Uozo wa ajabu Vunjo!

kuku dume

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
414
62
Ndugu wakuu!
Ni dhahiri kwamba ukikaa na kujadiliana na watu utajua mengi.

Nikiwa katika wilaya ya Moshi leo nimejaribu kufika katika kata ya Kirua Magharibi na nikapata taarifa zilizonisikitisha.

Mosi ni kwamba inaonekana kwamba serikali ni dhaifu kiasi cha kuwaambia wananchi wachague ni kijiji gani wanachotaka kuwepo kati ya Kanji na Marua. Kumbuka kwamba hili linafanyika bila kujali mipaka ya kijografia.

Pili ni kuwepo kwa vijiji likuki visivyokuwa na watendaji ambapo inakadiriwa kwamba takribani vijiji 15 katika jimbo la Vunjo havina Watendaji.

Tatu ni kwamba wamekuwa wakiteuliwa watendaji wakorofi katika vijiji vinavyoshikiliwa na upinzani.

Nne ni kwamba zipo tuhuma za ufisadi dhidi ya mtendaji wa kijiji cha Nduoni kinachoshikiliwa na upinzani kiasi cha kusababisha mtafaruku katika uongozi wa kijiji. Pia nimedokezwa kwamba huyu mtendaji aliomba uhamisho kutoka kata moja kwenda nyingine bila malipo kutokana na uchafu uliozidi.

Chanzo: wananchi na viongozi wa maeneo husika.
 
Jimbo la Lyatonga Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa. Atatue hayo matatizo.
 
Madhara ya kuchagua wazee kuwa wabunge ,Vunjo mtajuta kwa kutomchagua jembe Crispin Meela
 
vunjo si ndio wa mrema?? mbona sikikii kelele zake

ila hali ya hivi ni common sana katika vijiji vingi hapa bongo
 
Nyumbani hapo hata barabara ya pale kawawa kupandisha uparo ni usanii kwakwenda mbele ahadi ya miaka kibao bado ni vumbi tu.
 
hivii baada ya kunywa kikombe kwa babu hali yake inaendeleajee?? lazima tujue hali ya afya yake kwanza
 
Alikuwa nje ya nchi wakati Betwel anapokea rushwa pale mnazi mmoja. Sijui kama alisharudi!
 
Jimbo la Lyatonga Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa. Atatue hayo matatizo.
Huyu mzee anayelala na kutoa udenda bungeni unatarajia atasaidia nini? katika kosa walilofanya wananchi wa vunjo ni kumchagua huyu babu kuwa mbunge!! Jimbo halina maendeleo yoyote barabara hakuna shule zimechakaa, maji mpaka mvua zinyeshe! yeye kazi yake kukimbizana na wanywa gongo basi na hata wenyewe amewashindwa wanamlia timing tu akija wanatulia akiondoka wanakunywa kama kawa!!Afadhali wangemchagua yule John mrema wa chadema hata yule jamaa wa ccm kuliko huu mzigo!!
 
Mkuu ukisema jimbo la vunjo halina maendeleo yoyote nadhani utakuwa unatukana. Ninaamini hata kama huyu mbunge hafanyi kazi lakini jimbo hili liko mbali sana kimaendeleo ukilinganisha na majimbo mengine mengi.
 
Mkuu Jimbo lina maendeleo lakini linazidi kurudi nyuma, nakumbuka kwenye miaka ya tisini maisha ya wanakijiji wa vunjo yalikuwa bora zaidi kuliko sasa, hata miundo mbinu iliyopa ni ile ya miaka ya sitini , kwa mfano ni aibu kwa wanavunjo kuwa na hospitali moja tu yenye hadhi, shule nyingi zilizopo jimboni hasa za sekondari hazifanyi vizuri na kwa barabara ndio usiseme.NI AIBU kwa wana vunjo kurudi nyuma kimaendeleo badala ya kusonga mbele ilkizingatiwa ya kwamba jimbo la VUNJO ndio lenye wasomi wengi kuliko eneo lolote mkoani Kilimanjaro
 
Ni kweli wananchi wengi wa vunjo wanaongoza kwa maendeleo, tatizo miundombinu hakuna hasa barabara nyingi za kule mlimani ni mbovu sana, hata ukipita njiani unaona wananchi wamejenga nyumba nzuri lakini hamna barabara!. Jembe linalofaa kutuongoza sasa ni JOHN MREMA. Huyu mzee hana ishu.
 
Mrema kazi yake ni kupigia kelele wizi kwenye wilaya zingine yake imeoza! 2015 si mbali M4C itasafisha uozo wote
 
Madhara ya kuchagua wazee kuwa wabunge ,Vunjo mtajuta kwa kutomchagua jembe Crispin Meela

Jembe ni Mrema wa CHADEMA weww!!
Mlete meela na Mrema kwenye mdahalo tuone nani kiazi kikuu
 
Mkuu Jimbo lina maendeleo lakini linazidi kurudi nyuma, nakumbuka kwenye miaka ya tisini maisha ya wanakijiji wa vunjo yalikuwa bora zaidi kuliko sasa, hata miundo mbinu iliyopa ni ile ya miaka ya sitini , kwa mfano ni aibu kwa wanavunjo kuwa na hospitali moja tu yenye hadhi, shule nyingi zilizopo jimboni hasa za sekondari hazifanyi vizuri na kwa barabara ndio usiseme.NI AIBU kwa wana vunjo kurudi nyuma kimaendeleo badala ya kusonga mbele ilkizingatiwa ya kwamba jimbo la VUNJO ndio lenye wasomi wengi kuliko eneo lolote mkoani Kilimanjaro
Wana vunjo wengi ni wanafiki!mmemuacha yule jamaa wa chadema mkampa Mrema eti siku akifa azikwe kama mbunge!kazi kweli!mtayavamia mahandaki hadi mshangae!Mrema anakula posho na kusinzia tuu bungen
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom