Unafahamu vipi kuhusu miaka 6000 ya ukomo wa Dunia?

Jeho

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
5,053
5,504
Wakuu, heshima kwenu. Naleta kwenu mjadala huu unaohusu mpango wa Mungu kwa ukomo wa sayari dunia ambao kuna watu wamekuwa wakisema kuwa, Mungu kaipangia Dunia miaka 6000. Wanaodai hivyo wamekuwa na hoja wanazozitoa kuhalalisha madai yao. Nitaleta kwenu baadhi ya hoja hizo, na kwa kadri ya kila mtu anavyofahamu, ataongezea ili hatimaye nami pamoja na wengine tupate kitu.
Hoja namba 1
Kwamba, Mungu aliumba mbingu, nchi na bahari kwa muda wa siku sita na ya saba akastarehe.
Hoja namba 2
Yanatumika mafungu kadhaa ya biblia ambayo japo yana maana halisi (literal meaning), lakini yanatumika pia kama yalikuwa yanalenga kutoa ujumbe wa kinabii (prophetic meaning). Baadhi ya mafungu hayo ni haya yafuatayo.
Kutoka 21:2 Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.
Kutoka 23:10-11
Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake; lakini mwaka wa saba utaiacha nchi itulie na kupumzika..

Joshua 2:2-5 ...fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba
za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba
mtauzunguka mji mara saba.

Hata ukisoma habari za naamani, safari ya saba kujichovya katika maji, ndipo akatakasika ukoma wake.

Hoja hizo zote zinatumiwa kufikio hitimisho kuwa, Mungu hukamilisha mambo yake katika mfuatano wa vipindi 6, inaweza kuwa siku sita, majuma au miaka. Na kwenye ufunuo inaeleza watakaokwenda mbinguni, ama pasipo kuonja mauti au kwa kufufuliwa, watatawala na kristo miaka 1000 (Ufunuo 20:1-5). hivyo wanahitimisha kwa kusema kuwa. Muda ambao Mungu kaipa dunia (baada ya dhambi) ni miaka 6000, na miaka 1000 ni ya kupumzika mbinguni. Jumla miaka 7000, ndipo mbingu mpya na nchi mpya zinatengenezwa. Umeshawahi kusikia nadharia jii? kama ndiyo, hebu ongezea kuhusu ulivyosikia wewe.
cc: Ntuzu mshana jr TODAYS Eiyer na wadau wote, karibuni.
 
Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yaonekayo na ht yasiyoonekana,pia mambo haya hayana budi kutokea japo muda wake haujafika,MUNGU bado anatoa nafasi ya upendeleo ili tutubu na kurejea kwake
 
Tutaamia sayari nyengine kwani ipo dunia peke yake movement for change...!!
 
Wanasayansi wanasema ulimwengu una miaka bilion 13 toka utokee lakini lakini watu wa dini wanasema ulimwengu una miaka 6000 toka umeumbwa.
Kwahiyo nani tumuamini.
Lakini hapo wakumuani ziadi ni wanasayansi kwasababu hii dunia inaendeshwa kisayansi.

Na huyo wanae sema atauleta mwisho wa dunia ataanzia wapi hii dunia ni kubwa sana.
 
Sawa dunia ina miaka mingi, lakini tukianzia kuumbwa kwa Adamu ndiyo mwanzo wa kizazi cha mwanadamu
Kwa hiyo mwisho wa dunia itakuwa mwisho wa dunia na vilivyomo ndani au mwisho wa iko kizazi cha mwanadamu halafu dunia itaendelea kuwepo?
 
Wanasayansi wanasema ulimwengu una miaka bilion 13 toka utokee lakini lakini watu wa dini wanasema ulimwengu una miaka 6000 toka umeumbwa.
Kwahiyo nani tumuamini.
Lakini hapo wakumuani ziadi ni wanasayansi kwasababu hii dunia inaendeshwa kisayansi.

Na huyo wanae sema atauleta mwisho wa dunia ataanzia wapi hii dunia ni kubwa sana.
Correction kidogo universe ndio ina miaka bilion 13+ lakin dunia ina miaka bilion 4
 
Back
Top Bottom