Upendo huu wa mawifi zangu umenifika happaaa!

We mshikilie jamaa nawepende hao mawifi tena wasijue unawachukia na omba wasipite hapa, nenda nao sambamba.
 
Jamani mimi mawifi zangu (dada wa mtarajiwa wangu) wananitatiza. Mchumba wangu ni mtoto wa kiume pekee kwa wazazi wake na amebarikiwa madada sita. To be honest nawapenda mawifi zangu na wananipenda pia kwa maneno na matendo ila sasa upendo huu naona unaelekea kuwa mzito sana kwangu.

Mimi ni mwanamke simple sana. Mavazi na Hairstyle na muonekano wangu kwa ujumla ni simple. Sasa mawifi zangu tangu nimetambulishwa kwao wamekuwa ni watu wa kutaka kunibadilisha. Ninaletewa nguo, hereni, viatu na kila aina ya urembo ambao si kama ule ninaopendelea. Weekend lazima mmoja anitafute twende salon, tukifika huko nitalazimishwa mambo ya pedicure, manicure wakati sina mazoea hayo. Yani ni kama wamewekeana zamu, leo huyu kesho huyu. Mara shopping na tukifika huko sipewi uhuru wa kuchagua nivipendavyo bali naambiwa "wifi hii ndo itakupendeza bwana, tena hata kaka atapenda ukivaa hii".

Wiki iliyopita tulienda harusini mimi, mchumba wangu na dada zake wawili. Nikakutana nao mitaa ya Mwenge ili tuongozane kwenda huko. Nilikuwa nimevaa flat shoes na gauni langu la usiku. Jamani wifi zangu walilalamika kwanini nimevaa flat shoes kwa muda kama dakika 20 hadi baby ikabidi aseme mwacheni mke wangu. Leo wifi amenitag instagram kwenye picha ya viatu virefu ananiuliza kama nimevipenda. Sijajibu hadi sasa na najawa na hasira na mashaka kuwa endapo nikiolewa si watakuja kunipangia hadi nightdress za kumvalia mume wangu hawa..

Nifanye nini waniache alone bila kuwa na mtafaruku au wasijisikie vibaya kwani wananipenda na najua wanafanya kwa upendo na nafurahi kupendwa ukweni ila daaaaahhhh!
Wamo humu wameelewa.. Watapunguza
 
Asante kwa ushauri ila naogopa hata kumwambia, sitaki ionekane kama nina negativity kwa dada zake. Wako close sana na anajitahd wote tuwe kitu kimoja
Wanakupenda na wanaona kabisa unauzuri wa asili
Usikatae vi2 wanavyokupa maake wanajua wanachofanya
Jitaidi kuendana nao na uone kama utapenda muonekano wako mpya au vp
 
hongera mama

umefanikiwa kutujaza wivu
sie wenye mawifi hawana hela

na mawifi dada binamu kutwa kupigana vikumbo kisa kaka yao kinyama cha hamu...
 
kha!! jamaa hana mke kwa kweli. yaani wewe mwenyewe kwa mdomo wako unashindwa weka stand kwa mawifi kuwa this is me whether u like it or not. ata kama wataka kuolewa lakini mhmmmm.....
 
Umefanya kosa kujiweka humu na ulivyojieleza wakipita huku moja moja watajua umewaleta humu jambo ambalo litakuketea shida
 
hongera kwa mawifi wengi na wenye upendo
waeleze upendacho na usichopenda
 
mawifi sita?!..Natumai walau mmoja wao atakuwa mdau wa MMU..Kuwafikishia ujumbe wengine.
 
*NANI KAKUZUIA KUJIPAMBA, EBU JIPAMBE DADA... JIPAMBE UWE MREMBO ZAIDI*

Leo nataka kuwatia moyo wanawake kwa habari ya kujipamba, jipambe ili mpendeze mwaya.......

Najua zipo saloon nyingi zenye hadhi mbalimbali na zina wataalamu wa viwango tofauti tofauti lakini nimegundua saloon moja haihitaji gharama kubwa sana kama unataka kupambwa.

Nilikuwa napita mahali nikaiona, nikasema lazima niwashauri wanawake waende hiyo saloon wakajipambe na haipo mbali. Unakubalije kukaa bila kujipamba na wakati umeruhusiwa?

Mwanzoni nilipoiona hii saloon nilishtuka nikaambiwa, usishtuke .........nikauliza kwanini? Nikaambiwa...... _*Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwatii waume zao*_1Pet 3:5

Nikauliza walitumia mapambo gani hao wanawake wa zamani? Akasema; _*Wanawake wa zamani walijipamba kwa mapambo yasiyoharibika yaani roho ya upole na ya utulivu*_ 1Pet 3:4 Nikasema.... Imekaa poa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom