Upungufu wa Mafuta Tanzania - Ubabe wa EWURA na TRA

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,790
Kumekuwa na upungufu mkubwa wa mafuta ya Petrol, Diesel na mafuta ya Taa.

Na hii imesemekana ni kutokana na EWURA kupunguza bei ya mafuta siku chache zilizopita.

Serikali kwa kupitia EWURA wameamua sas kusitisha usafirishaji wa mafuta nchhi za nje (TRANSIT GGODS) ili yatumike hapa nchini, kitu ambacho kinaleta utata kwani hayo mafuta ya TRANSIT siyo mali ya Serikali bali yanapaswa kupelekwa nchi husika. Lakini Serikali wanatumia ubabe katika suala hili badala ya kutafuta mbinu nzuri ya kuondoa upungufu wa mafuta nchini.

Ubabe kama huu hausaidii kwani inaweza kusababisha nchi za Zambia, Rwanda, Congo, Burundi ambao wanapitisha mafuta hapa Bandari zetu wakaamua kuhama Bandari za nchi mfano Mombasa au Beira kitu ambacho kitainyima mapato TRA kwa kiasi kikubwa.

Ni wakati kwa Serikali yetu kutafuta mbinu mpya au waifufue TIPER ili wasafishe mafuta na kupunguza hali kama hii ya upungufu isitokee.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
serikali
imesema kuna mafuta ya kutosha kupitia kwa katibu mkuu wizara ya
nishati na madini na kuwataka wauza mafuta kuhakikisha mabasi yanayoenda
mikoani wanapatiwa mafuta naona makampuni makubwa yenye lessen za
mafuta yanawahujumu wananchi. source:taarifa ya habari ITV
 
heh, karibu mgeni, karibu hadi ndani, vua viatu, lete mzigo tukupokee, karibu jamvini..... subiri kidogo tukuonyeshe jiografia ya mahali ulipo... choooni ni kulee nyuma, jikoni ni kuleee nje kabla ya kufika chooni, wanaume wanalala chumba cha upande huu na wanawake cha upande wa kulia, watoto wanalala hapa jamvini tukiinuka.... SASA PAMOJA NA MAELEKEZO YOTE HAYO TOKA KWA WENYEJI, BADO TU UMEENDA KUKOOJOA JIKONI????????
 
Acha kukurupuka na ulimbukeni wa kuchangia mada hata usizozijuwa,kama huna cha kuchangia tulia kwako na pumba zako!
 
Hii serikali bwana, maneno maneno tu, kama kuna mafuta ya kutosha si iyasambaze yenyewe kutoka kwenye bohari zake? Kama wanaongelea mafuta ambayo yanasambazwa na makampuni binafsi basi wajue kuwa wanaongelea mambo ambayo yako nje ya uwezo wao!!!!!
 
je ni kweli kuna watu wanahujumu huduma ya nishati ya mafuta nchini kwetu,kutokana na mafuta kuhadimika sana
 
Acha kukurupuka na ulimbukeni wa kuchangia mada hata usizozijuwa,kama huna cha kuchangia tulia kwako na pumba zako!

Punguza jazba mkuu.
Unakuwa mkali kwa kuelezwa jambo.
Kama halikukupendeza usingehangaika kumjibu.
Ungenyamaza tu
 
Wanajamvi

Naomba niulize hivi hii serikali ni dhaifu kiasi hiki cha kuchezewa na wafanyabiashara wa mafuta namna hii?????

Yaani watu wa D'Salaam wamekuwa wahanga wakubwa wa tukio hili la uhaba wa mafuta na kwa muda serikali imekuwa ikikana juu ya uhaba wa mafuta!!!!

Tatizo ni mafuta au bei?????

Waswahili wana msemo wao wa kifedhuli, kweli ukimfanya mbwa awe kiongozi wako atakupeleka mpaka jalalani!!!! Naamini sasa wafanyabiashara wa mafuta wameipeleka serikali jalalani.

Kama hamuwezi kucontrol uhaba wa mafuta pandisheni bei ya mafuta tujue kuwa nchi imewashinda na serikali ambayo ina majeshi na silaha za moto imesalimu amri kwa kikundi cha watu ambao hawana hata jeshi lolote!!!!

Hilo ni swali ambalo nimejiuliza baada ya kuona habari saa mbili ya ITV leo.
 
Nje ya mada, kesho JK nasikia yupo Arusha huku karibu watumishi wote wa serikali kuu hawajapata mishahara ya Oct kisa Epicor 9 na bado anacheka haaaah!!!!

Epicor 9 ni mbwa mwingine ambaye serikali imeruhusu awe kiongozi wake,

Karibuni tuchangie wajameni.
 
Ukweli ni kuwa mafuta hakuna..leo nimepita mkoa mpya wa geita vituo vyote petrol hakuna!diesel kituo kimoja tu...halafu useme tuna serikali?sasa hv ni la manyani
 
kazi ya hii serikali ni kile ritz huwa anachangia humu that is it hamna kingine wao ni kufikiri namna gani watabaki madarakani kwa kukandamiza upinzani tuuuuuuuuuuu....hata ukisikiliza bungeni waziri mkuu na mawaziri na ag itaaamini
 
Tatizo la mafuta nchi hii litamalizika mara tu watawala watakapoacha kuyatumia(mafuta) kugharamia shughuli(chaguzi)
za vyama vya siasa. Wafanyabiashara wa mafuta wanakiburi kisicho kifani...kwani enyi watu wenye akili timamu hamuelewi kiburi hicho linatoka wapi?? Kwani unafikiri matokeo ya baba kumgeuza House Girl wake nyumba ndogo ni yapi?? vurugu ndani..watoto na mama watateseka sana...Hivi Jambo hili sio la dharura kujadiliwa na BUNGE letu???
Spika Makinda OKOA Watanzania wanaangamia kwa ukosefu wa mafuta!!! Wacha meno ya BUNGE yawaume hao wahujumu uchumi
 
Nje ya mada, kesho JK
nasikia yupo Arusha huku karibu watumishi wote wa serikali kuu
hawajapata mishahara ya Oct kisa Epicor 9 na bado anacheka haaaah!!!!

Epicor 9 ni mbwa mwingine ambaye serikali imeruhusu awe kiongozi wake,

Karibuni tuchangie wajameni.

ungetaja ni idara zipi maana wengi naowafahamu washalipwa mishahara yao!
 
Kwani Ewura haijapewa uwezo kisheria wa kulazimisha makampuni kuuza mafuta? Tatizo sio makampuni kukataa kuuza mafuta, I guess...tatizo ni kwamba hakuna mafuta ambayo makampuni yanaweza kuyauza. Kwa ufupi ukikataa mafuta ya Congo, Rwanda na Burundi yasiende, hilo halitakuwa tatizo la makampuni ya mafuta....litakuwa tatizo la kupitishia mafuta bandari ya Dar.
 
Ukweli ni kuwa mafuta hakuna..leo nimepita mkoa mpya wa geita vituo vyote petrol hakuna!diesel kituo kimoja tu...halafu useme tuna serikali?sasa hv ni la manyani

Mafuta yapo ila wafanyabishara wameyaficha. Nadhani kuna collution kati ya baadhi ya maofisa wa Ewura na wafanyabiashara wa mafuta kuficha kuamua kuficha mafuta kama Tanesco walivyokuwa wakichonga mgawo ili wapandishe bei. Ukitaka kujua mafuta yapo ngoja wiki ijayo Ewura wakitangaza tu kupanda kwa bei ya mafuta utaona vituo vyote vinauza mafuta na utajiuliza yalisafirishwa saa
ngapi.
 
What i know mafuta yapo ila EWURA ilikosea kuwa alert new price for this month which ll go up kuliko ya last month!! wanasubili kuuza kwa bei mpya ya juu.Nawaomba EWura wasipandishe mwezi huu tuone nani zaidi wao na govmnt
 
Ni kweli hili tatizo lilianza baada ya kutangazwa punguzo la bei. Wakaamua kuweka mgomo baridi ili kusubiri bei mpya ije.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Conflict of interest kuna makampuni wakubwa wana shares
Maana its common sense mtu ana mafuta ya kutosha alafu hayauzi si mnamfungia tuu to me its a common sense hauzi bse anataka create scarcity apige bei kubwa
 
Kwani Ewura haijapewa uwezo kisheria wa kulazimisha makampuni kuuza mafuta? Tatizo sio makampuni kukataa kuuza mafuta, I guess...tatizo ni kwamba hakuna mafuta ambayo makampuni yanaweza kuyauza. Kwa ufupi ukikataa mafuta ya Congo, Rwanda na Burundi yasiende, hilo halitakuwa tatizo la makampuni ya mafuta....litakuwa tatizo la kupitishia mafuta bandari ya Dar.

Serikali itakuwa inafanya tofauti kwa kuyazuia mafuta ya kwenda nje ili yauzwe hapa. Kwani yale ni mafuta ya Serikali za nchi husika (zambia, congo, burundi na Rwanda)

Kwa kufanya hivyo watasababisha uhaba wa mafuta katiak nchi za nje na pia ni wizi kwani mafuta yale siyo ya serikali ya Tanzania.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom