Upelelezi wakwamisha Kesi ya Watumishi TANESCO wanaodaiwa kuhujumu Tsh. Bilioni 2

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1694632708474.png
Ni Kesi ya Uhujumu Uchumi inayowakabili Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Mwanza, Abdukadri Lwassa (Fundi) na Respicius Rwegoshora (Afisa Bohari) imeshindwa kuendelea kutokana na upelelezi kutokamilika.

Watumishi hao wanakabiliwa na mashtaka 125 yakiwemo ya Kughushi Nyaraka, Ubadhirifu wa Mali ya Umma na Kutoa Nyaraka za Uongo ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Novemba 16, 2021 na Disemba 17, 2022 katika Ofisi za TANESCO, Nyakato.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ameahirisha Kesi hadi Septemba 14, 2023 Saa 3:30 asubuhi, itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa tena.

=============

Kesi ya Uhujumu Uchumi namba 5/2023, inayomkabili Fundi Mchundo wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Mwanza, Abdukadri Lwassa (39) na Ofisa Bohari wa Tanesco (mtunza stoo), Respicius Rwegoshora (33) imekwama kuendelea leo kutokana na upelelezi wake kutokamilika.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 125 likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh2 bilioni huku wakidaiwa kutenda makosa hayo katika Ofisi za Bohari ya Tanesco iliyoko Nyakato jijini Mwanza kati ya Novemba 16, 2021 na Disemba 17, 2022.

Kesi hiyo iliitwa leo Septemba 13, 2023 kwa ajili ya kutajwa ambapo Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Mwanahawa Changale ameiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa huku akidokeza kuwa upelelezi wake umekaribia kukamilika.

Kauli hiyo ya Changale, imepingwa vikali na jopo la mawakili wa utetezi katika shauri hilo akiwemo wakili wa mshtakiwa namba moja (Abdukadri Lwassa), Erick Mutta ambaye ameiomba mahakama kuihoji Jamhuri ili kupata uhakika wa lini upelelezi wa shauri hilo utakamilika.

Mutta amesema kuchelewa kwa upelelezi wa shauri hilo kunawafanya washtakiwa waendelee kusota rumande jambo ambalo amelitaja kama kuchelewesha haki ya wateja wao.

Kauli ya Mutta imeungwa mkono na mawakili wa mshtakiwa namba mbili (Respicius Rwegoshora), Amri Linus akisaidiana na Steven Kitale ambaye amesema tayari wameandika barua Mahakama Kuu kuomba amri ya wateja wao kupatiwa dhamana.

Wakili Linus amesema ombi lao limekubaliwa bila kuweka wazi masharti ya dhamana yaliyoainishwa katika majibu hayo huku akiomba shauri lipangwe kesho ili kukamilisha taratibu za dhamana kwa wateja wao kama ilivyoainishwa katika majibu ya barua hiyo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela anayesikiliza shauri hilo, Fortunatus Kubaja baada ya kusikiliza hoja za pande zote ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Septemba 14, mwaka huu Saa 3:30 asubuhi, itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa kukamilisha masharti ya dhamana.

MWANANCHI
 
Mtu yuko ndani kwa kesi ya uhujumu uchumi alafu bado anakitambi😁😁kwa nini upelelezi usikwame? Mambo ya shika nikushike😀😀😀
 
Back
Top Bottom