Upotoshaji wa Juliana Shonza na kundi lake kwa vyombo vya habari...

WanaJF,

Japo sikutaka kujibu hoja ya Shonza; maana si jambo zuri sana kujibu tuhuma ambazo zimetolewa na watu nje ya CHADEMA. Watu ambao hadi muda huu si wanachama wa CHADEMA, lakini kwa kuwa lengo la maadui wa CHADEMA (CCM na vibaraka wake) ni kueneza uongo dhidi ya CHADEMA, Viongozi na wanachama wake basi hatuna budi kujibu uongo huo kwa kusema ukweli.

Naomba nijibu machache yanayonihusu ili kuweka kumbukumbu sawa kwa kuwa uongo unapoandikwa na ukabaki hivyo bila kutolewa ufafanuzi unaweza kusababisha watu wakanukuu kitu ambacho siyo sahihi.

MOSI:
Sijawahi kumchafua kiongozi yeyote na sijawahi kuomba msamaha mahali popote kuhusiana na kumchafua kiongozi yeyote. Nilishawahi kulisema hapa, lengo la propaganda hii ni kutaka kuyumbisha mawazo ya watu na kuwafanya waamini kwamba yote niliyosema huku yalikuwa na lengo la kumchafua mtu. Nasizitiza kwamba kila nilichoandika ni sahihi na kamwe sitaomba radhi kwa lengo la kumridhisha yeyote. Nitausimamia ukweli tu na hakuna maridhiano nje ya ukweli.

Niliomba msamaha kuhusu kushirikiana kwangu na kundi la MASALIA/PM-7 na pia kujibu tuhuma zilizotolewa dhidi yangu kwa njia ya mtandao badala ya kufuata taratibu za vikao.

PILI:
Hoja kwamba nilisamehewa si kweli. Nilipewa adhabu ya Onyo kali na kuwekwa chini ya Uangalizi kwa kipindi cha miezi 12 kama ilivyotangazwa na Mwenyekiti wa vijana kwenye vyombo vya habari na pia mimi binafsi kupokea barua tarehe 11/01/2013.Naelewa taratibu za vikao na naiheshimu katiba ya CHADEMA,kanuni,itifaki na maadili ya CHADEMA.

Tarehe 12/01/2013 niliandika barua ya kukata rufaa na nikatoa sababu ni kwanini siridhiki na hukumu iliyotolewa dhidi yangu.

Nilitekeleza wajibu huu kwa kuzingatia Kanuni, Itifaki na katiba ya chama chetu katika sura ya 5 Ibara ya 2 kifungu cha 4 kama inavyoelekeza juu ya haki za Mwanachama naomba kunukuu ''5.2.4 Kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua za kinidhamu kichama''

Huu ndiyo utaratibu uliowekwa na unaoongozwa ma katiba ya CHADEMA kama hujaridhika na uamuzi uliotolewa kwenye ngazi za chini kuna ngazi za rufaa.kuna kamati kuu, kuna Baraza kuu n.k

TATU:
Hoja ya kuangalia watu wametoka wapi (ukanda) haina mantiki kikanuni, kikatiba na haiwezi kuwa hoja yenye uzito kwa Chama au Taifa linalojali misingi ya haki na maadili. Ni lazima nihukumiwe kulingana na Tabia yangu. Si sahihi kusema nimehukumiwa au kusamehewa kwa sababu ni Mchagga au Mkristu. Vigezo hivi vinatumika na maadui wa CHADEMA tu. Leo tumeshuhudia kigezo kingine cha jinsia kikitumika katika hoja ya Shonza ili kupata huruma (sympathy).

Katika walioenguliwa BAVICHA na mimi ni mmojawapo, hilo halitajwi kwa makusudi maalumu.

Katika adhabu niliyopewa, inalingana na adhabu ya Kasambala na Gwakisa kutoka Mbeya (Kama vigezo vya ulikotoka ni vya Msingi) tujiulize mbona nimehukumiwa na hawa wanapotosha wanasema nimesamehewa? Wote tuna fursa ya kukata Rufaa kwa mujibu wa kanuni niliyotaja hapo juu!

Sikuchagua kuzaliwa kabila fulani. I view it as wrong and unethical to discriminate against someone based on who they are – that is, based on what ethnic background or skin color they are, or any other trait that is beyond one's choice.

NNE:
Sijawahi kutumwa na kiongozi yeyote kuanzisha PM-7 tofauti na viongozi na wanachama walioshiriki kikamilifu ambao niliwataja katika tamko langu lililopita

TANO:
Uchaguzi wa BAVICHA tuligombea tukiwa tunajua kuhusu suala la kadi za BAVICHA na hakuna hata mmoja aliyewahi kuhoji hili. Tumpuuze mtu yeyote anayetaka kubadili kanuni na sheria hasa pale anapoona kuna maslahi yake tu. Tukiruhusu viongozi wa aina hii tutakuwa tunaandaa taifa la hovyo.

Mtu huyo huyo anayejenga hoja ya kitoto kuwa hakuna unachama wa BAVICHA na hivyo kutoa taswira ya kuwa BAVICHA haipo kihalali ndani ya muda mfupi tu anajitangaza kama Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA... Inashangaza!

SITA:
Tuendelee kusonga mbele na tuwapuuze hawa wanaotumiwa kufifisha nguvu ya Mabadiliko kwa kutunga uongo, uzushi na ghiliba ili malengo yatimie. Hawa tuwapimie kipimo kile kile kinachotumika dhidi ya CCM na maadui wa CHADEMA. Waache waendelee na matamko mfu yanayofadhiliwa na maadui zetu akiwemo yule aliyekuwa anatumia nguvu nyingi kudai posho ya wabunge iongezwe hadi kufikia laki 5 kwa siku (na kuibatiza jina-UJIRA WA MWIHA) ili aweze kufadhili uasi dhidi ya CHADEMA.

Naanza mchakato wa kisheria dhidi ya wale waliotoa madai na tuhuma za kuuana kwa kuwa ile ni jinai, zaidi ya hatua za kisiasa ni lazima nichukue hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa vijana wanaotumika vibaya ndan ya mfumo wetu wa siasa.

Mengine nitaachia mamalaka husika na taratibu za Vikao kwa mujibu wa Katiba, Maadili na Itifaki ya Chama.

Yote unayoyafanya hayanisumbui, ila niemgundua kwamba sasa kijana umeendelea kukuwa kisiasa vizuri sana.
Siasa ni mchezo kama michezo mingine, ukizubaa unaliwa na wapinza wako wa nje au wa ndani.
 
Nilishawahi kuuliza ni kazi gani Ben Saanane anafanya nje ya siasa! Ni nani anayemfadhili kwenye hizi harakati zake?

Tafadhari mwenye ufahamu wowote!

Fuatilia post zake, hapa JF na nje facebook ndio utajua kazi yake. Ana kazi maaalum huyo, na kazi yake itaisha baada ya uchaguzi wa ndani wa CDM.
 
Ni ujinga kumuamini Ben saa8, wakati yeye ndo mwanzilishi wa PM7.Nasema tena ni upumbavu uliopitiliza kumuamini huyu jamaa! hana sifa ya kuaminiwa tena.
 
anabiashara zake za kueleweka siyo ukwapuaji wa simu kama kazi ya masalia kama ungekuwa mfatiliaji wa sakata hili hata humu kazi ya ben ameitaja yeye mwenyewe...

Kasema ni consultant, nimejaribu kumwelewa kiasi. Ambacho sijaelewa ni kwamba yeye mwenyewe anapata wapi consultation ya haya anayoyafanya.

Na je ana-offer consultation services kwa CDM leaders?

All in all there is motivation behind this movement, I believe this is not charity job he is doing!!!
 
Huu ndiyo upuuzi wa akina ben na wenzake baada ya kujenga chama mwisho wa siku tunakaa jamvin kujadili migogoro ya chama,there is a need to build a party ethics from the root baadala ya hawa vijana wenye kulewa madaraka na wasio na utii kwa viongozi wa chama.
 
Sikutegemea vijana wa leo kama shonza na wengine wawe wavivu wakufikiri kiasi hicho na kuanza kulumbana kwa mambo yasiokuwa na tija kwa TAIFA wala chama chao kwa sababu ya njaa tu na kwa faida ya watu wachache ambao awalitakii mema TAIFA LETU pia CDM."!!makwazo haya budi kutokea lakini ole wake ajaye na makwazo"!!
 
Niliomba msamaha kuhusu kushirikiana kwangu na kundi la MASALIA/PM-7 na pia kujibu tuhuma zilizotolewa dhidi yangu kwa njia ya mtandao badala ya kufuata taratibu za vikao.

SITA:
Tuendelee kusonga mbele na tuwapuuze hawa wanaotumiwa kufifisha nguvu ya Mabadiliko kwa kutunga uongo, uzushi na ghiliba ili malengo yatimie. Hawa tuwapimie kipimo kile kile kinachotumika dhidi ya CCM na maadui wa CHADEMA. Waache waendelee na matamko mfu yanayofadhiliwa na maadui zetu akiwemo yule aliyekuwa anatumia nguvu nyingi kudai posho ya wabunge iongezwe hadi kufikia laki 5 kwa siku (na kuibatiza jina-UJIRA WA MWIHA) ili aweze kufadhili uasi dhidi ya CHADEMA.

Big up kamanda...
Ila take care hayo maandishi ya bluu yasije yakakulazimu kufanya hayo ya red...
 
hivi huyu juliana shoza ni nani hasa! halafu mbona anajiamini sana anatumiwa na magamba nini! hivi visichana vinavyo jichubua si vya kuvipa uongozi! BAVICHA mlimtoa wapi huyu! kana kadodo hela kitinasa na vanu vazima,nige sambi tufika mkambie kakae kimyaaaaa!
 
Kwangu mimi hii ni aibu kubwa sana kwa vijana...hasa tunaowategemea kuja kulikomboa taifa hili kiuchumi na mizizi mirefu na mikubwa ya rushwa. Vijana hawa Ben saa8 na Shonza wote wanatumia mitandao hii ya kijamii kuonesha nani ana hoja bora kuliko mwenzie, nani anaweza kupanga ama kupangua hoja, nyuma ya pazia wote mienendo yao kimaadili inabaki kuwa ni swali zito. Wanachofanya sasa ni kuiweka CDM kwenye hali tete na hivyo kuonekana ni chama ambacho hakiandai warithi wenye maadili ya dhati kiuongozi. Kumbuka kwamba CDM kama taasisi inatakiwa ijiuze kwa wananchi na kuonesha waziwazi ipo tayari kulikomboa Taifa hili kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kutupwa unaowakabili wananchi. CDM iangalie vizuri BAVICHA kwani kwa sasa sidhani kama inafanya kazi iliyokusudiwa vizuri.
 
Kasema ni consultant, nimejaribu kumwelewa kiasi. Ambacho sijaelewa ni kwamba yeye mwenyewe anapata wapi consultation ya haya anayoyafanya.

Na je ana-offer consultation services kwa CDM leaders?

All in all there is motivation behind this movement, I believe this is not charity job he is doing!!!

-Uliniuliza ninafanya kazi gani nyingine nje ya siasa nikakujibu.

-Sipati tenda yoyote ya consultancy CHADEMA au kwa viongozi wake

-Hapa ninafanya siasa kwa kujibu uongo uliotungwa na wanasiasa kwa narrow interests za kisiasa.Uiihusishe na profession yangu nje ya Siasa

-Nimetumia haki yangu ya kusema ukweli.Sihitaji kulipwa kwa ajili ya hili unless unanielekeza niwe too materialistic na ku-compromise principle zangu.Wapo vijana ambao hawawezi kufanya hiki na ni wengi ndiyo maana unaona hili ninalofanya ni strange.Una haki ya kufikiria hivyo kutokana na Mazoea.

Rather, you would have us accept that your stance on the matter at hand is justified and right even when you provide no basis for your position..You can do better than this

Since you know so much about this issue, do you mind telling us why you hold the views you have expressed here and why you think that this saga is relevant to my professional carrier?.

Tumekusoma na ww ndo walewale wachumia tumbo..once a traitor always a traitor!!!!

You are right,

Post zako zilizotangulia zinajua intention yako ni nini.Nasonga Mbele
 
haya bwana,naona kazi imeanza tena.
mimi naomba tuwe na wagombea huru/binafsi ili kuondoa haya mambo ya kujiunga na chama chochote kile cha siasa.
 
-Uliniuliza ninafanya kazi gani nyingine nje ya siasa nikakujibu.

-Sipati tenda yoyote ya consultancy CHADEMA au kwa viongozi wake

-Hapa ninafanya siasa kwa kujibu uongo uliotungwa na wanasiasa kwa narrow interests za kisiasa.Uiihusishe na profession yangu nje ya Siasa

-Nimetumia haki yangu ya kusema ukweli.Sihitaji kulipwa kwa ajili ya hili unless unanielekeza niwe too materialistic na ku-compromise principle zangu.Wapo vijana ambao hawawezi kufanya hiki na ni wengi ndiyo maana unaona hili ninalofanya ni strange.Una haki ya kufikiria hivyo kutokana na Mazoea.

Rather, you would have us accept that your stance on the matter at hand is justified and right even when you provide no basis for your position..You can do better than this

Since you know so much about this issue, do you mind telling us why you hold the views you have expressed here and why you think that this saga is relevant to my professional carrier?.

You are right,

Post zako zilizotangulia zinajua intention yako ni nini.Nasonga Mbele

Kudaadeki.Ben Saanane unajua kuwapatia watu naona mara moja anayekutuhumu umemgeuzia kibao yeye ndiyo aje hapa kujitetea tena?Dogo unateleza kama mlenda
Umenikuna sana kwa jinsi ulivyo mwepesi wa kujibu mashambulizi na kwa ushawishi.Ila sasa vurugu zako jimbo la Rombo uache
 
Back
Top Bottom