Ups and down miaka 8 ya kubet (addiction) bila ya mafanikio

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,549
2,989
Ndugu zangu

Kwenye jukwaa hili nimeshuhudia hadithi na mikasa mingi watu waliyokutana nayo kabla na hata baada ya kujiunga mtandao huu mwaka 2014 hivyo kwanza nijipongeze kwa kufikisha miaka 10 kwenye hili jukwaa na miaka yangu hii kumi napenda kutoa stori fupi ya maisha yangu ambayo ni ya kusikitisha niliyaiga kutoka kwa Rafiki yangu mmoja mwaka23/3/ 2017.

MAISHA YA KUBETI

Watu wengi wanaoingia kwenye mikwamo ya ulevi hawaingii kwa kupenda ila mara nyingi huwa ni externally forcing huenda ni vichochezi vya marafiki,mitandao ya kijamii,dhiki na mengineyo.

Nakumbuka nilikuwa ni mtu safi ambaye nilijiapiza kutojihusisha na kamari pamoja utumiaji wa bangi ila la haula bahati mbaya iliyoje kote nimepakanyaga lakini nimeweza kuacha bangi ila siyo kamari ambayo imenicost muda,kuniathiri akili,fedha,magonjwa pamoja na tabia.

Kama hamutambui Magonjwa mengi ya akili,moyo na mabadiliko ya tabia huchochewa na kuanzisha tabia hizi mpya mimi nakumbuka 2016 nilimaliza masomo yangu ya kidato cha 6 kama mtahiniwa wa kujitegemea baada ya kushindwa kulipa ada,namshukuru mungu nilifaulu lakini ndiyo kipindi ambacho niliadapt tabia mbaya ya uchezaji kamari ambapo Rafiki yangu alikuwa ni mwenye kuicheza na kunishawishi sababu alikuwa anapata vishilingi na kwa bahati mbaya maisha yangu mimi toka udogoni ni mabovu pesa ni ngumu kushika hivyo nikasema acha nijitafutie bahati.

Lahaulaaaaa!!!nilijiunga na mtandao wa m-bet nilipigwa kila siku basi ikafika kipindi nikaanza kuhudhuria meridiani pale magomeni mkabala na mwendo kasi kwa siku ya kwanza niliweka 500 nikaweka odd ndogo nikala 4500 nikasema hapa mambo fresh,basi tangu hapo nilikuwa napigwa tu,kila navyopata pesa naenda kuongeza napigwa pesa yote na sikuwahi kuvuka hata kiasi cha 10,000.kuna siku nilibet PM bet nikala 15,000 ebwaa eeeh nikasema nicheze visual throne nikagongwa yote basi tangia hapo napigwa tu.

NIMEPATA KAZI YA KUUZA DUKA(2017)
Mwanzoni kabisa nilipata kazi ya kuuza duka xxxxxx basi ilitokea tu!bahati jamaa wa duka aliniamini sana,ila kwa bahati mbaya kamari ilivunja uaminifu nilikuwa kila usiku nikifunga duka hua naenda kubet thrown visual ya mpira nililiwa pesa ya watu mpaka nikawa najilaumu na kuapa viapo vyote kuwa nitaacha ila wapi!!.

Kibaya zaidi,nilikuwa natumia pesa ya dukani kila siku 20,000-30,000/= kuzani nitarejesha lakini wapi na mshahara wangu ulikuwa 90,000/= ilitokea siku nikafunga duka ili niende kufanya kitu fulani mkononi nilishika 60,000/= sijui ndiyo shetani akanipitia nikajiona naelekea thrown kucheza visual aiseee niligongwa yote yaaani unaweka mpira nyau nyau, dog hamna kitu,namba hamna daaaah toka siku hiyo nikajiapiza tena kuwa sitacheza ila wapi.

siku inayofata jamaa akaja dukani tukapiga hesabu kiasi kama cha 235,000/= kilipungua ndani ya siku chache tu, nikataka kupelekwa polisi ila huku na huku pesa ikalipwa..sikuwa mwenye kupata chochote ila nafsi yangu tu ni ngumu kuacha.

niliachishwa kazi,nilijutia ila niliendelea basi ilitokea home napewa pesa naenda kwenye kamari naliwa alafu nasingizia imepotea dah maisha yalikuwa ni ya kipumbavu sana.

Ukweli nikipiga hesabu ya pesa nilizotumia kwenye kamari naweza kupata 6,000,000/= mpaka kufikia sasa sina hata kiwanja wala chochote nipo nipo na bado nacheza tu.

WADAU MIAKA 8 BILA MAFANIKIO KATIKA KAMARI,MISUKOSUKO YA MAISHA KISA KAMARI

UKWELI BADO NACHEZA JAPO NIMEPEVUKA NIMEACHA MAMBO YA VISUAL ILA NINGELIKUWA RAIS NINGELIFUKUZIA MBALI HIZI KAMPUNI ZA KUBETI SIYO POWA VIJANA WANAKUWA WAGOJWA WA AKILI,MWILI N.K SABABU YA KAMARI

MWISHO UZI USIUNGANISHWE
 
Usiwe na tamaa kwenye kubeti, hii ni rule namba moja. Usitake kushinda fedha nyingi kwa wakati mmoja. Weka fungu dogo, kwa muda maalum likiisha subiri .
 
Betting nilianza 2014 ila kwasasa nimepunguza kwa asilimia 70 u 80 kabisa,kimahesabu pesa nilizopata kwa kushinda tangu nianze inafika milioni 4,ila nilizopoteza zinazidi hiyo.Kiufupi addiction kama pombe,kamari,punyeto, picha za ngono,na madawa zinahitaji nguvu za maombi na Dua kwa kumaanisha ni ngumu kuacha kwa kuzungumza tu.
 
Mimi nilianza 2018 , nilianza Keno na baadaye kuwa addicted wa casino za online.
Nimeliwa zaidi ya milioni 30 nadhani mpaka sasa.
Ila nimekula pia pesa nyingi tu. Ungecheza casino siku moja Moja ungekuwa unatoka na pesa
Vipi tathmini yako betting imekutoa kimaisha au ndio majuto kama mleta uzi? Huko kitaa vijana huwaambii kitu kuhusu kubeti..
 
Betting nilianza 2014 ila kwasasa nimepunguza kwa asilimia 70 u 80 kabisa,kimahesabu pesa nilizopata kwa kushinda tangu nianze inafika milioni 4,ila nilizopoteza zinazidi hiyo.Kiufupi addiction kama pombe,kamari,punyeto, picha za ngono,na madawa zinahitaji nguvu za maombi na Dua kwa kumaanisha ni ngumu kuacha kwa kuzungumza tu.
Kitu ninachowaambiaga wacheza kamari za kisasa kama hii betting ni kwamba kama uliwahi kuijua probability kwenye statistics basi yatosha kuelewa kwamba msingi wake mkubwa ni kwamba mkicheza watu 1000 lazima watu 900 mpaka 950 mliwe ili fedha yenu walau itumike asilimia 20 - 30 kuwalipa hao watu 50 - 100 wanaoshinda. 70% inayobaki ni faida yao baada ya kutoa kodi na running costs. Yaani lazima hayo makampuni yamefanya statistical analysis ya kuona chances of winning Vs losing.. Zamani hata ile kamari ya karata ya keusi kekundu walikuwa wanatumia ujanja na uongo ili uliwe pesa zako.
 
Back
Top Bottom