"Unakwenda wapi"; "Unatoka wapi" Maswali yenye dalili za matatizo kwenye mahusiano?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,996
Hivi mtu akiuliza maswali haya ina maana gani katika mahusiano? Je uhusiano unaweza kuimarishwa kwa maswali haya au ni dalili ya matatizo? Kama watu wanamawasiliano mazuri kwanini haya maswali yanatokea? Je nilazima kuaga kila ukitoka. Na katika mahusiano kuagana au kuombana ruhusa ni muhimu?
 
haya maswali ni dalili ya kupungaua kuamininia ikiwa yanaulizwa katika kutia shaka, si mabaya kama yanaulizwa katika upendo lakini bahati mbaya iliyopo; mara nyingi maswali haya yamekuwa yakiulizwa wakati tayari muuliza swali hamwani mwenye kujibu hii ikiwa na kutoamini hata jibu litakalotolewa. Ni ugonjwa mbaya sana kama wewe upo kwenye hali hii na unahitaji jitihada kujinasua maana tiba ni wewe mwenyewe kuanza kujiamini ndipo utamwamini na mwenzi wako.

Kuhusu kuaga hili linategemea mazoea ya wanafamilia lakini si lazima na inategemea pia na sehemu uendayo umbali ama muda utakaokuwakuwako huko........suala la kutaarifiana ni jema lakini lisichukuliwe kuwa ni sheria ambayo ikivunjwa inawakosanisha.
 
damn straight muhimu kuaga....sasa wewe wakurupuka waenda wapi ? ukifa huko hujui kuwa utakuwa wamuweka mwenzio roho juu juu?
kuaga kunaonyesha kuwa unamjali mwenzio....na respect ni muhimu katika mahusiano yoyote. kama unataka kuwa free basi kuwa single...lakini ukishaingia kwenye uhusiano kuaga na kusema upo wapi ni unwritten rule!!!!
 
ww,katika mahusiano ni lazima awepo kiranja ambae mara zote tunaamini ni mwanaume! kumuaga mpenzia kisheria ya imani yangu ni amri!!sasa kama hujaaga unakwenda wapi swali kama unatoka wapi lazima liwepo!!!
 
Swali la kuulizwa kuwa umetoka wapi huwasilipendi, lakini kuulizwa kuwa unakwenda wapi, sio siri hilo swali huwa naema ninapokwenda incase kunawezakutokea matatizo au kitu chochote janua nimemtaarifu mwenzangu basi atajua paakuanzia kunitafuta, nahuwa simdanganyi kwa hilo
 
naamini ni vyema wewe utokae umwarifu mwenzako unakoenda japo wengi husema tofauti na waenakoelekea mtu anakuambia anaenda ubungo kutoka magomeni kumbe anaenda kawe ... hata kama kuna matatizo yanatokea inakuwa ni ngumu kupata msaada wa kifamilia.
 
Sasa ukiaga kuwa unakwenda mahali x na kumbe unaenda mahali y bado utakuwa umetimiza wajibu?
 
Sasa ukiaga kuwa unakwenda mahali x na kumbe unaenda mahali y bado utakuwa umetimiza wajibu?

Moja kati ya maswali ambayo siyapendi...saa nyingine mtu anajua kabisa upo kazini lakin atapiga kukuuliza upo wapi?unafanya nini?dah majibu yake kama nina stress zangu za kaz ni simple tu....nipo msalan cha kwamba nafanya nini jibu atakuwa nalo kwa huo muda
 
PAMOJA N MASWALI HAYA KUUDHI......kwa upande mwingine hebu jiulize utajiskiaje pale ambapo mwenzio hakuulizi kitu.Unenda huulizwi.......unarudi huulizwi............ siku nenda rudi...utajisikiaje?
 
PAMOJA N MASWALI HAYA KUUDHI......kwa upande mwingine hebu jiulize utajiskiaje pale ambapo mwenzio hakuulizi kitu.Unenda huulizwi.......unarudi huulizwi............ siku nenda rudi...utajisikiaje?

mmh kwa kweli hiyo ni dalili kuwa uhusiano umefika magogoni...
 
Back
Top Bottom