Unamjua mdudu (malware) mbaya zaidi katika chombo chako cha mawasiliano?

x - mas

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
915
598
Habari zenu wanajukwaa, poleni na pilikapilika za hapa na pale za kutafuta mkate wa kila siku. bila kupoteza muda niende kwenye mada.

vifaa vyetu vya mawasiliano vinaweza kukabiliwa na malware mbalimbali ikiwa hatutakuwa makini katika mambo ya usalama katika matumizi ya vifaa vya mawasiliano, hata hivyo kwa kiasi fulani unaweza kushambuliwa na malware hatakama utakuwa makini katika usalama kutumia vifaa vya mawasiliano lakini madhara yanaweza kuwa madogo kulinganisha na mtu ambaye siyo makini kwa suala zima la usalama.

Malware ni nini?

ni ufupisho wa maneno malicious software, malware ni programs ambazo zinaingizwa katika kifaa chako kupitia udhaifu uliopo kwenye kifaa chako, programs hizo zinakuwa na malengo mbalimbali kulingana na aina ya malware.

Aina za malware:
  • virus
  • bot
  • ransomware
  • trojan horse
  • adware
  • spyware
  • rootkit
  • scareware
  • worm
  • MitM
  • Mit Mo
Malware yupi ni mbaya zaidi?
Nitaelezea madhara yanayoweza kuletwa na kila aina ya malware anapoingia katika kifaa chako, kujua malware yupi ni mbaya zaidi hiyo kazi nakuachia wewe, najua nikukuelezea tabia na madhara ya kila malware basi utajua ni yupi mbaya zaidi kulingana na vipaumbele vyako katika maatumizi ya vifaa vya mawasiliano. Naamini tunatofautiana matumizi hivyo aiwezekani wote tukawa na jibu moja incomon kuwa malware wa aina fulani ni mbaya zaidi.

Virus
Virus au kirusi ni malware ambaye uhusisha maelekezo / codes ambazo zinaambatanishwa au kuchanganywa katika codes za program yoyote halali ambayo unaitumia kwa shughuli zako, kirusi akiingia anaweza kuharibu files, kufuta data au kubadilisha data / modify. baadhi ya virusi wanatengenezwa wakiwa na uwezo wa kujibadilisha / mutate kila baada ya muda fulani ili kukwepa kugundulika kuwa anaishi katika kifaa chako. Njia ambazo kirusi huingizwa katika kifaa chako ni kupitia USB drives, optical disks, network sharing au email.

Bot / robot

huyu yeye yupo kwaajiri ya kufanya tendo fulani katika kifaa chako mara nyingi unapokuwa online, kompyuta nyingi zinazo malware huyu bila mtumiaji kujua na anakuwa hana madhara hadi pale alliyemtuma/attacker atakapo amua kum-command afanye tendo fulani katika computer yako.

Ramsomware.

kama jina linavyoashiria romson(fidia) walware huyu lengo la kuingia katika kifaa chako ni kufungia / isolate / encrypt data zako muhimu kiasi kwamba haitakuwa rahisi kuzifungua naweza sema kwamba mshambuliaji anateka data zako kwa kutumia ransomware, lengo la utekaji huu ni malipo, inamaana lazima umlipe ili aziachie huru data zako.

Trojan horse
kwa wale wapenzi wa movies za panga za kigiriki mtakumbuka namna wagiriki wazamani walivyokuwa wanatumia farasi wa kuchongwa kubebea wanajeshi na kuwaingiza katika mji kwa ajiri ya mashambulizi ambayo hupelekea kushinda vita kirahisi(check movie ya troy).

Turudi ki tehama dhana hii ya mbinu ya kigiriki ndiyo inayotumika kuhusianisha malware trojan horse. Trojan horse malware anatangenezwa kufanana na program yoyote ambayo hupendwa zaidi mfano visual studio, games au media player yoyote lakini ndani ya program hiyo fake kunakuwa na codes kwaajiri ya kufanya uharifu katika kifaa chako mara nyingi trojan horse hubeba malware aina ya viruses. kwamaana hiyo mtu anaweza akadownload program fulani akijua ni program og kumbe ni fake ingawa inafanya anachokitaka lakini kuna mambo mengine yanafanyika bila yeye kujua.

OIP.jpeg

Farasi wa kuchongwa aliyebeba wanajeshi wa kigiriki

Spyware
Malware huyu anapoingia kwenye kifaa chako kazi yake kubwa ni kukupeleleza na kukusanya taarifa zako mbalimbali mfano sites unazotembelea, programs uanazotumia, taarifa zako zingine zilopo kwenye kifaa chako lakini pia spyware anaweza kufanya kitu kinaitwa keystroke collections (matumizi ya keyboard). spyware anatabia nyingine ya kuboresha mazingira ya usalama uliyo ya-set ili asiweze kugundulika kiurahisa. kama nikiulizwa ni malware yupi ni mbaya zaidi kwa mimi namba moja ningemuweka spyware namba mbili rootkit.

Adware
Huyu lengo lake ni kusaidia kufikisha matangazo hasa ya kibiashara kwa mtumiaji wa kifaa cha mawasiliano mfano smartphone, kompyuta au tablet. malware huyu uingia katika kifaa chako kupitia matoleo mapya / version za software mbalimbali. baadhi uingia adware kama adware lakini baadhi pia huambatana na spyware.

Rootkit

Huyu anatumia udhaifu uliopo kwenye program endeshi (operating system OS mfano windows ) ya kompyuta kisha tengeneza kitu kinaitwa backdoor / mlango wa nyuma ambao utamewezesha mshambuliaji kuweza kuendesha kompyuta yako kama yake vile huku akiwa eneo la mbali kwa maana hiyo hiyo mshambuliaji anaweza kubadilisha chochote katika compyuta yako hii inapelekea kuwa ni vigumu sana kugundulika uwepo wa shambulizi katika kompyuta.

Scareware

Hii ni program inayotengenezwa kwa lengo la kumshawishi mtumiaji kufanya jambo fulani mara nyingi huwa kama inamtia hofu, mfano wakati mtuamiaji anapotumia OS inaweza kuingia ujumbe unaofanana na jumbe za OS ikimpa taadhari kuwa kuna uvamizi wa malware hivyo ili awesalama obonyeze scan, kitando cha mtumiaji kufuata hayo maelekezo tayari anakuwa ameruhusu malware kuingia katika kifaa chake.

Worms

Hii ni program ambayo inajiongoza yenyewe haitaji mtu kuiongoza, program hii pindi inapofanikiwa kukuta udhaifu na kuingia katika kompyuta basi ujitoa nakala nyingi hivyo kasi nakala hizo zinaanza kusambaa kwenye mtandao kila zinapoathiri kompyuta zinaendelea kujizalisha. mfano mwaka 2001 red worms awali walivamia servers 658 lakini baada ya masaa 19 tu worms hao walijizalisha na kuvamia servers 300,000 kote duniani. madhara ya worms ni kama kufuta mafail, kutumia njia yote ya mawasiliano(bandwidth) hivyo kufanya mtandao kuwa slow sana na kusaidia kuingiza malwares wengine.

UVAMIZI WA AWALI WA RED WORMS 2001
download.png

BAADA YA MASAA 19 BAADAE
download (1).png

Man in the Middle (MitM) .
Hizi ni progam ambazo zinamuwezesha mshambuliaji kuweza kuzidaka taarifa zako ulizotuma kabla hazijafika mahali ulipo kusudia, programs hizi hutumika mara nyingi kwa lengo la kupata taarifa za kifedha ili uwizi uweze kufanyika.

Man in the Mobile (MitMo)
Ni aina ya MitM ambayo inaendeshwa katika mobile devices / vifaa vya mkononi mfano simu. Mfano wa MitMo ni Zeus ambayo ni program yenye uwezo wa kujua taarifa zinazotumwa (ikiwemo namba ya siri) kwa njia ya sms kutoka kwa mtumiaji.

Nimatumaini yangu somo litakunufaisha, tuvumiliane kwa uandishi wangu wa ovyo hasa kwenye r na l, h n a,e...
 
Back
Top Bottom