Ungekuwa wewe ungefanyaje?? Jamaa awavimbisha wawili kwa mpigo..

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66
Nilikuwa nasikiliza Radio Maria jana usiku mida ya saa mbili hivi ya usiku,
kama kawaida leo kulikuwa na kisa kingine, acha bwana duniani kuna mambo.
Kisa chenyewe ni hichi,

Nilikutia kati lakini kwa haraka ni kuwa kuna Mwana Dada mmoja ameolewa na wanaishi pamoja na mume wake na walikuwa na msichana wa kazi (House Girl/ Maid), Huyo mdada alikuwa anafanyakazi lakini huyo mume alikuwa hafanyi kazi kwa wakati huo haya yakitokea na walikuwa hawajafanikiwa kupata mtoto.
Kutokana na kazi huyo Mdada huwa anaondoka nyumbani asubuhi na kurudi jioni karibu kila siku. Yule mdada alianza kusikia kwa majirani kuwa yule jamaa hana tabia nzuri, alikuwa "anatembea" na yule msichana wa kazi na pia alikuwa anatongoza tongoza wanawake wa hapo mtaani na amekwisha tembea na wasichana/wanawake kadhaa wa hapo mtaani.
Baada ya kusikia hivyo akatafuta jinsi ya kujua ukweli wa hili suala, kutokana na ratiba yake ya kazi akaona njia nzuri ni kuleta mdogo wake aje akae pale nyumbani ili awe kama mchunguzi wake japokuwa hakuwa amemwambia kuhusu huyo kazi kwani aliona ni wazi kama kuna vitu visivyo vizuri vinaendelea kwa mme wake ni wazi mdogo wake angemwambia tu.

Muda ukapita bila kusikia lolote kutoka kwa mdogo wake na zile story za mtaani zikiendelea. Baada ya muda hivi hali ya pale nyumbani ikaanza kibadilika. Yule msichana wa kazi akaanza kulalamika mara kwa mara kuwa anajikisika mgonjwa huku akitapika tapika, punde na yule msichana mwingine (mdogo wa yule mke) na yeyey akaanza hali kama ile ya yule house girl kuugua mara kwa mara pamoja na kutapika tapika.

Kuona hivyo yule mdada siku moja akaomba ruhusa kazini na kuwachukua wote wawili na kuwapeleka hospitali kwa ajili ya vipimo, walichekiwa na wote kuonekana wanafanana kwa kila kitu, wote wawili walikuwa na malaria na pia walikuwa wajawazito. Akarudi nao nyumbani akawaweka kitimoto mme wake nae akiwepo ili wataje ni wa kina nani walio wapa hizo mimba ili waone hatua cha kuchukua. Lakini wale wasichana hawakutaja mtu huku wakati wote wakiwa wanamuangalia yule jamaa. Baada ya kugoma kutaja akaachana nao siku hiyo na kama baada ya siku 2 akamhoji kila mmoja kivyake. Kutahamaki wote wakamtaja kuwa yule jamaa (Mume wa huyo Mdada) ndio aliowapa mimba.
Duh kusikia hivyo yule mdada akachanganyikiwa asijue nini cha kufanya,
baada ya mume wake kampa mimba msichana wa kazi pamoja na mdogo wake (mdogo wa huyo Mke wa jamaa).

Aliona uamuzi mzuri ni yeye kuondoka na kuwaachia nyumba hao wasichana wajawazito na mume. Kabla hajachukua uamuzi akapeleka radioni kupata ushauri wa nini cha kufanya.
Kuna watu walipiga simu na wengi waliangukia katika makundi haya 3 walisema aondoke kwani kilikuwa ni kitendo cha aibu sana, wengine wakasema aendelee kukaa na mume wake ila awafukuze wale wasichana na wengine wakasema waendelee kuishi tu kama sasa awaache wale wasichana wakae hapo wajifungue na wawatunze tu hao watoto.

Ungekuwa wewe ungefanyaje? ama unamshauri nini huyu dada?

N.B: Hiki ni kisha cha kweli
 
hiki kisanga kweli lakini siku zote watu tutatoa ushauri tutaimba weeeeeeee mwisho wa siku mwenye kutoa maamuzi ni mhusika binafsi na nafsi yake

Kwa hapo inabidi akae chini ,afikirie kwa busara anahitaji nini
 
Ingekuwa wewe na wivu wako huo ungekaa chini ufikirie kwa busara? Acha kumdanganya mwenzio. Cha msingi hapo ni kuanza mbele na maisha mapya.
 
Ingekuwa wewe na wivu wako huo ungekaa chini ufikirie kwa busara? Acha kumdanganya mwenzio. Cha msingi hapo ni kuanza mbele na maisha mapya.

Umejuaje FL1 ana wivu?
Hiki kisa kimenikumbusha jamaa mmoja mtoto wa family friend wetu nae alishawahi kuwapa mimba wanawake wawili kwa wakati mmoja na watoto wakazaliwa wote wa kike na wote wakaitwa jina moja la mama yake, ilikuwa kasheshe wadada walikua wanawindana kama ndege siku mmoja akipata taarifa kuwa mwenzake kasafikri anahamia kwa jamaa siku akirudi anakuta mwenzake kajaa ndani ya nyumba kwa hiyo ikabidi mmoja apangishiwe chumba na mwingine abaki kwa jamaa.

Kwa ushauri hapo ni ngumu ni kumwacha mhusika mwenyewe aamue cha kufanya maana nakumbuka hata kwa huyo jamaa hatukutoa ushauri wowote tuliwaacha wenyewe wakaparangana na mwisho wa siku kila mdada akamkataa jamaa,mmoja akamwambia hata mtoto sikupi naondoka nae na yule mwingine akamletea jamaa mtoto akamwambia wakati tunafahamiana ulinikuta sina mtoto kwa hiyo chukua mtoto wako ndo ikawa mwisho jamaa akaoa mdada mwingine. Kwa hiyo huyo mama mwenye nyumba akae tu chini atafakari na kama ni maamuzi ayatengeneze mwenyewe kwa kuusikiliza moyo wake ikizingatiwe kwamba yule ni mume wake.
 
Ingekuwa wewe na wivu wako huo ungekaa chini ufikirie kwa busara? Acha kumdanganya mwenzio. Cha msingi hapo ni kuanza mbele na maisha mapya.

Chrispin ndo maana nimeshindwa kumshauri ,kwa sababu maamuzi yangu ningeyajua mie mwenyewe ...
 
Umejuaje FL1 ana wivu?
Hiki kisa kimenikumbusha jamaa mmoja mtoto wa family friend wetu nae alishawahi kuwapa mimba wanawake wawili kwa wakati mmoja na watoto wakazaliwa wote wa kike na wote wakaitwa jina moja la mama yake, ilikuwa kasheshe wadada walikua wanawindana kama ndege siku mmoja akipata taarifa kuwa mwenzake kasafikri anahamia kwa jamaa siku akirudi anakuta mwenzake kajaa ndani ya nyumba kwa hiyo ikabidi mmoja apangishiwe chumba na mwingine abaki kwa jamaa.

Kwa ushauri hapo ni ngumu ni kumwacha mhusika mwenyewe aamue cha kufanya maana nakumbuka hata kwa huyo jamaa hatukutoa ushauri wowote tuliwaacha wenyewe wakaparangana na mwisho wa siku kila mdada akamkataa jamaa,mmoja akamwambia hata mtoto sikupi naondoka nae na yule mwingine akamletea jamaa mtoto akamwambia wakati tunafahamiana ulinikuta sina mtoto kwa hiyo chukua mtoto wako ndo ikawa mwisho jamaa akaoa mdada mwingine. Kwa hiyo huyo mama mwenye nyumba akae tu chini atafakari na kama ni maamuzi ayatengeneze mwenyewe kwa kuusikiliza moyo wake ikizingatiwe kwamba yule ni mume wake.

kwi kwi kwi ngoma ukiipiga lazima ucheze ..kuna watu kweli wanayaweza
 
Chrispin ndo maana nimeshindwa kumshauri ,kwa sababu maamuzi yangu ningeyajua mie mwenyewe ...

Hahaha! Kwa jinsi navyokujua na kawivu kako ungeshatimka zako. Humu jamvini mvumiliwa wa ukweli ni MJ1 tu.
 
huyo dada asepe zake amwache jamaa na wajawazito wake wawili. ikiezekana afile divorce kabisa au ampe talaka apate kujua ustaarabu mwingine wa maisha yake.
huyo braza na yeye lol yani anakula vitu hapo ndani kwa ndani!!!changanya hausigeli na shemegi
 
Jamaa hachezi mbali? Ni balaa huyu! Lakini hao wasichana nao hamnazo, wanakubalije kucheza na hilo limjamaa, tena peku? Hapo kila mtu alipie dhambi zake. Wenye mimba wazilee, wazae. Aliyewapa mimba atajiju, alifikiria nini, akawatafutie pa kukaa. Mama mwenye nyumba ajitafiti alipokosea, akipaona naye alipie kosa lake.

Kwa kifupi, kila aliyelikoroga alinywe!
 
huyo dada asepe zake amwache jamaa na wajawazito wake wawili. ikiezekana afile divorce kabisa au ampe talaka apate kujua ustaarabu mwingine wa maisha yake.
huyo braza na yeye lol yani anakula vitu hapo ndani kwa ndani!!!changanya hausigeli na shemegi

Kuna ubaya gani kama wote wanataka? Acha awape ile kitu roho zao inapenda.
 
Hahaha! Kwa jinsi navyokujua na kawivu kako ungeshatimka zako. Humu jamvini mvumiliwa wa ukweli ni MJ1 tu.

mj1 i salute 2 her du ni mvumilivu kweli yule dada

ngoja aje amshauli huyu jndugu tusikie mawazo yake :)
 
Kuna ubaya gani kama wote wanataka? Acha awape ile kitu roho zao inapenda.

halafu hapo pia huyo dada naye anaeza kuwa na makosa. kutokana na kazi zake arudi usiku kuondoka alfajiri hapati muda wa kukaa na mumewe faragha anampa haki yake kwa bajeti jamaa akajionea bora nile vya humu humu ndani ambavyo havina hata bei zaidi ya maneno matamu.
saa zingine wanawake wana makosa ila wanaishia kulaumu wanaume tuu something which aint right kabisa.problem na professional ladies wana mambo hao
 
Ni bora ameziona hizo mimba alizoletewa, Je angeletewa Ukimwi ungeujuaje mapema kiasi hicho.

Cha Msingi uamuzi ni mtendwa, lakini angalizo ni kuwa mume wake, hamuheshimu, hajiheshimu na uaminifu kwake ni Negative, Ni bora akaanza mbele ili mbele ya safari waendelee kuwa na mahusiano na mdogo wake.
 
halafu hapo pia huyo dada naye anaeza kuwa na makosa. kutokana na kazi zake arudi usiku kuondoka alfajiri hapati muda wa kukaa na mumewe faragha anampa haki yake kwa bajeti jamaa akajionea bora nile vya humu humu ndani ambavyo havina hata bei zaidi ya maneno matamu.
saa zingine wanawake wana makosa ila wanaishia kulaumu wanaume tuu something which aint right kabisa.problem na professional ladies wana mambo hao

Am trying to figure JS, ungekuwa na wewe upo kwenye mazingira km haya ungetekeleza km jamaa alivyofanya.

Acha hizo ni lazima uwe na miiko JS. Ni kumdhalilisha mkeo kuchangia penzi na HG au Mdogo wake.
 
hii ni kali na kwa kweli uamuzi anao huyo mdada mwenyewe, ajiulize maswali kadhaa- bado anampenda mumewe baada ya kujua hayo? yuko tayari kumsamehe kabisa na kuendelea kama kawaida na mumewe?Kama majibu yote ni ndio na amesamehe toka ndani ya moyo wake na kusahau na yuko tayari kuendelea kuishi na mumewe asamehe na afungue ukurasa mpya kama laa aanze mbele kivyake!
 
aaaah mie hapa sisamei hili jamaa linaweza kubaka kabisa :)
 
Hapa hakuna cha kujishauri,jamaa mwenyewe hana kazi kazi yake ndio kumimbalaize watu tuu,mama fungasha vilago uondoke,ukisubiri tuu utaletewa ngoma!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom