Updates kutoka Uwanja wa Mashujaa Mtwara: Mkutano wa Kampeni za mgombea Urais CCM

...(Gesi imepatikana Mtwara! Serikali ya awamu ya nne imeanza kuweka viwanda kikiwemo cha Dangote, Serikali ijayo itasambaza viwanda Mtwara; viwanda vikubwa, vya kati na vidogo. Kupitia viwanda tutafikisha asilimia 40 ya vijana walioajiriwa.

Tanzania ya MAgufuli itakuwa ya viwanda!).....

Nimequote hiyo paragraph sababu nina hakikika kuwa hakutakuwa viwanda vingine mtwara tofauti na Dangote cement ambavyo vitajengwa kabla ya uhakika was oil and gas. Na hii ndio itamtoa magufuli 2020 endapo atapita huu mwaka. Kwa nini nasema hivyo? Ni kuwa nimewahi hudhulia moja ya workshops za BG and StatOil ambao ndio wamiliki wakubwa hiyo gas and oil na wao wanasema kuwa Decision to invest on oil and Gas wataitoa mwaka 2019 ama 2020. Na ikumbukwe kwamba viwanda vinavyosemwa kujengwa mtwara ni vya oil and gas related industries kama services industries to the oil and gas companies ama viwanda vinavyotegemea Gas and oil kama raw materials e.g. fertilizer company. Sasa kama hawa jamaa kama watatoa decision to invest mwaka 2019/20, hivyo viwanda vitajengwa link????. Na moja ya sababu zinazowafanya wachelewe kutoa decision hiyo ni Ardhi ya kuweka kiwanda cha kuchakata gas (LNG) na mwenye mamlaka ya Ardhi yote ya nchi mnamjua. Viwanda kujengwa Mtwara ni ndoto zinaotwa.
 
Kwa kauli moja, wananchi wa Mtwara.... wamemkubali Dr. Magufuli,

Imani yao yote kwa magufuli. Vijana kwa maelfu, wamesema... UKAWA ipo kwenye hifadhi ya barabara... Na tingatinga lishawashwa.
Ni kanyaga kanyaga.

Wamezielewa sera, ilani na mipango ya maendeleo ya Dr. Magufuli.. Wamesema ukawa hawajajipanga na hawawezi kuiweka nchi kwenye majaribio.

#CCM mbele kwa mbele
#HapaKaziTuu
 
CCM WAONGO JAMANI, MANENO MENGI UTEKELEZAJI 10.03% ya 100%. ATUWAAMINI TENA
 
Magufuli anasubiri kuapishwa tu sasa. Hongera sana Rais wa 5 JMT.

Queen Esther

Leo kutakuwepo mkutano wa kumtambulisha Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli. Mkutano huo utakuwa live kuanzia saa nane mchana.

Updates: 8:00 Mchana

Tuko live kutoka Mtwara, mkutano wa kampeni unaendelea katika viwanja vya Mashujaa mkoani humo, watu ni wengi kama ilivyo kwenye mikoa yote ambayo mgombe huyo amepita.

Star TV wako hewani moja kwa moja kutoka viwanjani hapo, endelea kuwa nasi kwa taarifa za kinachojiri!

===============================
===============================

6.jpg

Mgombea amepanda jukwaani sasa, anawasalimu wanaMtwara. Anasema anatambua kuwa wanahitaji mabadiliko, ndio maana akaomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais.

Hakuwa anataka kujaribu Urais, amekuwa mbunge kwa miaka 20 na amekuwa waziri kwa miaka ishirini pia, anaifahamu vizuri Serikali, anajua wapi pamelegea, wapi pa kurekebisha!

Akiwa Waziri wa Ujenzi, ametengeneza barabara zilizokuwa zinazowahusu. Kwa muda mrefu wakazi wa Mtwara wameteseka na barabara kwenda Dar es Salaam, sasa hivi wanaenda asubuhi na kurejea jioni.

Kwenda mwanza zamani iliwalazimu kupita Uganda na Kenya, sasa safari ya Dar - Mtukula inawezekana hata kwa bajaji na wakati huo alikuwa anatumwa, saa anataka awe mtumaji na alete maendeleo.

Atateua makandarasi wanne wa kutengeza barabara kutoka Mtwara - Newala - Masasi, ole wake huyo Waziri atakayemtuma kufanya hiyo kazi! Barabara itatengenezwa kwa kiwango cha lami!

Bandari ya Mtwara itaimarishwa iwe sawasawa na bandari ya Dar na Zanzibar na Tanga ili wakazi wa Mtwara wapate ajira za kutosha. Mizingo inayoenda Malawi na Zambia itateremshiwa hapo. Mtwara Kuchele!

Gesi imepatikana Mtwara! Serikali ya awamu ya nne imeanza kuweka viwanda kikiwemo cha Dangote, Serikali ijayo itasambaza viwanda Mtwara; viwanda vikubwa, vya kati na vidogo. Kupitia viwanda tutafikisha asilimia 40 ya vijana walioajiriwa.

Tanzania ya MAgufuli itakuwa ya viwanda!

Makusanyo ya fedha yameanza kuimarika! Katika kipindi chake makusanyo yatakuw amara mbili zaidi, Serikali itadhibiti wizi na ufisadi, wezi wataipata! Kutakuwa mahakama maalumu ya wezi na mafisadi, ili wafungwe haraka! Pesa inayopatikana iende kwa wananchi wanyonge!

Wanaosema CCM imechoka wasisikilizwe! Hatuwezi kuchoma kitanda kwa sababu ya kunguni wawili au watatu, ameomba urais ili aweze kuwaondoa hao kunguni wachache!

Kuna usumbufu kidogo kwenye maswala ya kilimo, soko la korosho litaimarishwa. Serikali itapunguza machungu ya wananchi kwenye kilimo cha korosho.

Kuanzia mwaka ujao, wanafunzi hawatalipa ada kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne! Uwe CCM, UKAWA, CHADEMA, Mkristu, Mpagani na kadhalika, HAKUNA KULIPA KARO!

Kuanzia mwaka kesho, Mtwara itafanywa kuwa sehemu kubwa ya uwekezaji. Itajengwa reli ya kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay, itaunganishwa na Liganga na Mchuchuma.

Kila kata itapewa sh. 50Milioni kwa ajili ya kukopesha vijana na akinamama!

Anaomba kura za watu wa vyama vyote, Tanzania inagitaji maendeleo! Wanaosema 'People's Power' wampe yeye hizo nguvu! Watu wa CUF nao wahakikishe yeye anakuwa rais wa awamu ya tano! WanaCCM nao wanatoa dole, wampe dole kubwa, zito!

Matatizo ni mengi kwa sasa, anazungumzia hujuma kwenye sekta ya afya na vifaatiba! Serikali yake itayamaliza hayo, dawa zote zitapatikana hapo hapo hospitali. Fedha zilizokuwa zinapotea zitatumika kwenye kuhakikisha hilo.

Kila kata itakuwa na kituo cha afya, kila wilaya itakuwa na hospitali na kila mkoa utakuwa na hospitali ya rufaa. Anamaanisha hilo!

Anaomba wakazi wa Mtwara wazingatie amani na usalama, ndio msingi wa mafanikio! Libya ilikuwa nchi ya amani chini ya utawala wa Muamar Ghadaffi, huduma zilikuwa bure! Wakazi wakataka mabadiliko kwa kushirikiana na Wazungu, Libya wakaanza kupigana wao kwa wao, wakamuua kiongozi wao na maisha yameharibika.

Leo hii vijana wa Libya wanakimbia taifa lao, nchi haikaliki kwa kutaka mabadiliko yasiyo na mpango! Sisi tusifanye kosa kama walilofanya Libya!

Sio kila anayeahidi anatekeleza anachokiahidi, mengine ni maneno ya kilaghai tu! Tusije tukadanganywa na matapeli wa kisiasa! Maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kwa kushikamana na kuwa na amani bila kujali itikadi zetu!

Wazee wamefanya kazi kubwa, kuanzia mwaka kesho tutaanza kutoa pensheni kwa wazee!

Wananchi wa chini wamekuwa wakisumbuliwa na kero na kodi za ajabu; mama ntilie, bodaboda na kadhalika. Serikali ijayo itahakikisha hakuna usumbufu kwa makundi ya chini ya wananchi!

Wafanyakazi wametishiwa kuwa Magufuli atakomesha wafanyakazi, anadai hana ukatili wa aina hiyo! Anataka wtu wafanye kazi, na walipwe mishahara mikubwa kulingana na kazi yao. TANROADS inalipa wafanyakazi wanaolipwa vema, na wanaowajibika! Serikali yake itaboresha maslahi ya wafanyakazi na kuboresha utendaji kwa wote!

Serikali itaanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya wasanii, yeye mwenyewe ni msanii anayepiga tumba! Serikali itaboresha haki za wasanii, wasiibiwe tena!

Haki za walemavu zitasimamiwa, sisi wote ni walemavu watarajiwa!

Wajane nao watatazamwa! Wataangaliwa wakati wakiwa wanatafuta wanaume wengine wa kuwaoa. CCM imeonesha mfano kwa kumteua Samia Sululu kuwa mgombea mwenza na makamu wa Rais. Atakuwa pia mshauri wa Rais kuhusu mambo ya wanawake!

Kuna vyuo Mtwara! Serikali itahakikisha mikopo kwa wanafunzi inaboreshwa, itapatikana bila usumbufu kama zamani. Anayewakopesha wanafunzi ajiandae... Anawaasa pia wanafunzi kuwa makini na matumizi ya fedha wanazokopeshwa, wanaozifuja watawajibishwa pia!

Sekta ya kilimo, uvuvi na sekta husika zitaboreshwa pia. Kutakuwa na viwanda vya kusapoti sekta hizo, tutaacha kuagiza bidhaa za kilimo kutoka nje!

Majeshi yetu yataimarishwa kwa malengo ya kuimarisha ulinzi na usalama! Majeshi yataboreshewa mishahara, motisha na vifaa vya kazi. Jeshi la Polisi wanafanya kazi nzuri, sawasawa na majeshi mengine yote. Yeye atakuwa rafiki wa majeshi yote!

Nidhamu ya jeshi itaimarishwa, kujiamini kwao pia kutaimarika!

Bei za vifaa vya ujenzi zitapunguzwa, tumeanza mfano kwa kuweka kiwanda cha Simenti Mtwara. Serikali ijayo imejipanga kwa ajili ya kuleta maendeleo...

Anamtambulisha Hasnein Murji, mgombea wa Ubunge wa Mtwara Mjini!

Wagombea udiwani wote kwa tiketi ya CCM Mtwara Mjini wanatambulishwa sasa, wanandiwa pia!

=============================
=============================

7.jpg

Wananchi wa Tunduru wakifurahia jambo kwenye mkutano wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.

2.jpg

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Mchinga waliojitokeza kwa wingi kumsalimia wakati akiwa njiani kuelekea Masasi.

Nimequote hiyo paragraph sababu nina hakikika kuwa hakutakuwa viwanda vingine mtwara tofauti na Dangote cement ambavyo vitajengwa kabla ya uhakika was oil and gas. Na hii ndio itamtoa magufuli 2020 endapo atapita huu mwaka. Kwa nini nasema hivyo? Ni kuwa nimewahi hudhulia moja ya workshops za BG and StatOil ambao ndio wamiliki wakubwa hiyo gas and oil na wao wanasema kuwa Decision to invest on oil and Gas wataitoa mwaka 2019 ama 2020. Na ikumbukwe kwamba viwanda vinavyosemwa kujengwa mtwara ni vya oil and gas related industries kama services industries to the oil and gas companies ama viwanda vinavyotegemea Gas and oil kama raw materials e.g. fertilizer company. Sasa kama hawa jamaa kama watatoa decision to invest mwaka 2019/20, hivyo viwanda vitajengwa link????. Na moja ya sababu zinazowafanya wachelewe kutoa decision hiyo ni Ardhi ya kuweka kiwanda cha kuchakata gas (LNG) na mwenye mamlaka ya Ardhi yote ya nchi mnamjua. Viwanda kujengwa Mtwara ni ndoto zinaotwa.

Siyo lazima yeye ndiyo ajenge hivyo Viwanda bali anaweza pia akaweka mazingira mazuri kwa raisi atakayemfwatia ili aweze kuvijenga, cha muhimu ni kwamba tunakwenda kutoka A kwenda B na kama akiweza kulifanya hilo yaliyobakia wengine watayafanya kinachokosekana mpka sasa hivi nchini mwetu ni Utawala wa sheria na Haki hivyo akipatikana mtu anayeweza kuzisimamia sheria zetu na kwamba zitoe haki kwa kila mmoja wetu basi mengine yoote yatafwata tu kama vile maji yanavyofwata Mkondo!
 
Masikini magufuri anahutubia na kushangiliwa na kikundi kilichopangwa na ccm,wakati kila mtu anaye msikiliza amenuna na wengi wao ni watu wa upinzani wameenda ku muinjoy
Wameenda kuenjoy burudani, maskini hao huwa hawana pesa za kutizama ze comedy live, sasa wakiletewa mpaka mlangoni tena bure kwa nini wasikimbilie
 
Kwa kauli moja, wananchi wa Mtwara.... wamemkubali Dr. Magufuli,

Imani yao yote kwa magufuli. Vijana kwa maelfu, wamesema... UKAWA ipo kwenye hifadhi ya barabara... Na tingatinga lishawashwa.
Ni kanyaga kanyaga.

Wamezielewa sera, ilani na mipango ya maendeleo ya Dr. Magufuli.. Wamesema ukawa hawajajipanga na hawawezi kuiweka nchi kwenye majaribio.

#CCM mbele kwa mbele
#HapaKaziTuu

wakumbushe kuwa na Mwenezi wa Wilaya wa Chadema amejiunga na CCM...
 
Wadanganye ambao hawana umeme na hawaijui Mtwara!naifahamu kuliko unavyodhani na huo uwanja wa mashujaa naufahamu vizuri sana!uwanja umejaa kuliko kawaida na Dunni haji hakujaza watu kiasi hicho!

Muwe wakweli wakati mwingine hizo propaganda zenu Bavicha zimeshapitwa na wakati,mnatumia mitandao kupotosha watu na kuwaaminisha kwamba CCM hakuna anayeipenda tena wakati si kweli!

Ikulu haendi mtu dhalimu hata siku moja!
Mimi binafsi nilienda kumwangalia joti, masanja,mzee, yusuphu na temba, CCM siipendi hata kidogo
 
Acha matusi wewe...

Matusi gani kwani uongo, leo nilikuwa kwny harakati zangu nikakutana na msafara wa magufuli toka Tandahimba, Namnyamba mpk Mtwara, yaani watu wangombea fulana za ccm mpk aibu, shortly wamakonde badilikeni na ktk sehemu ambazo ccm itavuna kula nyingi tz ya kwanza Mtwara
 
yaani trust me not this year...
wanawalaghai tu hao..!wameichoka mnoo CCM
 
Nimequote hiyo paragraph sababu nina hakikika kuwa hakutakuwa viwanda vingine mtwara tofauti na Dangote cement ambavyo vitajengwa kabla ya uhakika was oil and gas. Na hii ndio itamtoa magufuli 2020 endapo atapita huu mwaka. Kwa nini nasema hivyo? Ni kuwa nimewahi hudhulia moja ya workshops za BG and StatOil ambao ndio wamiliki wakubwa hiyo gas and oil na wao wanasema kuwa Decision to invest on oil and Gas wataitoa mwaka 2019 ama 2020. Na ikumbukwe kwamba viwanda vinavyosemwa kujengwa mtwara ni vya oil and gas related industries kama services industries to the oil and gas companies ama viwanda vinavyotegemea Gas and oil kama raw materials e.g. fertilizer company. Sasa kama hawa jamaa kama watatoa decision to invest mwaka 2019/20, hivyo viwanda vitajengwa link????. Na moja ya sababu zinazowafanya wachelewe kutoa decision hiyo ni Ardhi ya kuweka kiwanda cha kuchakata gas (LNG) na mwenye mamlaka ya Ardhi yote ya nchi mnamjua. Viwanda kujengwa Mtwara ni ndoto zinaotwa.

Ningependa kujua kiwango chako cha elimu ndugu. Mimi ni mfuatiliaji wa maendeleo ya gesi. Mradi mkubwa kama huo una mchakato mrefu. Decision to invest ilishahalalishwa baada ya kupata gesi zaidi 45 billion cu.ft. Kupata wawekezaji wenye mtaji wa kujenga LNG plant ya $20-$30bn. Ni process. Na huwezi kuwaambia kwa staili zetu za kiswahili. Vigezo mbali mbali na soko la dunia vinatizamwa. Hiyo miaka uliyoitaja ni ujenzi kuanza. Na kuanza maana yake maandaluzi yalianza miaka kadhaa kabla. Maandalizi pia yalikuwa yamecheleweshwa na ukosefu wa sera ya gesi. Msumbiji wako mbele yetu. Ni kweli gesi itakuwa mama wa viwanda vingi sana kama ilivyo kwa chuma cha liganga na makaa ya mawe vitakuwa mama wa viwanda vizito. Ili tupae tunavihitaji sana viwanda hivyo. Ila kwa utafiti wangu msimu wa kuvipata hivyo umefika ili mradi tuwe na rais mchapakazi, siyo fisadi. Kuna hatari ya kuchagua watu watakaowekea vikwazo duniani kwa uwezo wao wa kupora rasilimali za nchi. Ni muhimu mahakama maalum ziwafunge mafisadi wote bila kujali chama ama sivyo tutaendelea kubaki masikini. Kutotambua haki zetu ni ugonjwa mbaya sana. Tuanze na katiba ya warioba
 
Back
Top Bottom