Unakuta BUS limeandikwa VIP/VVIP lakini likifika mahali linapandisha abiria wasiokuwa na Seat (wanasimama)

Mr Nyau

JF-Expert Member
Oct 18, 2018
1,129
2,339
Unakuta BUS limeandikwa VIP/VVIP lakini likifika mahali linapandisha abiria wasio na siti

Kuanzia Ally stars BUS wanaoisifia , katarama BUS na Bus zingine nyingi hali hii inafanyia abiria wake.

Unakuta umepanda bus kila abiria amekaa katika seat yake ikifika mahali Bus linaruhusu kupakiza abiria wengine wanaanza kusimama pembeni ya seats za abiria wengine wanakaa katika njia za kupita.

Nini maana ya Bus kuipa Hadhi ya VIP/VVIP?

Wamiliki wa Bus suala hili mnalifahamu?

- Ni bus gani haina tabia hizi?
 
VIP kibongo bongo bado sana, ndio tunajifunza tuseme ukweli tu... Labda miaka michache ijayo tutafika

Sasa hivi sio ajabu kukuta gari ni VVIP lakini choo kibovu, AC ya magumashi, mwendo wa dereva ni kanyaga twende babaakee, movie zilezile kila siku za mkojani, Ringo, Nagwa... Customer care mbovu, usalama wa mizigo muda mwingine mdogo kwa hiyo ni vuruguvurugu

Kuna bus (Sitalitaja) nilipanda kwenda mkoani nikajutia kutoa hela yangu kwamba nimepanda VIP.
 
Miaka ya nyuma nilibahatika kupanda bus ilikua na hadhi ya VIP kiukweli niliifurahia ata abiria wake walikuwa watulivu na wastaarabu, video zilizokuwa zinaoneshwa pamoja na mpangilio wa nyimbo katika bus hilo lilimfanya abiria ajihisi yupo katika sehemu salama sana ubora wa viti vyake na hata eneo la choo.

Tofauti na bus za siku hizi nyingi bus lina AC lakini abiria anafungua fungua madirisha , mfumo wa music mbovu upangiliaji wa music na filamu mbovu inafikia hatua unajua kabisa baada ya hii nyimbo inafuata nyimbo gani muda wote abiria unakuwa upo katika hofu KILA abiria anaetaka kushuka unakuwa na wasiwasi nae.
Kuamshwa amshwa kwenye seat mara ticket

Abiria anafahamu kabisa kuna mahali utafika utapewa breakfast na food bites lakini ndio kwanza kuanza kuagiza maembe mahindi ya kuchoma na kuchemsha hali ya Hewa kwenye bus inabadilika
 
Tofauti na bus za siku hizi nyingi bus lina AC lakini abiria anafungua fungua madirisha , mfumo wa music mbovu upangiliaji wa music na filamu mbovu muda wote abiria unakuwa upo katika hofu KILA abiria anaetaka kushuka unakuwa na wasiwasi nae.
Kuamshwa amshwa kwenye seat mara ticket
Ni kweli, safarini ni sehemu ya kutuliza mawazo na kupata utulivu lakini kukiwa na mihangaiko na usumbufu wa hapa na pale kiukweli inakera sana

THAMANI YA HELA iendane na huduma itolewayo, siku hizi naona wameona sifa kukimbizana kuwahi kufika kuliko usalama wa abiria
 
Miaka ya nyuma nilibahatika kupanda bus ilikua na hadhi ya VIP kiukweli niliifurahia ata abiria wake walikuwa watulivu na wastaarabu, video zilizokuwa zinaoneshwa pamoja na mpangilio wa nyimbo katika bus hilo lilimfanya abiria ajihisi yupo katika sehemu salama sana ubora wa viti vyake na hata eneo la choo.

Tofauti na bus za siku hizi nyingi bus lina AC lakini abiria anafungua fungua madirisha , mfumo wa music mbovu upangiliaji wa music na filamu mbovu inafikia hatua unajua kabisa baada ya hii nyimbo inafuata nyimbo gani muda wote abiria unakuwa upo katika hofu KILA abiria anaetaka kushuka unakuwa na wasiwasi nae.
Kuamshwa amshwa kwenye seat mara ticket

Abiria anafahamu kabisa kuna mahali utafika utapewa breakfast na food bites lakini ndio kwanza kuanza kuagiza maembe mahindi ya kuchoma na kuchemsha hali ya Hewa kwenye bus inabadilika
1. Kajifunzeni South Africa basi halina Kondakta Wala kugawana pipi/biskuti/maji/soda. Vyote unapata hotelini/supermarket mtakaposimama kupata chakula

2. Mwendo wa wastani. Ila usafi ndo mpango,

3. Basi Ina tracking device na camera inakuwa monitored na kila station, hakuna dereva atataka kupoteza kazi Kwa ujinga wa kuokota abiria njiani na overspeed.

NB: Madereva wengi Ni NGUMBARU wenzangu na hawana exposure
 
Back
Top Bottom