
Wanasema tulichokifanya kwake Ni kumdhalilisha,
Wanasema Kama urafiki ni Bora ufe,
Wanasema tunamnyanyasa kusudi kisa alioa mchumba wa rafiki yetu, eti tuna nongwa
Wanasema tulishindwa Nini kuwaona wao kama ndugu Kama ndugu yao alikua hatoi ushirikiano, Tukawaambia Mbona akiwa na matatizo yake nyie hatuwaoni mkishiriki. Nyumba mpk inauzwa hamjatokea Leo mnajifaya mnampenda Sana ndugu yenu.

Jamaa kaondoka na ndugu zake Ila kasema Yuko tayar kwenda jela sisi ni wanafiki, wenye wivu natunamuonea kijicho kisa kamuoa mchumba wa uyu Dogo
Wanarudisha nyuma kwamba ndo maana wote pale ile harusi yake na mchumba yule wa Dogo wote tuligoma kushiriki.
Hii tunamtafutia TU sababu.

Eti kisa Dogo nae alikuepo pale

Wkt kiuhalisia suala Lile la ugomvi wao na dogo Wala halikua ajenda yetu,
suala lililokuja mezani Ni nyumba TU. Dogo Yuko pale maana nae amechagia kwenye ile nyumba siku ya mnada wa benki.

Yaani
Ni kana kwamba Hawa ndugu pamoja na uyu brother wanajaribu kuhamisha mjadala wa nyumba, kuhusianisha na mgogoro wa kimahusiano na dogo

ila Sisi hayo yote tumeyapokea.

Ila tulichoazimia Ni kumfungulia mashtaka kwa kuuza Mali isiyokua ya kwake.

Na tushaongea na polisi kua muafaka umeshindikana, uyu kesho tunaazimia akamtwe awekwe ndani kesi iende mpk mahakamani nyumba ile irudi.

Sijajua tutakua tumekosea sana au Kama Kuna mahali pa kushaur pia tunaomba kwa dhati USHAUR wenu khs uyu mwenzetu maana tumembeba sana ila HABEBEKI

Natanguliza shukran wakuu
We ni zwazwa...

Ila nasikitika tunacomment wakati ni story ya kutunga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom