Ungekuwa rais ungefanya nini?

ni kuwanyima kura tu,
huu muda tuendelee kuwatazama na hivyo vituko vyao wanavyotufanyia
tuviweke kwenye kumbukumbu, kwa kuwa siku yao itafika tu.

Ndio maana tunajadili. Nyumba yenye baba usiyetofautishwa na watoto, ni hatari. Nchi yetu inaangamia jamani. Tufanye kuiokoa maana tuliowapa dhamana heri wangelala bali hawafanyi tulichowatuma na wanatutusi!
 
Tafadhali naomba mchango wa kila mdau hapa. Kadri mambo yanavyoendeshwa endeshwa na serikali naona ama kichwa changu kina tatizo ama ndio ukweli wa mambo. Labda kukubaliana na hali naomba michango ya mawazo ya kila mdau kuwa endapo utakuwa rais wa nchi hii ungefanya nini kuhusu mambo yafuatayo ili kuwanusuru watz na janga kubwa la umasikini;

1) KILIMO
2) AFYA
3)MALIA ASILI NA UTALII
4)VIWANDA NA BIASHARA
5)NISHATI
6)ARDHI
7) ELIMU
8) MADINI

9) UJENZI NA MIUNDO MBINU
10) USAFIRISHAJI
11) RUSHWA NA UFISADI
12) KUKOSEKANA AJIRA KWA VIJANA
13) BAJETI TEGEMEZI KWA WAHISANI

Toa mchango wako usipite tu, haijalishi wewe ni mtaaluma ama la, haijalishi wewe ni mrengo gani, toa mawazo yenye kuelimisha labda wataguswa pia. Si lazima kutoa mawazo kwa mada zote bali ile unayodhani unaweza.

Asanteni.
 
Ningekuwa rais kama aliyekuwepo au vipi?

Kwa kuwa kama rais wa sasa ningetangaza NIMESHINDWA KUONGOZA nchi.

Vinginevyo ningefuta chama tawala maana wanatoa povu baada ya kuvimbiwa lawama naibeba peke yangu.
 
Wana jamvi kama tank la great thinkers tujaribuni kushauri ama kupendekeza mambo ya kufanya ili kunusuru hali tete inayotokea mtwara bila kuathiri usalama wa nchi na raia kwa ujumla! toa pendekezo kwa manufaa ya nchi bila kujali itikadi ya chama.
 
Watanzania wote wajua kuna siasa nyuma ya vurugu hizi, wanasiasa walioko nyuma ya vurugu hizi waambiwe waache mara moja mchezo huo na ikinidi wapewe muda wa saa 24 la siyo sheria ichukue mkondo wake na wakabiliwe na kosa la uhaini
 
Serikali isitishe ujenzi wa bomba la gesi. Ijenge viwanda inavyoahidi huko mtwara gesi ipelekwe huko kwanza ndipo iende dsm au dodoma au zanzibar
 
Hatumpi faida JK, maana atacopy na kupaste!
Mambo mengi yenye nafuu waliyoyafanya huko ccm so far ni yale ya copy and paste toka cdm!
Kama aligombea urais ina maana anaweza, acha awashirikishe akina Mwigulu wafanye wanaloweza!
 
In JK's shoes - in perspective, nimejivika uprezdaa......na sasa niko Mtwara.

1. Naitisha Kikao cha Viongozi wa Mkoa, napewa Taarifa na kuhoji hatua zilizochukuliwa kabla na baada ya fujo na uharibifu wa mali na madhara kwa maisha ya watu kadhaa.
2. Naitisha kikao cha viongozi wa makundi yote ikiwemo vyama vya upinzani, wanawake, vijana,wazee, bila kusaha viongozi wa kidini wa Mkoa, na kuwasikiliza kwa kina hoja zao kuhusu Bomba la Gesi kutoka Mtwara kwenda Dsm.
3. Napima hoja za wana-Mtwara na mustakabali wa maendeleo yao kutokana na raslimali zilizoko katika Mkoa wao na maendeleo ya Taifa zima kwa jumla.
4. Nafikia maridhiano na wanchi wa Mtwara juu ya uendelezaji wa miradi ya kuvuna raslimali, faida ya moja kwa moja kwa wananchi wa Mtwara na jinsi watakavyofaidi kutokana na vyanzo hivyo vipya vya mapato katika mkoa wao.
5. Napanga muda wa kufikia malengo yaliyoazimiwa na kuridhiwa na wana-Mtwara, wananchi wanaeleweshwa na hadi hapo hali itakavyoniridhisha kuwa tumekubaliana na tumeelewana, ikibidi kukaa Mtwara majuma mawili hakuna shida, cha msingi ni suluhu ya kweli ipatikane.
6. Hatimaye mambo yanakuwa shwari na tunaelekea kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
7. Nawasiliana na BAKWATA, Baraza la Idd kitaifa lifanyike Mtwara, nami naenda kushiriki na wana-Mtwara kula Idd-el-Fitri ili kujenga mahusiano mazuri na kuonyesha kuwa nawajali na kuwasilikilza shida zao.
8. Natoa maelekezo kwa viongozi wote wa Mkoa yote nchini Tanzania, kuhakikisha kuwa wanakuwa karibu na wananchi na kuwa na mikutano ya kusikiliza kero zao walau mara moja kila mwezi.

Mengine yanabakia kuwa kazi ya utekelezaji, na gesi ya Mtwara inaendelea kuzalishwa kwa maslahi ya kizazi hiki na kizazi cha baadae.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika!
 
Wewe mwenyewe ni prezidaa wa familia yako, Nenda katoe directives hz huko ila si kama rais wa nchi.
 
1. Ningeagiza majeshi ya ulinzi na usalama kuacha kutumia nguvu na kufanya ukatili kwa wananchi kama inavyoripotiwa wanafanya
2. Ningemuondoa Nchimbi kwenye nafasi yake kwa haraka kwa sababu ya kauli ya uchochezi wa vurugu kwa wanajeshi aliyoitoa leo bubgeni kwa kusema "damu yao haitamwagika bure" nini maana ya maneno hayo? si mmesikia leo Mtwara yanayoendelea ni mabaya kuliko ya jana?
3. Sospeter Muhongo na ubabe wake ningempiga chini haraka maana yeye ndiye chanzo cha vurugu hizi zote
4. Ningeagiza bunge liendelee na shughuli zake na kuacha kuingilia mihimili mingine na kumuonya spika
5. Ningewapa pole wanachi wa Mtwara kwa maswahiba ya jeshi lisilo na weledi (policcm)
6. Ningeagiza seize fire ndani ya dk chache maana wananchi wa Mtwara wasingechokozwa wasingepigana
7. Ningekaa mezani na wananchi wa Mtwara kujadili kwa upya mustakabali wao juu ya suala la gesi na kuhakikisha tunaelewana na kukubaliana juu ya modality ya namna ya kuendesha jambo hili
8. Ningetangaza kuwithdraw mpango wa serikali wa kulazimisha gesi kusafirishwa kwa mabomba kwani najua hautafanikiwa kwenye visasi na vurugu
 
1] kwanza ningewaambia watu waheshimu sheria za nchi

2] Ningeamuru vyombo vyote vya usalama viwajibike kuhakikisha hakuna mtu au mali itakayoharibiwa kwa kuvunja sheria za nchi.

3]watanzania waelewe hakuna rasilimali ya mtwara au kigoma rasilimali za nchi ni za watanzania wote

4]ningewaambia wanamtwara kuwa daraja la Benjamini mkapa halijajengwa na pesa kutoka mtwara limejengwa na pesa za watanzania.

5]Ningewaambia wanamtwara gesi iliyopatikana ni lazima iende Dar kwa sababu kuna viwanda vingi

na waelewe tukiwa na umeme wa kutosha gharama za uzalishaji zinakuwa chini, Na watanzania watanufaika ni pamoja na mtwara kwani mpaka sasa vijana wanasoma bure kwenye vyuo vya veta

na pia gharama za kuunganisha umeme mtwara ni za chini kupita mikoa yote ya Tanzania.

HITIMISHO KWA KUWA WANAMTWARA HAWANA HOJA ZA MSINGI NINGETANGAZA HALI YA HATARI KWA MKOA WOTE HAKUNA KUTOKA NJE YA NYUMBA ZAO NA PIA NIKIHAKIKISHA WANA USALAMA WOTE WAMEUZINGIRA MJI WOTE. NA ENDAPO KUNA ATAKAYEKAIDI LITAKALOMPATA AJILAUMU MWENYEWE.

Kwanza sitamani kuwa na akili kama zake.Hili swala ni dogo na linaweza kumalizika ikiwa viongozi wataachana na tamaa ya kujilimbikizia mali.Kwa mtazamo hiyo gesi ingeachwa mtwara na hicho kiwanda wanachotaka kujenga dar kikajengwe mtwara kwa maana napo ni tanzania
 
Jambo lililo wazi ni kuwa wanaMtwara wanpotoshwa na baadhi ya watu wachache na kwa hiyo la muhimu ni kuwatambua hao mbao kwakweli ni wachochezi(kwa maana halisi ya neno la uchochezi). Uchochezi wa kiwango hiki unastahili adhabu kali ikiwa ni pamoja n a kuwekwa kizuizini kwa maslahi ya Taifa
 
Hili mbumbumbu angalia lilivyokosa upeo sasa hapa umepinga nini mtu katoa mawazo au ulitaka alete malumbano kama yangu na yako hapa..nyie ndio kina mulongo nyie maguvu mengi bila akili...kwani akisema yeye ni prezidaa inabadilika kuwa kweli kuwa yey ni prezidaa..k*m* wewe ilibidi ujadili alichokiandika sio unamjadili muandishi..stupids pipo discus pipo great mind cjui nini nini ila i have the idea sasa wewe uko wapi?acha umburula
wewe mwenyewe ni prezidaa wa familia yako, nenda katoe directives hz huko ila si kama rais wa nchi.
 
Hii ndo karata yake ya mwisho kujiuzuru vinginevyo atakuja ozea the hague 2016

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kila kitu kimeshaongelewa na wana NTWARA wanajua kilichoongelewa na wamekielewa ila kuna watu nyuma ya pazia ndo wenye kutaka kuharibu mambo.
Ningekua ndo Braza K ningefanya jambo 1 tu

1} Ndani ya siku 2 hizi ningehakikisha wale vinara wa kuchochea vurugu japo wawili tu wanaamkia mabwepande najua hapo ningekua nimesolve kila kitu

REJEA MGOMO WA MADAKTARI SASA WAMESHIKA ADABU
 
Back
Top Bottom