Leo kuna njia mbalimbali za kuwasiliana ila kile kipindi tunaandikiana mabarua ",....kwako wewe uliyembali sijui na upeo wangu..,,.....," dhumuni la barua hii......"jamani barua (sio kadi) zimepoteza mvuto??? au ndo kwenda na wakati!
Barua za mapenzi zilikuwa nzuri na za kusisimua zaidi kuliko meseji za simu, kwa sababu.
SIMU HAZINA UTAMU
- Mtu alikuwa anaandika kitu alichokibuni kutoka moyoni
- Barua ilikuwa na michoro ya kusisimua yenye ishara za mapenzi
- Barua ilikuwa ndefu haaishi hamu
- Wakati mwingine ilikuwa na nyongeza ya mashairi au nyimbo za wakati ule ambazo zilikuwa zinasisimua sana sio hizi za sasa eti demu wangu, demu wangu sijui kachakachuliwa aaah!
- Mapenzi yake ni ya kompyuta yaani mtandao unatengeneza meseji za mapenzi wewe unatuma tu.
- Ujumbe wake ni mfupi sana na hauingii moyoni
- Ubunifu wa maneno matamu ya mapenzi unakuwa mdogo kwa sababu yanakuwa mafupi mno.
- Watu hawabuni kutoka moyoni ndio maana meseji ya aina moja unaweza kutumiwa na watu kumi tofauti Natamani zama za barua zirudi tena.
- Halafu unajua tu kuwa hizi ni kamba za mtandao
Maneno haya ilikuwa ni lazima yawepo: '... mpenzi ninakupenda sana, kula sili, kulala silali. Tafadhali naomba majibu mapema baada na hata kabla ya kupata barua hii ...' Lo, kilikuwa kipindi kizuri sana ambacho kizazi cha leo wanakosa mengi.
Niliacha kusoma na kuandika barua nilipoandikiwa mwishoni mwa barua ' usipopata hii barua nijulishe'
Niliishiwa nguvu kabisa