Planner
JF-Expert Member
- Apr 5, 2011
- 348
- 148
Tunachohitaji watanzania kitakachotusaidia ni elmu ya uraia na elimu ya kujitambua...na hili ndilo wanalofanya CDM kwa sasa (ila kama kuna mdau ana objection nalo anakaribishwa kuchangia).Nadhani si siri kua ndani ya CCM na serikali yake kiongozi anayeonekana kuwa mchapakazi na mpinga ufisadi ataandamwa na vigogo wa ufisadi..nani asiyejua kua Mh.Magufuli alikua anabadilishwa wizara mara kwa mara "ili kumkata maini asioshe"!anayebisha hilo anhitaji maombezi tu.kwa msingi huo huo CDM wanachofanya kinaonekana,wangapi walikua wanajua fedha zetu zinavyoibiwa,kama Dr.Slaa angekua mzushi unadhani serikali ya JK ingemuacha atambe tu?pia suala la kua data za ufisadi kudaiwa zinatolewa na watu walioko kwenye mfumo ndio wawape CDM halina nafasi sana cha msingi ni je taarifa hizi ni za kweli au uongo,mfumo wa kupata taarifa hua ni wa ki-intelijensia si lazima kila mtu atajiwe techniques.Hivi enzi zile za mzee Lyatonga akigombea ubunge TMK ma Abdul Cisco mtiro wa CCM,Mrema alitoa tuhuma kwa Rais mstaafu Mkapa za kula milioni 900 pamoja na waziri wa fedha(Mh mbilinyi by that time),CCM walisema mengi lakini finally waziri na naibu wake waliondokakujiuzulu).ninachotaka kusisitiza ni kua kutaka kujisafisha kupitia mgongo wa Dr. Slaa ni uvivu wa kufikiri.kamwe uchafu hauondolewi kwa uchafu mwingine wa kudandia watu.nadhani Nape ameanza kucheza madogoli ambayo hajui hatma yake,pia kama watanzania hamjashtukia sasa ni mfumo wa kurithishana serikali na chama pia,,tafutateni takwimu mtaona kila palipo na viongozi wa serikali/chama watano watatu wamewachomeka watoto wao kwenye mfumo hata isivyo halali(sina tatizo na wale wanaopata nafasi ki halali) CCM tudanganyeni lakini kuna siku itakua historia kenu kuongoza.Tuamke watanzania.mwenzako akimwaga ugali we kula mboga!!!!