Unene wa mke wangu unamuweka matatani

Sasa stress si angekonda stress gani ananenepa
Watu wakiwa na stress wana react tofauti, some tend to lose their appetite lakini wengine wanajifariji kwa msosi so they tend to over eat na kuongezeka uzito kwa kasi. Mpokee baadhi ya majukumu haswa yanayohusu watoto ili apate muda kwa ajili yake ndio ataweza kuwa na interest na vitu kama muonekano wake hata gym anaweza ku attend. Amezidiwa na majukumu, msaidie mkeo.
 
Nilifanikiwa kupata mwenza wa maisha (kuoa) mnamo mwaka 2006 kipindi ninaoa mimi nilikua na uzani wa kilo 50 na wife alikua na kilo 42 maisha yalisonga tukapata mtoto wakwanza. Wife alijifungua normal kabisa na tukalea mtoto wetu wa kwanza wife alikua na kilo 44 mpaka mwanetu anafikisha umri wa miaka mitatu mwaka 2009. Tukafanikiwa kupata mtoto wa pili ambae Mungu si athumani wife alijofungua salama pia na mpaka mwanetu anafikisha miaka mitatu wife alikua na kilo zile zile 44.

Hatujawahi kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango ila mnamo mwaka 2014 wife alianza kunenepa katika kipindi cha mwaka mmoja alitoka kilo 44 mpaka 76. Nilijitahidi kumshawishi japo kwa njia ambayo isinge mkwaza kua tuwe tunakimbia kimbia jioni wife akisikia swala la mazoezi anakua mkali nitanuniwa hata wiki tatu haongei yeye ni ku deal na watoto tu.

Ilipofika mwaka jana mwishoni wife alifikia kilo 95 kuna kipindi alikuwa anappata dalili za pressure tukaenda hospitali daktari alimshauri apunguze weight lakini alimgombeza daktari kama mtoto mdogo kua amuache yeye ni mtu mzima kama kumtibu ameshindwa aseme. Sikuwa na jinsi zaidi ya kua mpole na kupewa baadhi ya vidonge na kurudi nyumbani.

Mwezi uliopita wife amefika kilo 110 ambazo zinazidi kumuweka katika hatari yakupata magonjwa mengine ya hatari zaidi. Ameanza kukoroma kwa sauti kubwa sana usiku na akilala hataki umuamshe hata kama kuna kitu chochote kile amekua mkali sana na hata haki ya ndoa anasema anachoka sana skuizi ananipiga kalenda. Unene wa wife umekua ukinipa uoga na kumuonea mke wangu huruma sana hasa nikiona anapokua akilalamika miguu inamuuma.

Kuna siku nilijaribu kumwambia miguu inakuuma kwasababu ameongezeka uzito katika kipindi kifupi mno, hili lilizua ugomvi mpaka tukaenda kusuluhisha kwa wazazi baada ya miezi miwili ya kuvutiwa mdomo na kukosa amani ndani ya nyumba kwa kumshauri wife jambo la busara tu.

Kwa sasa nina kilo 54 wife anachezea 110 ninaomba ushauri nifanyeje wife anielewe na aweze japo kufanya mazoezi amekua kibonge sana na anapata matatizo ambayo yananiogopesha naweza kumpoteza mama watoto. Nilishawahi kujaribu kumshauri tujiunge kwa pamoja gym hilo ndilo lilizua maneno kuwa ninafuata wanawake huko gym namshangaa wife japo ni msomi ana masters yake ila haoni umuhimu wa afya yake.

Kitu kinachomfanya wife awe hivi ni kula kupita kiasi na kupenda sana vitu vya wanga kuna siku kulikua na birthday ya mwanetu alikula keki ya kilo tatu na ile sukari ya juu yote baada yakuwakatia watoto. Anaweza kutoka kazini akapita mahali akala hata kilo mbili za kitimoto, kuna siku nilimfuma anakula kitimoto bar kwa makadirio kilikua kama kilo 2 nikajaribu kudadisi nikagundua huwa ana desturi yakupita pale kila siku na ameweka oda kabisa na akifika nyumbani pia anafanya majukumu yake vizuri ikiwa ni pamoja na kuwapikia watoto na hula tena mara yapili na kulala akimaliza tu kula.

Ninaombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje kunusuru afya ya mke wangu.
 
Mi nimecheka hapo kwenye kula kilo 2 za kitimoto. Asee mwanamke unakula namna hiyo hatari, ndio maana anakuwa mzito kupita kiasi.
 
Pamoja na uwezekano wa stress lkn pia kuna ugonjwa wa kongosho unaowapata watu wa kisukari una dallili hizo za kuongezeka uzito kwa haraka namna hiyo ndani ya kipindi kifupi. Nendeni hospital kubwa kuangalia, yaweza tiba isiwe gym tu km unavyofikiri
 
Hivi wewe si ndio nimetoka kuchangia thread yako unasema huwezi kudumu na mwanamke zaidi ya siku nne? Eti ukisha do naye hamu inakuisha?

Au ndo umeamua kutuchanganyia madesa?
Kwa design hii ukute jamaa analala sebuleni kwa mjomba sasa kuvuta time watu wote walale anatunga stori. Usishangae baadae akaja na uzi kuwa mumewe hampi haki yake ya ndoa kusahau kuwa alishaanzisha mada kama mwanaume. Ukiwa muongo sharti uwe na kumbukumbu.
 
Dah huyo wife ni noumer...anapeleka pwani kg 2 za pork peke yake....hahahaha hatari sana. Pole sana mkuu ila hamna zoezi gumu kama kupunguza uzito. Inabidi ajitoe sadaka kweli kweli. Kama ana nia ya dhati ataweza vinginevyo jifunze kuishi naye kama alivyo.
 
Back
Top Bottom