Unatumia mbinu gani Kuishi na mwanamke na huna hela?? Nataka Nianze kuishi na mchumba wangu wa muda mrefu ila sina hela

Oyaa acha kuuliza maswali ya kijinga basi vipi wewe unafurahia watu wakikusaidia, kwa hali hii acheni tu hao wanawake waendelee kuwachuna, hakuna cha kuwavumilia wala kuwaonea huruma
Mboni unapanic hivyo tena 😂
 
Kama huna hela unachopaswa kufanya ni kumrhusu awe anadanga.

Halafu hela inayopatikana kupitia udangaji ndiyo itumike kuendesha maisha.

Huo ndiyo ujanja unaofanyika hapa mjini
Ha ha ha ha ha jamani
 
Yani ukisikia jinsi wanaume wanalalamika kuhusu wanawake utasema wanaonewa, na kwamba wao ni innocent na wana mapenzi ya dhati kwa wanawake, wakati hapo hata akisema akuvumilie ukizipata hakuna rangi ataacha kuiona
Akizipata anakuwa kware sahizi anamlalamikia tu mwanamke, siku zikamtembelee utasikia Nina ndugu zangu, mara wapwa zangu, mara oho mama yangu wakati ananiangaikia ulikuwepo hapo tayari anaenda kufuata anayefanana na pesa zake, wanawake shikirieni hapo hapo
 
Oohh kumbe lengo lako lilikuwa kunipanikisha, basi umefeli kwa sababu huna hoja za kunipanikisha mimi, next time try to make sense when you quote me
Sio kwa ajili ya kukupanikisha Ila nimeshangaa umepaniki kirahisi hivyo 😂
 
Akizipata anakuwa kware sahizi anamlalamikia tu mwanamke, siku zikamtembelee utasikia Nina ndugu zangu mara zangu mara oho mama yangu wakati ananiangaikia ulikuwepo hapo tayari anaenda kufuata anayefanana na pesa zake, wanawake shikirieni hapo hapo
Hahaha kwa kweli huu ulimwengu wa Sasa hivi ni wa kibepari hakuna kuoneana huruma
 
Hahaha kwa kweli huu ulimwengu wa Sasa hivi ni wa kibepari hakuna kuoneana huruma
Huruma atatuonea Mungu, mtu anaoa mke akiwa anajua ni kidato Cha nne hata kama STD seven, mke nyumbani na shughuli zake familia yeye anajiendeleza mpaka huko kama ni master sawa hapo kaoa akiwa na degree yake moja, akifika huko sasa matusi Kwa mke unajiuliza kwani wakati unamchumbia alikwambia ana PhD wewe ng'ombe ndama?
 
Ndio shida ilipoanzia mkuu alishapoteza imani tena kwako, hapo kwa vyovyote vile ataendelea kuamini kwamba unachepuka na ni lazima unahonga, hivyo hata ukimuambia huna hela hawezi kukuelewa lazima atahisi unazo ila unahonga tu

Sasa unashindwa kuelewa kampuni ya mumeo imefungwa msomi mzima na Degree yako. Ni mchoyoo tuu.
 
Mwisho mwanaume asiye na kazi kuishi na mwanamke ni miaka miwili hadi mitatu.

Baada ya hapo hakuna rangi utaacha kuiona wewe mwanaume.

Yaani hata kama hapigi kelele unahisi anakupigia mayowe.

Kiasili mwanaume hakuumbwa kuletewa na mwanamke; inatesa sana akili ya mwanaume na mwanamke pia.
 
Umesema kweli kabisa ,atakuvumilia mwisho atachoka,wanawake sisi ni bora tuhudumie watoto wetu lakini sio kumhudumia mtu mzima na ndevu zake ,wengi hua hawafanyi huo ujinga wa kulea marioo.

Mwanamme ni bora ujitafute kiuchumi ndio uoe ,sio kukimbilia kuoa ili jamii ikuone na wewe una mke wakati uchumi wa kulisha familia na kulipa kodi huna tena ukioa aliekuzidi kiuchumi ndio utajuta zaidi hakuna rangi utaacha kuiona,wachache naona wanawapa mitaji waume zao ili na wao wajitaute,ila sio wote wengi hawawezi.
 
Asheeena
 
🙄
Usikimbilie kwenye mahusiano kama huna kipato cho kueleweka, mambo mengine ni kujitafutia matatizo tu.
Unakuta mwanaume yuko na mwanamke na kamzalisha watoto kibao halafu maisha ya kuunga kwa kutegemea vibarua vya 3000 kwa siku.
Inatakiwa vibarua vya shilingi ngapi kwa siku?
 
Yani ukisikia jinsi wanaume wanalalamika kuhusu wanawake utasema wanaonewa, na kwamba wao ni innocent na wana mapenzi ya dhati kwa wanawake, wakati hapo hata akisema akuvumilie ukizipata hakuna rangi ataacha kuiona
Sasa ukikaa na mtu kwa kumnanga, kumsema vibaya, kumfedhesha, kumkejeli, kumdhalilisha, kumbania, na kumfanyia vituko kwasababu tu hana uwezo wa kifedha, unataka akifanikiwa aendelee kukaa na wewe ili agundue nini zaidi na umeshamuonyesha true colors zako.

A good woman character is seen when her man has nothing to his name, and a good mana character is seen when he has wealth to his name and plenty of women after him.

Kuwa makini sana namna unaishi na mwanaume ambaye hana kitu yaani yupo zero level ya Maisha kwasababu ndio muda atakutazama na kukuona kwa uhalisia wako na kila zuri utamfanyia litabakia kuwa sehemu ya kumbukumbu zake, kila baya utamfanyia litaacha makovu na madonda mabichi yasiyopona kamwe hata iweje na akifanikiwa kupata njia ya mafanikio hataweza kukushika mkono muendelee pamoja.
 
Wanaume tumeumbwa mateso,
Unamkumbuka yule shehe wa uamsho alieachwa na mkewe akiwa jela,

Alipoyoka kwny interview alisema

"Nilipokua jela, MKE wangu Akija kunitembelea, akiaga anaomba na Ela ya matumiz, Nabaki kujiuliza, mtu niko jela pesa ya matumizi kumpa natoa wapi"
Dah ila yule mke wa yule ustadhi sijui kama ana Amani huko aliko. Imagine alidhani mwanaume wake hatotoka ina maana hata kumuombea atoke alikuwa haombi alishamkatia tamaa. Kaenda kuolewa na kapata watoto wengine huko.

Jamaa katoka imagine maumivu yake aiseee. Imagine angemkuta mkewe bado anamsubiria jamaa angejiona ameoa malaika aisee.
 
Back
Top Bottom