Uongozi wa Yanga wajitafakari sana kwa hili la Privadinho kukataliwa na mashabiki

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,203
27,326
Hekima inatuelekeza kwamba "Justice should not only be done but it must also seems to be done", kwamba haki haitakiwi kutendeka tu bali inatakiwa ionekane ikitendeka.

Hata kama Privadinho kweli ni shabiki wa Yanga kweli lakini mashabiki na wapenzi wa Yanga bado hawajaridhishwa na suala la Priva kupewa nafasi hiyo Yanga kwa sababu gestures zake zina demonstrate Usimba wake.

So katika hilo kwa wanayanga haki haionekani kutendeka.

Suala la Privadinho kupewa nafasi ya uongozi Yanga halijawapendeza wana Yanga wengi.

Mashabiki wa Yanga bado wanaamini kwamba Privadinho ni mshabiki wa Simba.

Ni tusi kubwa sana kwa wana Yanga kumpa nafasi shabiki wa Simba katika eneo ambalo wapo wanachama wapenzi na mashabiki wa Yanga wenye sifa ambao Uyanga wao hauna ukakasi.

Kwako Eng. Hersi Said, please lifanyie kazi, suala la Priva lime wanyong'onyesha wana Yanga wengi sana.
 
1664619831175.png
 
Muulize swali la aina hii leo, halafu usubiri majibu yake! Siku zote njaa haina baunsa. Mkate hata uwe mgumu vipi, ukiuchovya tu kwenye chai unalainika.

Hivyo kwa upande wangu, nadhani hao mashabiki wangempa muda kama walivyofanya kwa Haji Manara na Bernard Morrison. Na mwisho wa siku ahukumiwe kwa matokeo, na siyo unazi wake na simba.

Siyo vizuri kujenga uhasama wa kipuuzi kwa misingi ya usimba na uyanga. We are all Tanzanians.
 
Mbona Manara ni Simba tena aliwacharura kwelikweli na mnamchekelea leo. Kuna tatizo gani kwa Priva hata kama ni Simba kufanya kazi kwenu? Acheni ubaguzi au kisa yeye si mropokaji kama Haji?
Manara came to Yanga as an asset.
 
Muulize swali la aina hii leo, halafu usubiri majibu yake! Siku zote njaa haina baunsa. Mkate hata uwe mgumu vipi, ukiuchovya tu kwenye chai unalainika...
Kaka hizi timu Simba na Yanga zinapendwa kuliko unavyo weza kufikiri.

Mwaka 93, Mwameja (ambae ni shabiki wa Yanga lia lia ) akiwa ana dakia Simba alisaini mkataba na Yanga habari zikawafikia wanazi wa Simba.. kuna wanazi wali kwenda nyumbani kwake usiku waka mwagia tindikali kwa lengo la kumpofusha bahati nzuri haikuweza kumfikia wala kumdhuru..

Hili la Priva hapana kwakweli.

And am telling you muda si mrefu watu wataanza kuandamana
 
Hekima inatuelekeza kwamba "Justice should not only be done but it must also seems to be done", kwamba haki haitakiwi kutendeka tu bali inatakiwa ionekane ikitendeka...
Mbona na takadini ni Simba lialia na mnamkubali hadi mnataka kuandamana ili afunguliwe?
 
Si Privadinho pekee, ata kama MO, au Barbara ikioneka anauwezo wa kuongeza kitu kwenye malengo ya Yanga aajiliwe tu uko duniani kwenye mpira wao walisha vuka vikwazo hivyo vya kipuuzi.

Na Yanga walisha jipambanua Kwa kuanza na Senzo aliyekua Simba.
 
Nimeshasema sana humu tuelewe siasa na mpira nchi hii ni pete na kidole. Kuna mambo yanatestiwa upande mmoja yakikubali, yanapelekwa kwenye upande wa pili. Kuna kipindi ilikuwa ni vita kweli kweli mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine. Ilipozoeleka ikaingizwa kwenye siasa, ndiyo tukawaona kina Mrema baadaye Lowassa baadae wimbi la viongozi wa CHADEMA kuhamia CCM kuunga mkono juhudi.

Hayo yote yamewezesha leo hii mtu kama Manara (ambaye kwa upande wangu ni mtu mdogo sana tofauti na tunavyomkuza na anavyojikuza) kupokelewa Yanga na leo hao kina Privadinho sijui. Si muda mrefu hadi viongozi waandamizi wa hizo timu watakuwa wanaweza toka timu moja kwenda nyingine.

Kwenye upande wa siasa, naona tumeshayaona yote kipindi cha Magufuli. Labda imebaki tuone wanajeshi wastaafu waingie upinzani, ingawa na lenyewe kama tumeshaanza kuliona kwenye kesi ya Mbowe.
 
Hekima inatuelekeza kwamba "Justice should not only be done but it must also seems to be done", kwamba haki haitakiwi kutendeka tu bali inatakiwa ionekane ikitendeka...
Wewe Ni PUMBAVU SANA. YAANI TUMKATAE PRIVADINHO HALAFU TUMKUBALI HAJI MANARA? WEWE UNA AKILI KWELI?

MANARA TULIMKUBALI KWA KIGEZO GANI? nyie ndo mnafanya wote Yanga tuonekane hatuna akili na tutukanwe.
 
Back
Top Bottom