Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Most likely jina la Patel halitarudi kutoka juu......... kuna faida pia ya "Ku post picha zake na viongozi wakuu huko Instagram na Facebook". Tuhuma za rushwa zitamuangusha Patel. Si unakumbuka 2010 Kigwangala alikuwa mshindi wa tatu kwenye kura za maoni?

wakimkata Patel UKAWA tunachukua jimbo kiulaini
 
Ningekuwa mwana ccm ningepatwa na hofu sana wafuasi kindakindaki wa EL kubaki ccm na kuwa kwenye vyombo nyeti vya maamuzi.

Mfano Nchimbi, Kimbisa et al. Kama unajua siasa utakuwa umenielewa

Furahia Bashe kushinda kura za maoni kwa sasa


hili neno hili
 
Mkuu tupe Ukonga,Instagram kila mgombea anasema ameshinda hapo Ukonga,tupe uhalisia!!!
Hata kwa yeyote anaejua Hilo jimbo,Mengine sijasikia Utata!!ok na kule kwa kabaka Gaudensia na Matiko Easther sijui nani kashinda
Yeyote mwenye taarifa

Jimbo la Rufiji jamani?
 
Kama kuna watu alikuwa anawategemea sana Lowasa katika mikakati yake basi ni pamoja na huyu Hussein Bashe. Bashe ni miongoni mwa makada wa CCM ambao walitajwa kuhamia CHADEMA kumfuata bosi wao Lowasa. Pia alikuwepo Mussa Zungu, Kangi Lugola, Christopher Ole Sendeka nk. Ushindi wa makada hawa hakika ni pigo kubwa sana kwa Lowasa. Sidhani kama kuna dalili za yale Mafuriko ya makada wa CCM kukimbilia CHADEMA. Mpaka sasa, katika watu wake wa karibu, ni mkewe tu ndiye aliyeenda CHADEMA.

Na bado

Ww usifuate mambo yako fuata ya lowasa
 
Kwa upande wangu sijui mnalichukuliaje hili lakini kwangu mimi nionavyo watu HAO wa LOWASA kubaki CCM nalichukulia kama anguko la SERIKALI ijayo kwani wabunge hao masalia (CCM) hawatakua na umoja kama Uliokuwepo hapo awali WABUNGE hao hoja ya serikali ikija na wakaona wanaweza kuungana na wale wa upande wa pili alipo EDDO hoja za serikali zitakwama. Na mambo mengi ya serikali yanaweza kuwa hayasogei.
 
Hawa wapiga kura za maoni wangezingatia pia uadilifu wa mgombea,maana ndugai anaweza kupiga hata wapiga kura wake,hana uvumilivu,tunasubiri kamati kuu kumwengua vinginevyo ukawa chukua jimbo
 
Back
Top Bottom