UOZO HUU WA TFF NANI ALAUMIWE??Milioni mbili za Chuji kugawanya

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,149
Milioni mbili za Chuji kugawanya
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd June 2009 @ 07:19 Imesomwa na watu: 22; Jumla ya maoni: 0


06_09_pg3puz.jpg








Utata wa mchezaji aliyeibuka mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Taifa ‘Kili Taifa Cup’ iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita umepatiwa ufumbuzi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage alisema Dar es Salaam jana, kuwa baada ya kuzuka zogo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa timu ya Temeke ‘TMK’ wakipinga mchezaji wa timu ya Ilala, Athumani Idd ‘Chuji’ kutangazwa mfungaji bora wa michuano shirikisho limepata ufumbuzi wa suala hilo.

TMK walipinga Idd kutangazwa mfungaji bora wakidai mchezaji wao Yahaya Tumbo ndio anastahili kushinda zawadi hiyo. Kwa mujibu wa Kaijage, TFF walipitia upya na kwa makini takwimu za ufungaji mabao katika michuano hiyo na kubaini kuwa wachezaji hao wawili Idd na Tumbo wote kwa pamoja wamefunga mabao matano kila mmoja na kustahili zawadi hiyo.

Kutokana na hayo TFF wameamua zawadi ya mfungaji bora ambayo ni Sh milioni mbili igawanywe kwa wachezaji hao. Baadhi ya viongozi wa TMK walisababisha malumbano mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika walipomvamia Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni wakihoji kupewa zawadi hiyo Chuji.

Watu wengine waliozawadiwa katika michuano hiyo iliyorindima kwa takribani wiki mbili katika hatua ya vituo kabla ya kuhamia Dar es Salaam kuanzia hatua ya robo fainali ni Salim Aziz wa timu ya Mkoa wa Tanga ‘Wagosi wa Kaya’ aliyeibuka mchezaji bora na kuzawadiwa Sh milioni 1.5. Wakati tuzo ya kocha bora ambayo iliambatana na zawadi ya Sh milioni mbili ilikwenda kwa kocha wa timu ya Ilala, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye aliiwezesha kutetea taji lake katika michuano hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo.

Na Mwamuzi Bora katika michuano hiyo iliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro alikuwa ni Oden Mbaga aliyejinyakulia Sh milioni mbili pia. Katika mchezo wa fainali ambao ulizikutanisha timu za Ilala na Temeke, Ilala waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Salum Mpakala na kuwazima vijana wa Temeke mbele ya Mbunge wao Abbas Mtemvu na mamia ya mashibiki wake waliofurika kwenye Uwanja wa Uhuru uliopo Temeke, Dar es Salaam.
 
Tabu ya Nchi hii kila kitu kinaendeshwa kisiasa. Uozo kama huu utaendelea tu kama atutaacha kufanya kila kitu kisiasa (Yaani kiuongouongo)
 
Tabu ya Nchi hii kila kitu kinaendeshwa kisiasa. Uozo kama huu utaendelea tu kama atutaacha kufanya kila kitu kisiasa (Yaani kiuongouongo)

Sidhani hapo kama tatizo ni siasa pekee kujipenyeza, bali ni kuwapa watu wenye mawazo za karne za zama za mawe ili watuongoze. Haiwezekani ktk muda wa wiki 2 tu, watu wazima wenye akili timamu tena wanajiita wataalam halafu wanashindwa ku-keep track ya wafungaji ..Hivi tutafikia lini kuwa na uwezo wa kutrack mambo madogo kama haya? Tuna matatizo ya msingi vichwani mwetu, si bure.
 
Tatizo ni Kayuni, sijui jamaa ana mkono wa nani? hana ajualo zaidi ya mmajungu na kujipendekeza. Tenga ondoa hilo jamaa halina faida zaidi ya kujitibia njaa dot com. Kwani hakuna watu proficient? zikitoka nafasi za kozi za fifa kila mwaka anaenda kayuni na madadi, kwa nini hawawapi walimu wa vyuo na sekondari? kuna walimu wazuri Chuo cha michezo Malya lakini fitina na njaa za wahuni TFF wanagawana wenyewe. Shame on you TFF na Kayuni
 
Jamani wiki mbili tu mnashindwa kujua mfungaji bora

mngepewa na hiyo mwaka si mngetaja na marefaree nao wafungaji/.....
 
Tatizo ni Kayuni, sijui jamaa ana mkono wa nani? hana ajualo zaidi ya mmajungu na kujipendekeza. Tenga ondoa hilo jamaa halina faida zaidi ya kujitibia njaa dot com. Kwani hakuna watu proficient? zikitoka nafasi za kozi za fifa kila mwaka anaenda kayuni na madadi, kwa nini hawawapi walimu wa vyuo na sekondari? kuna walimu wazuri Chuo cha michezo Malya lakini fitina na njaa za wahuni TFF wanagawana wenyewe. Shame on you TFF na Kayuni

OOOOOOOOOOOOOHHHHHHHH YESSS

MR N HANDSOME........THIS IS STUPIDITY.......NA SIJUI UTAISHA LINI.........
 
Back
Top Bottom