Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,306
- 12,969
Maelfu ya wapalestina wengi wao wakiwa waislam na waandishi wa habari wameuawa na wanaendelea kuawa kila siku huko Gaza na majeshi ya Islaeri.
Nchi yetu ina mahusiano ya kibalozi na Israel na Palestina pia. Je ni upi msimamo wa serikali kuhusu mauaji haya ya watu wasiokuwa na hatia wakiwemo wanawake, watoto, wanaume na waandishi wa habari yanayoendelea kila siku huko Gaza.
Na je mbona BAKWATA wapo kimya kabisa kana kwamba hakuna masaibu yanayowapata waislamu wenzao huko Gaza?
Wenzetu Afrika ya kusini wameshajipambanua kwa kupinga mauaji hayo kwa kupeleka kesi ICJ kutaka Israel ichukuliwe hatua kwa mauaji inayofanya kwa raia huko Gaza. Mbona sisi tupo kimya?