Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Unapoulizwa swali, Kinachotakiwa ni jibu,
Usingoje mara mbili, na kutafuta sababu,
Wewe useme ukweli, au bora uwe bubu,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!!
Wewe toa hilo jibu, usiulize maswali,
Usipekue vitabu, jibu huna ukubali,
Ujibu kwa taratibu, bila kufanya ukali,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!
Ee ndugu habari gani, hilo ni swali rahisi,
Jibu lake siyo geni, akilini hulikosi,
Usiulize kwa nini?, wewe si Abunuwasi,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!
Kaka unakwenda wapi, akuuliza jirani,
Unajibu kwani vipi, siyo jibu ni uhuni,
Ukafanya chapichapi, mguu uko njiani,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!
Dada unaitwa nani, swali linataka jina,
Unauliza kwa nini?, hilo si jibu bayana,
Ni ujanja wa mjini, kwepa swali kiaina,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!
Hoja yangu nimeweka, swali halijibu swali,
Ujumbe uje kufika, zikue zenu kauli,
Na uhuni kuwatoka, mnapoulizwa swali,
Swali halijibu swali, kinachotakiwa ni jibu!!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)