Unafiki huu wa wanaharakati (CHADEMA), kiboko

Nape Nnauye

MP Mtama
Dec 26, 2012
99
408
Naandika hili kwa masikitiko makubwa maana watani zangu CHADEMA siku zao zinahesabika kwa kasi inayonitisha sana. Mimi ni muumini wa uimara wa CCM kutegemea sana uimara na umakini wa upinzani nchini! Kwahiyo anguko la upinzani nchini si jambo zuri kwa CCM, nchi na demokrasia yetu, CHADEMA kikiwa moja ya taasisi muhimu kwenye ukiaji wa demokrasia hiyo.

Kilichonistua ni degree ya unafiki inayojidhihirisha kila kukicha ya viongozi wengi wa CHADEMA. Kupinga ufisadi kwa mdomo mpana halafu unaendesha Chama kwa pesa hizohizo huu ni unafiki wa ajabu! Tunajifunza nini kwa kiongozi wa Chama anayesema pesa ni pesa tu inategemea unaitumiaje!!? Ha! Kwahiyo unaweza kuuza nchi ilimradi unapewa pesa.

Niliwahi kutoa mfano mkubwa wa unafiki wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa (sikuhizi nasikia vijana wanamwita Mzee wa Gongo) akihubiri watu waichukie CCM.

Na wakati mwingine alihamasisha wachane na hata kuchoma kadi za CCM wakati yeye kabanisha yake tena kwa matunzo makubwa! Huu ni unafiki mkubwa! Vijana tunajifunza nini kwa unafiki huu.

Lakini niliwahi kusema Chadema kinaendeshwa kwa pesa kutoka nje, wakabwata wakinipa siku saba kukanusha, kabla mate hayajakauka, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Ndg. Zitto anakiri hadharani kuwa gazeti leo, ambacho ni chombo kikuu cha propaganda limeanzishwa kwa pesa kutoka nje!! Huwezi kujenga Chama kwa msingi wa uongo kuliko wa shetani halafu ukadhani chama kitadumu.

Utaratibu wa vyama kufukuza wanasiasa vijana kwenye vyama hivyo ni wa hovyo na unapaswa kukemewa! Vijana wasipokosea mnataka wakafanyie wapi makosa?? Vyama lazima vitumike kulea na kuwafumdisha vijana badala ya kuwafukuza. Toka watani zangu waanze kufukuza wamekuwa wakifukuza vijana tu hasa wanaohoji. Kuhoji ndani ya CHADEMA ni mwiko! Mtakumbuka ya Kafulila na vijana wengine wengi tu. Mtauliza we Nape!! Ndio mimi chama changu kilinisikiliza na ndio maana nipo sikufukuzwa! Ukomavu ni pamoja na kuwa tayari kusikiliza maoni tofauti na uliyonayo.

Ushauri wa bure: Watani anzeni upya! Msione aibu fumua anza upya tutawasubiri mkomae msihofu kuachwa sana! Mmekutana na ajali ya kisiasa kutafuta mchawi sio dawa, tafuteni mmejikwaa wapi.
 
Nape, yaani 2014 imeikuta CDM na aibu kubwa sana

Nape, chadema sio chama cha kitaifa believe it or not

chadema akijawahi kuleta njia mbadala zilizosheneni ufikirisho wa ubongo kutatua matatizo mengi sana ya kijamii, ikiwemo sehemu wanazoishi

their first and foremost priority is making Money, moneeeeeeey, pesa baba , pesa


huku cdm wengine wanatoa povu na kutaka kuua kwa hasira za kumchukia zitto

hakuna kitu kibaya kama kugundua unafanywa msukule
 
Tangu umekuwa kiongozi wa CCM hujawahi koma kusema siku za CDM zinahesabika... hadi leo CDM hao hao wamekukalia kooni na wewe na viongozi wenzio mmeweka historia ya kupoteza viti vingi zaidi kwenye chaguzi ndogo...

Unashindwa kuhesabu kilo unazoongeza unahesabu siku za CDM kufa!!!
 
Naandika hili kwa masikitiko makubwa maana watani zangu CHADEMA siku zao zinahesabika kwa kasi inayonitisha sana. Mimi ni muumini wa uimara wa CCM kutegemea sana uimara na umakini wa upinzani nchini! Kwahiyo anguko la upinzani nchini si jambo zuri kwa CCM, nchi na demokrasia yetu, CHADEMA kikiwa moja ya taasisi muhimu kwenye ukiaji wa demokrasia hiyo!

Usitudanganye. Huwezi kupenda upinzani wakati huo huo unapenda uimara wa Chama chako cha CCM. Kama unataka kutuambia kuwa unaamini vile vile kuwa unapenda CCM kitoke madarakani kwa sababu umakini wa upinzani lazima mwisho wake uwe kushika dola.
 
Bwana Nape kwa failure unayoendelea kuonesha kisiasa ndani ya chama chenu once likiingia tinga tinga Lowassa madarakani jiandae kuomba hifadhi ya kisiasa china kwa yule afisa balozi mliyemvika fulana zenu! Umekuwa mtu wa kuattack wakubwa zako bila hata apparent reason,ya ndani kwako yamekushinda kutwa kuwa msemaji wa nyumba ya mwenzio...

Naweza kuthibitisha kwa hoja kuwa una mapenzi mema na Chadema na huenda ndio maana unaijua kuliko hata wanachama wake...

Still loading.....
 
Tangu umekuwa kiongozi wa CCM hujawahi koma kusema siku za CDM zinahesabika... hadi leo CDM hao hao wamekukalia kooni na wewe na viongozi wenzip mmeweka historia ya kupoteza viti vingi zaidi kwenye chaguzi ndogo...
Unashindwa kuhesabu kilo unazoongeza unahesabu siku za CDM kufa!!!
Mkuu, kwani wewe hulioni anguko la CHADEMA? Au mpaka kwenye ballot box ndo utathibitisha kuwa hakika hiki chama kimesambaratika. Huwezi kumfukuza ZITTO bado kajifariji kuwa chama kiko imara
 
Bwana Nape kwa failure unayoendelea kuonesha kisiasa ndani ya chama chenu once likiingia tinga tinga Lowassa madarakani jiandae kuomba hifadhi ya kisiasa china kwa yule afisa balozi mliyemvika fulana zenu! Umekuwa mtu wa kuattack wakubwa zako bila hata apparent reason,ya ndani kwako yamekushinda kutwa kuwa msemaji wa nyumba ya mwenzio...
kwani Lowasa ni mwanachama wa chama gani? Huku ni kukata tamaa mkuu. Maana umechunguliaaaa ukagundua kuwa ndani ya chama chako hakuna mtu wa kukivusha kutwaa nchi badala yake unadandia wanasiasa wa ccm
 
Ni sehemu ngap CCM inatafta madiwani wa kugombea inapata kwa mbinde kisa CHADEMA? We unasema inakufa amka ndo mwisho wa CCM huu? Mtakaa mkisema mwisho wa CHADEMA, kwani 2013 haijafka si ndo mlisema kinakufa bado kadi tunagawa tu; mtaelewa hata kama hamtaki.
 
Ama kweli Umesahau Kauli ya Mangula juu ya lowasa je akiendelea kutoa misaada yake hyo ya Rushwa mtamfukuza? Na je hilo ndio anguko la Ccm?
Kujivua gamba kwa viongozi wa cdm haitakuwa mwisho wa uimara wa cdm msidanganyane.
Ccm ndo nina hakika haiwezi kujivua gamba maana limeshikamana na ngozi.
Amini usiamini cdm bado itaendelea mbele.
 
Nsehem ngap ccm inatafta madiwan wakugombea inapata kwa mbinde kisa chadema we unasema inakufa amka ndo mwisho wa ccm huu mtaka mkisema mwisho wa chadema kwani 2013 haijafka sindo mlisema kinakufa bado kadi 2nagawa 2 mtaelewa hata kama hamtaki people
Mkuu, CCM ni chama makini sana. Kina utaratibu wa kuwapata wagombea wasio na shaka. Si kuokota okota tu kama mfanyavyo chadema
 
Naunga mkono hoja ,Mbowe ni mpiga madili anachukua fedha kutoka kwenu,kwa akina Nimrod,Rostam na anaingia mikataba na akina kinana na Sumaye ya madeni then zigo wanapachikwa chadema kama chama
Mbaya zaidi amekiri kwa mdomo wake eti uchukue fedha kwa mpinzani wako kipindi cha uchaguzi then uhoji zinalengo gani?
 
Kwa hali ilivyo sasa CDM twapaswa kujadili namna ya kupata ufumbuzi na si kuwabeza watazamaji ambao wanaehangilia mpira unaochezwa na CDM Kikubwa labda ni kusitisha mechi.
 
Kwa upande mmoja nakubaliana na Nape hasa kuhusiana na suala la kufukuzana katika Chama na katika hili suala la baadhi ya watu kutaka kuhodhi fikra ndani ya Chama hii kwakweli si nzuri kwa afya na ustawi wa Chama.

Ila kwa upande mwingine sikubaliani ikiwa anaamini kuwa Chadema itasambaratika hii si kweli hata kidogo. Kwa mtu yeyote aliyesoma political science ataelewa nini ni significance/implications wa mnyukano unaoendelea ndani ya Chama. Kuna njia nyingi sana za kuleta mabadiliko katika taasisi yoyote ile Duniani na migogoro ni moja wapo ya hizo njia.

Ninaamini ndani ya Chama kuna watu walio-reasonable na intelligent enough so wata-handle hii issue kwa uweledi na tahadhari kubwa ambapo siku ya siku Chadema itaibuka kutoka katika huu mgogoro ikiwa imara zaidi kuliko wakati wote.

Mkakati wetu wa kuitoa CCM madarakani 2015 bado upo pale pale ilikuwa ni lazima kwanza Chama kianze kujichekecha chenyewe kwanza pumba ziondoke na chenga/mchele ubakie na huu mgogoro unaoendelea ndio njia sahihi ya kuendesha mchujo huo.
 
Back
Top Bottom