Unaweza kugonga Treni, au Kauli ya Kugonga Treni inatoka wapi?

Adil_101

Senior Member
Jul 26, 2022
110
339
Mara nyingi tumepata kusikia kuwa gari limegonga treni au wanyama wamegonga treni

Labda hata wewe umewahi kujiuliza msingi wa kauli hii ama sheria inayoongoza jambo hili na walioitunga waliwaza nini.

IMG_20230402_134630.jpg
 
Mara nyingi tumepata kusikia kuwa gari limegonga treni au wanyama wamegonga treni...
.
Labda hata wewe umewahi kujiuliza msingi wa kauli hii ama sheria inayoongoza jambo hili na walioitunga waliwaza nini...View attachment 2573969
Sasa nakupa summary fupi kuhusu hili swala la kugonga treni au kuhatarisha usalama wa treni..
.
Ili siku usije ona treni ukarusha Jiwe wazee wakakudaka ukaona unaonewa kumbe umevunja sheria..
.
Twende pamoja ndani ya dakika moja tu utakua ushamaliza na kuelewa..
IMG_20230402_134715.jpg
 
Sasa nakupa summary fupi kuhusu hili swala la kugonga treni au kuhatarisha usalama wa treni..
.
Ili siku usije ona treni ukarusha Jiwe wazee wakakudaka ukaona unaonewa kumbe umevunja sheria..
.
Twende pamoja ndani ya dakika moja tu utakua ushamaliza na kuelewa..View attachment 2573972
Sasa nilitaka nianze na definition ila natumaini kila mtu anaijua..
.
Kwanza kabisa tuelewe kwamba gari moshi au treni mwenendo wake unaongozwa na sheria ya Reli (Railways Act of 1977)..
.
Hii ni tofauti na magari na watumiaji wengine wa barabara ambao wanaongozwa na Sheria ya
IMG_20230402_134728.jpg
 
Sasa nilitaka nianze na definition ila natumaini kila mtu anaijua..
.
Kwanza kabisa tuelewe kwamba gari moshi au treni mwenendo wake unaongozwa na sheria ya Reli (Railways Act of 1977)..
.
Hii ni tofauti na magari na watumiaji wengine wa barabara ambao wanaongozwa na Sheria yaView attachment 2573975
Usalama Barabarani (Road Traffic Act)...
.
Kifungu cha 47 cha sheria ya reli kinahusu kuhatarisha usalama...
.
Kwa mujibu wa kifungu cha 47 cha Sheria ya Reli, mtu yeyote ambaye kwa kitendo chochote kisicho halali..
.
Kwa makusudi, kwa uzembe, au kwa kupuuzia, akafanya au
IMG_20230402_134827.jpg
 
Usalama Barabarani (Road Traffic Act)...
.
Kifungu cha 47 cha sheria ya reli kinahusu kuhatarisha usalama...
.
Kwa mujibu wa kifungu cha 47 cha Sheria ya Reli, mtu yeyote ambaye kwa kitendo chochote kisicho halali..
.
Kwa makusudi, kwa uzembe, au kwa kupuuzia, akafanya au View attachment 2573977
Akaacha kufanya lolote kati ya yafuatayo, anatenda kosa na akitiwa hatiani adhabu yake ni faini..
.
Faini isiyopungua shilingi milioni 5 au kifungo kisichozidi miezi 18 au vyote kwa pamoja, mambo hayo ni kama yafuatayo..
.
(a) Kuzuia au kusabaisha treni au au gari linalotumia
IMG_20230402_134848.jpg
 
Kiufupi ni kwamba treni ina barabara yake, na inajulikana.

Sasa wewe kitendo cha kwenda kwenye barabara yake ndio hapo tunasema umeigonga.

NB: kugongwa sio lazima wewe uwe mbele ya kichwa cha treni pale. We ukijileta pale ikakufumua basi wewe ndio mwemye makosa umeigonga treni
 
Akaacha kufanya lolote kati ya yafuatayo, anatenda kosa na akitiwa hatiani adhabu yake ni faini..
.
Faini isiyopungua shilingi milioni 5 au kifungo kisichozidi miezi 18 au vyote kwa pamoja, mambo hayo ni kama yafuatayo..
.
(a) Kuzuia au kusabaisha treni au au gari linalotumia View attachment 2573978
reli kuzuiwa;..
.
(b) Kuhatarisha au kusababisha kuhatarishwa kwa usalama wa mtu yeyote ndani ya treni au kwenye treni au gari linalotumia reli..
.
(c) Kuweka au kurusha kitu chochote kwenye reli..
.
(d) Kuchukua, kuondoa, au kutawanya reli au kifaa kingine chochote cha reli..
.
(e) Kurusha au kusababisha kudondoka au kupiga dhifi ya treni kwa kitu chochote ikiwemo jiwe au ubao kwa nia ya kujeruhi au kuhatarisha usalama..
.
(f) Kuwasha moto au kwa njia yoyote kuharibu reli au njia yake au stesheni ya treni, chumba cha injini,karakana au jengo lolote la reli au kitu chochote kilichomo..
.
(g) Kufanya jambo lolote kwa nia ya kuzuia,kuvuruga, kupindua, kuharibu,au kuleta madhara yoyote kwenye treni au gari linalotumia reli au kuhatarisha usalama wa mtu yeyote kwenye treni..
.
Na mtu yeyote atakayesaidia kufanyika kwa lolote
IMG_20230402_134949.jpg
 
Na mtu yeyote atakayesaidia kufanyika kwa loloteView attachment 2573983
Kati ya yaliyotajwa hapo juu pia anatenda kosa na faini yake ni shilingi milioni 4 au kifungo cha miezi 12 jela..
.
Aidha kwa mujibu wa kifungu cha 30(1) ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha kuwa awapo karibu na reli au treni kuenenda katika namna ambayo haitahatarisha usalama wa Watu wengine kutokana na matendo yake au kupuuzia tahadhari husika..
.
Na kwa mujibu wa kifungu cha 30(2) mtu yeyote anayeenenda katika namna ambayo inahatarisha usalama wa miundombinu ya reli au treni anatenda kosa..
.
Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 27 LATRA inahusika katika Kuhakikisha usalama wa undeshaji wa huduma za reli nchini Tanzania.
.
LATRA pia ndio inayohusika na uchunguzi wa ajali zote za treni.
.
Kifungu cha 29 pia kinamtaka mtoa huduma ya usafiri wa treni (operator) kuhakikisha usalama wa wanaoathirika na huduma yake.
.
Kwa hiyo basi
IMG_20230402_135318.jpg
 
Kwa hiyo basi View attachment 2573985
Unapokuwa umekatisha mbele ya treni linalokuja ukasababisha ajali au ya kugongwa wewe au gari lako au mifugo yako..
.
Unakuwa umeingilia njia ya reli au kuzuia (block) treni na pia kuhatarisha usalama wake..
.
Hapa ndipo dhana ya kuligonga treni inapokuja. dhana hii inakaziwa Na kifungu cha 55 kinachomlazimisha dereva kusimama kabla ya kuvuka makutano ya reli na barabara ili kujiridhisha kuhusu usalama wake..
.
Ni Imani yangu kwa makala hii utakuwa umeelewa kuhusu dhana ya kuligonga treni sasa itakua vyema ukigonga like na wengine wapate hii elimu...
IMG_20230402_135343.jpg
 
Unapokuwa umekatisha mbele ya treni linalokuja ukasababisha ajali au ya kugongwa wewe au gari lako au mifugo yako..
.
Unakuwa umeingilia njia ya reli au kuzuia (block) treni na pia kuhatarisha usalama wake..
.
Hapa ndipo dhana ya kuligonga treni inapokuja. dhana hii inakaziwa Na kifungu cha 55 kinachomlazimisha dereva kusimama kabla ya kuvuka makutano ya reli na barabara ili kujiridhisha kuhusu usalama wake..
.
Ni Imani yangu kwa makala hii utakuwa umeelewa kuhusu dhana ya kuligonga treni sasa itakua vyema ukigonga like na wengine wapate hii elimu...View attachment 2573987
Imeletwa kwako na..
.
RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote

Asante kwa kusoma.
IMG_20230402_135520.jpg
 
Ni kauli tata, bora wangesema reli ndiyo imegongwa kwa maana hayo mataruma yapo hapo hayajongei. Mtu au kitu kitagongaje treni, wakati treni yenyewe ndiyo inagonga? Labda dereva wa gari akute treni imepaki kwenye reli aigonge, hiyo kauli itaeleweka maana yake
 
Back
Top Bottom