Updates kesi ya lisu, shahidi asema wenzake waongo, shahdi hamjui wakli wake, wala mlalamikaji wake

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
SHAHIDI WA 17 MATEMBELE ALLY MKWIZU.= POSTA MASTER WA SINGIDA
Meneja wa Posta Singida.
Posta ni nini?
Ni shirika la Umma.
Tuambie Chama cha mapinduzi wanatumia anwani gani?
S. L. P. 99, Singida.
Tuambie TLP, NCCR Mageuzi, APPT Maendeleo, CUF, wote hawana masanduku.
Je CHADEMA, Hawana sanduku.
Bwana matembele,
Umesema eneo lako ni wapi?
Mimi ni meneja wa Posta Mkoa wote wa Singida.
Tusaidie, Box namba Brac Tanzania.
Nani anakuwa mmiliki?
Kuna fomu Maalumu tunayojaza, kama ni mtu binafsi au Taasisi.
Kuna utaratibu Mwingine?
Hakuna.
Kwa hiyo kati ya mmiliki na Mtumiaji ni nani anahusika.
Mmiliki ndiyo huwa anapewa ufunguo na kadi halali ya kuchukulia mzigo Posta.

MAHOJIANO NA TUNDU LISSU.
T/L. Unanifahamu?
Ndiyo.
Unanifahamu kama nani?
Kama Mbunge
Nimewahi kuja posta kupata huduma ni sawa?
Ni sawa.
Unakumbuka nilikuja Posta kuja kuchukua pesa kwa western Union, je ni sawa?
Ndiyo,
Na unakumbuka kipindi hicho nilikuwa Mgombea Ubunge
Ndiyo.
Mweleze jaji, kama mimi unayenifahamu nina sanduku la Posta Singida
Sina Kumbukumbu, sina hakika na inawezekana huna.
Unamfahamu mtu anaitwa Alute Simon Mughwai?
Simfahamu
....................... Box 987........... ni la Alute Simon Mughwai, ni wakili Arusha
Mweleze jaji, je ni kitu cha ajabu kwa mtu kutumia sanduku la mtu mwingine?
Sio ajabu
Itakuwa ajabu kwa sanduku la Box 261, linalomilikiwa na Brac kutumiwa na watu wengine au taasisi kama wamekubaliana?
Sio ajabu.
Kuna mtu amekuja mahakamani, anaitwa Cosmas Kasangani, Alikuwa Katibu wa CCM ameiambia mahakama hilo sanduku 261, linamilikiwa na CHADEMA, wewe kama Meneja wa Posta sem a je ni sahihi?
SIO SAHIHI, chadema hawana Box hilo Mkoani Singida, huyo shahidi amedanganya.
Meneja wa Posta amemaliza ametoka.


Umesema kuwa uliambia kura zisiibiwe ni kweli?
NDIYO.
Mwambie jaji, Kwenye Kituo chako kura ziliibiwa au hazikuibiwa?
Ziliibiwa.
Kwa hiyo unasema kura ziliibiwa?
NDIYO.
Mweleze jaji, hizo zilizoibiwa Isuna ziliibiwa na nani?
Ziliibiwa na Mawakala wa CHADEMA.
Nimekusikia ukitaja Robert Kimanda, ni ndg yako kweli au si kweli?
Sio kweli.
Sasa mbona yeye alitoa ushahidi hapa mahakamani akakutaja wewe kuwa ndugu yake, je kati yako nay eye nani Muongo?
Yeye ndiye Muongo.
Umesema ulikuwa wakala, aliyekuwa wakala wa Isuna namba 2,
Ndiyo.
Orodha inasema kuwa aliyekuwapo hapo Ni Mghenyi Hasan je mlikuwa naye.
Ndiyo.
Kati yaw ewe unayesema fomu ilijazwa, na Mghenyi aliyesema ilichanwa chanwa baada ya CCM kushindwa kituoni, nani Muongo?
Yule aliyekuja mara ya kwanza ni mwongo.
Mweleze jaji, kama mimi na wewe tumewahi kukaa na kuzungumza ukiacha leo.
Ndiyo, tulikaa ukanipa semina,
Itakuwa tarehe 25, ila mwezi nimesahau, yawezekana ni Juni, Julai au Agosti. Wala haikuwa tarehe za Mwezi wa Kumi.
Jaji naomba nimwonyeshe shahidi Ratiba ya kampeni.
22/Agosti/2010. Ratiba inaonyesha nilikuwa kijiji cha Matongo, siku hiyo nilikuwa kijiji cha Ighuka maseke.
Mweleze jaji, niliwezaje kutoa semina Issuna wakati nilikuwa na Kampeni katika vijiji vingine?
Hiyo mimi sijui.
Mweleze jaji, nani amekupa nauli kuja Singida mjini?
Nimekuja kwa nauli yangu Mimi,
Shahidi, unamfahamu wakili wako?
Simfahamu.
Unamfahamu mlalamikaji katika kesi hii?
Simjui.
Kama wewe huwafahamu, wao wamekufahamuje mpaka wakakuweka kuwa shahidi?
Labda watakuwa wametajiwa na waliotangulia.
Mahakama hii imeambiwa kuwa Cleti Kidamwina ndo aligawa Juice, maji na soda je ni kweli?
Sio kweli.
Vilifikaje katika kituo chako, kwa gari, baiskeli, au pikipiki.
Sijui vilifikaje hapo, mimi nililetewa ndani.
SIJUI
Mwambie jaji, nani katika wagombea wa urais alishinda katika Kituo chako?
Kikwete.
Je kwenye kituo chako, pamoja na CHADEMA kuiba kura nani alishinda?
Njau wa CCM.
Kura zilipoibiwa ulitoa taarifa
Ndio,
Tatizo lilishughulikiwa vipi?
Halikushughulikiwa.
Katika Kituo chako, ngazi ya Udiwani nani alishinda?
Mgombea wa CCM.
Kwa hiyo licha ya wizi unaodai ulifanywa na CHADEMA katika kituo chako bado Waligaragazwa na CCM?
Ndiyo mheshimiwa
T/L........... SINA SWALI ZAIDI.
WAKILI WA SERIKALI AKAANZA:
Shahidi, umesema wewe ni Mwaachama wa CHADEMA?
Ndiyo.
Katika kituo cha kupiga kura mlikuwa mawakala wangapi?
Tulikuwa sita.
Umesema wewe ni mwana chama wa CHADEMA, ila ulisimamia CUF
Ndiyo.
Umesema mlielekezwa kuhakikisha kuwa mnalinda kura zisiibiwe ni kweli?
Ndiyo.
Je ilikuwaje ninyi mkaanza kuiba kura
Hapo sasa unanichanganya.
Tueleze mliibaje kura? Mbinu iliyotumika?
Kama ni kweli umesema kura ziliibwa saa tisa, je zoezi la kuhesabu kura lilimalizika saa ngapi?
Saa kumi?
Je ziliibiwa vipi wakati zoezi la kuhesabu lilikuwa halijaanza?
Hapo unanichanganya.
Je ni kweli kura ziliibiwa?
Ndiyo.
Ziliibiwaje?
Najua ziliibiwa lakini sijui ziliibiwa namna gani?
Kama hukuona zilivyoibiwa, ulijuaje zimeiibiwa?
Ziliibiwa, ila njia zilivyoibiwa sijui.
Umesema kuna wakala wa CCM alilalamika je ni kweli?
Ndiyo.
Alilalamikia nini na kwa nani?
Alimlalamikia msimamizi, kuhusu wingi wa mawakala wa chadema.
Je alijaza fomu ya malalamiko?
Ndiyo.
JAJI: VIPI MBONA SHAHIDI SAUTI HAITOKI, MPENI MAJI.
 
Hizi kesi za kuunga unga zina taabu kweli, lakini mwisho wa siku wataaibika sana hao
 
Njaa zetu zitatumaliza na hakika tuchapwa lakini tutapewa amri ya kunyamaza na hakika haki na usawa haitapatikana
Na viongozi wa chama na serikali mwogopeni Mungu na hakika wananchi ni dhalili kwenu kwanini mnawatumikisha kama punda au kisa umaskini wao? Je mtu kusimamia uchaguzi sasa anahangaika na kesi je ni Haki? na je wakati mwingine mtapata mawakala? Kwanini msikubali kushindwa? kwani mnataka kuwaona kuwa hawana kazi za kufanya ila za kwenu?
Naomba amri itoke na ikiwezekana wanaosumbua wananchi wapewe adhabu kali na iwe fundisho kwa watu wabinafsi na walafi wa madaraka
 
Hii sehemu inatia shaka kuhusu "credibility" ya shahidi:

"Umesema mlielekezwa
kuhakikisha kuwa mnalinda kura zisiibiwe ni kweli?
Ndiyo.
Je ilikuwaje ninyi mkaanza
kuiba kura
Hapo sasa unanichanganya.
Tueleze mliibaje kura? Mbinu iliyotumika?
Kama ni kweli umesema kura
ziliibwa saa tisa, je zoezi la
kuhesabu kura lilimalizika saa
ngapi?
Saa kumi? Je ziliibiwa vipi wakati zoezi la
kuhesabu lilikuwa halijaanza?
Hapo unanichanganya.
Je ni kweli kura ziliibiwa?
Ndiyo.
Ziliibiwaje? Najua ziliibiwa lakini sijui
ziliibiwa namna gani?
Kama hukuona zilivyoibiwa,
ulijuaje zimeiibiwa?
Ziliibiwa, ila njia zilivyoibiwa
sijui."
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
do! kazi ipo siku zote nasema haki haitakuwepo duniani! duniani kuna sheria binafsi naona kunamazingira ya watu kushinikizwa kutoa majibu au ushahidi ambao hata wao hawahukubali lakini watafanyaje ikiwa walio shikilia kula yao ndio wanao watuma? hapa nauhakika mwili na roho havifanani katika kutoa ushahidi. na wadanganyika tumezoea kuzurumiwa! kuna tetesi zisizo rasmi zilisikika kuwa bora silaa kuingia ikulu kuliko lisu kuingia bungeni hivi hii inamaana kesi hii inashinikizo sioni mazingira ya haki kabisa
lakini mungu yupo bora salama
 
Ningekuwa jaji na kama mazingira yangeruhusu, bila shaka ningeifuta kesi hii!!!!!
 
Back
Top Bottom