Uonevu unaofanywa na Maofisa wa polisi wa Upelelezi hapo Airport Dares-Salaam

Dawa yao unaongea kiingereza tu! Akikusalimu wewe mkate lugha anakuacha.Mbinu hii imenisaidia nakatiza..tu.halafu ukiwa umevaa nadhifu suti ya nguvu wanakuwa na wasi wasi na wewe hata kukubebea mizigo yako na kukuwekea kwenye usafiri wako pale nje. Vaa Tshirt na jeans, ama kaptura na malaba lazima wahangaike na wewe.
Points taken, lkn lile joto ...MMHm
Kuna siku nilivaa T-shirt, na nilikuwa nimefuatana na Mghana ambae alivaa nguo zao za kighana na dada mmoja wa kizungu. Wenzangu walikenuliwa mimeno nami nikazuiwa na kuanza kuulizwa maswali ya ajabu ajabu.

Moja ya swali ambalo mpaka leo linanikera moyoni ni pale waliponiuliza nimekuja kufanya nini Tanzania? ilhali nina pasipoti ya Kitz!
 
Ndugu zangu mpaka wakati huo huyo Rafiki yangu aliyezuiliwa vitu vyake hapo Dar Airport hajapatiwa na hao Mapolisi wa upelelezi wamesema kuwa endapo hatotowa Shilingi laki moja hawatampatia hata kama mwaka atakuwa anakwenda hapo Airport Dar kuviulizia vitu vyake hata kama itakuwa mwaka mzima hawatampatia hivyo vitu vyake je Ndugu zangu Wana Jf hiyo ni haki jamani? Au ndio hivyo nchi yetu haiwezi kwenda mbele mpaka kwa Rushwa? nimejaribu kuwapelekea habari hii yote Wizara ya mambo ya ndani na Kamishna Mkuu wa polisi wa Upelelezi wa Nchi lakini mpaka leo hawajanijibu. Sijuwi wamenitia kapuni?kwa sababu hayo yanayofanyika hapo Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha hapo Dar Airport hata hao wakubwa wanajuwa ila wamekaa kimya sasa Tutendelea kweli kimaisha? ndugu zanguni wana Jf na Viongozi wa Serikali wanaohusika nawaombeni munisaidie ili huyo rafiki yangu aliyezuiliwa vitu vyake hapo Kiwanja cha ndege Dar Airport aweze kupewa haki yake asanteni


nundu yumo humu atajibu hizi tuhuma
 
mimi waliniuzi kweli.tumetoka safari na familia.mara tunaambiwa tusimame.na kufunguliwa mabegi yetu kwa kuchanwa(yaani tunawaambia tuna ufunguo lkn wameyachan).walivuruga vuruga nguo nakutupa chini,aliangusha kifaa kimoja cha kioo.na kikavunjika(ulikuwa mzigo nilipewa na mtu nimpe ndugu yake tz).alafu hawajarudishia chochote walicho vuruga na kuomba hela ya chai!!!.
 
mimi waliniuzi kweli.tumetoka safari na familia.mara tunaambiwa tusimame.na kufunguliwa mabegi yetu kwa kuchanwa(yaani tunawaambia tuna ufunguo lkn wameyachan).walivuruga vuruga nguo nakutupa chini,aliangusha kifaa kimoja cha kioo.na kikavunjika(ulikuwa mzigo nilipewa na mtu nimpe ndugu yake tz).alafu hawajarudishia chochote walicho vuruga na kuomba hela ya chai!!!.
Hii ikikutokea tena usijibishane nao...wewe tafuta ofisi zao hapo ukawajuze maboss wao. Lakin ukiondoka eneo hilo ndio ukawalalamikie they don't care for you! Watakwambia unawasingizia!
Hiyo ilinitokea japo hawakunichania bag ila waliharib lock sikugundua mpaka nlipofika home...nlipoenda kuwalalamikia nilijibiwa ingekua ni hyo siku ya tukio kabla sijaenda home wangenilipa bag jipya.
Hawa huwa wanafanya hayo mda mwingine hawajui madhara yake.
Hiyo ndio njia yakuwadai!.
 
Pale airport kuna matatizo. Kila ninapotoka nje lazima niishie kwenye mikono ya hawa jamaa ambao kimsingi wanaonekana kabisa wanataka mahela.
 
pale wanapaswa kuwekwa maafisa wasomi na wenye mbinu za kutosha na wanajua kumtreat mteja vizuri kisheria mpaka waprove wanachotaka na sio askari wanywa gongo,elimu duni wanafikiri kumghasi mtu ndio kazi!
 
jeshi la polisi lipo nyuma ya wakati mno hawana utaratibu mzuri wa kushughulikia malalamiko ya watu alafu wanahimiza polisi jamii!! Mwema alianza vizuri lakini anamaliza vibaya mno jeshi limejaa ubabe mtupu!!
 
Ndugu zangu wana JF na pia viongozi wa Serikali wanaohusika ningependa kuwataarifa kuwa kuna vitendo vinafanywa na baadhi ya Maofisa wa Polisi wa Upelelezi hapo uwanja wa Ndege wa kimataifa Wa Dares-Salaam.

Hawa Mapolisi wa kipelezi wakikuona unatoka nje ya nchi wanakungoja tu umalize kutoka nje ya uwanja na hukukamata mpaka kwa ofisi zao za kipelelezi na kuanza kukuhoji na pia kukuweka ndani kwa muda wanaotaka wewe bila ya kosa lolote na wanaanza kukusachi wakihisi labda wewe ubeba madawa ya kulevya na endepo hautakuwa na hayo madawa watakuachia lakini kwa masharti lazima ukae kwao uende Toilet mara 3 ndio waweze kukuachia.

Na wakikuachia wanavizuia vitu vyako ulivyokuja navyo toka nje ya nchi eti wanavichunguza kwa muda basi hata kama ndio wanavichunguza haitowezekana wewe wakuache na vitu vyako wavizuie tena sio kwa muda mchache inachukuwa hata mwezi mmoja wanavichunguza.

Sasa inakuwaje hivyo vitu vyako ulivyokuja navyo wavichunguze kwa huo muda wa mwezi na haswa ukizingatia umekuja na mabegi ya nguo, zawadi kwa ndugu zako simu ya mkononi, Computer ya Laptop na vitu vingine vidogo vidogo?

Ninachoshangazwa mimi inakuwaje hivyo vitu vyako vinazuia kwa muda wa mwezi eti kwa sababu ya kwa uchunguzi? Swali hili itabidi tumulize Kaimu kamishna mkuu wa Upelelzi ndugu Fred Nzoe inakuwaje watu wake waliopo hapo kiwanja cha ndege cha kimataifa kuwanyanyasa raia wema?

Kwa hivyo vitendo vyao vya kuzuia mizigo yao kwa huo muda wa mwezi mzima kwa kisingizio cha kuvichunguza hivyo vitu?

Hayo yametokea kwa rafiki wangu alie toka nje hivi karibuni kafanyia hivyo na kila akienda huko Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha hapo Dares-Salaam anazungushwa mara aambiwe kuwa Mkuu wa kituo wa Polisi hayupo njoo keshokutwa na akienda hiyo kesho kutwa hurushwa tena njoo tena kesho kutwa hii kweli ndugu zangu wana JF na Viongozi wa Serikali wanaohusika tutaendelea kweli?

Kwa fikira zangu hao wanaohusika hapo Aiport inaonyesha wanataka Rushwa wapewe pesa ili wapate kumuachia huyo Rafiki yangu vitu vyake walivyovizuia bila sababu yoyote ile ya maana. Je Ndugu Wana JF Mnalichukulia vipi hilo suala na hivi karibuni Mheshimiwa ndugu Rais wa nchi yetu JM Kikwete aliwakemea maofisa wa kuzuia rushwa wawajibike kikazi sasa ikiwa Mapolisi wetu wa kipelelezi wanamzungusha huyo rafiki yangu kumpa vitu vyake sasa inapata mwezi hawajibiki, je hao aliowakemea Ndugu Rais JM Kikwete maofisa wa kuzuia Rushwa wanafanya kazi gani?

Ningeomba mnisaidie hilo tatizo langu maoni yenu ndugu wana JF wenzangu asanteni sana.
mimi nilikuwa =natoka Uk kwenda dar, nilipofika pale airport nikakutana na limama limoja hivi chafu sana nimevaa oversize t-shirt nad very long skirt, akaniambia haya fungua sanduku hilo! yaani hiyo lugha tu, nilimtazama nikaongea kithungu, akashindwa mwenyewe, akaniambia haya Go! better kilimanjaro Airport.
 
Asanteni sana Wakuu wahusika watalifuatilia hili tatizo na kupata ufumbuzi wake ingawa mpaka sasahayo matatizo bado yapo hayakwisha matatizo ya polisi kusmbuwa Raia na hata kudai Rushwa ya pesa sijuwi yatakwisha lini jamani asanteni.
 
Siku nyingine mkipaki mizigo pichu zenu ndio mziweke juujuuu ili wakiomba ifungue washindwe hata kuweka mkono
 
Back
Top Bottom