mnepha
JF-Expert Member
- Apr 5, 2016
- 300
- 280
Wakuu, heshima kwenu. Naleta kwenu mjadala huu unaohusu mpango wa Mungu kwa ukomo wa sayari dunia ambao kuna watu wamekuwa wakisema kuwa, Mungu kaipangia Dunia miaka 6000. Wanaodai hivyo wamekuwa na hoja wanazozitoa kuhalalisha madai yao. Nitaleta kwenu baadhi ya hoja hizo, na kwa kadri ya kila mtu anavyofahamu, ataongezea ili hatimaye nami pamoja na wengine tupate kitu.
Hoja namba 1
Kwamba, Mungu aliumba mbingu, nchi na bahari kwa muda wa siku sita na ya saba akastarehe.
Hoja namba 2
Yanatumika mafungu kadhaa ya biblia ambayo japo yana maana halisi (literal meaning), lakini yanatumika pia kama yalikuwa yanalenga kutoa ujumbe wa kinabii (prophetic meaning). Baadhi ya mafungu hayo ni haya yafuatayo.
Kutoka 21:2 Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.
Kutoka 23:10-11
Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake; lakini mwaka wa saba utaiacha nchi itulie na kupumzika..
Joshua 2:2-5 ...fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba
za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba
mtauzunguka mji mara saba.
Hata ukisoma habari za naamani, safari ya saba kujichovya katika maji, ndipo akatakasika ukoma wake.
Hoja hizo zote zinatumiwa kufikio hitimisho kuwa, Mungu hukamilisha mambo yake katika mfuatano wa vipindi 6, inaweza kuwa siku sita, majuma au miaka. Na kwenye ufunuo inaeleza watakaokwenda mbinguni, ama pasipo kuonja mauti au kwa kufufuliwa, watatawala na kristo miaka 1000 (Ufunuo 20:1-5). hivyo wanahitimisha kwa kusema kuwa. Muda ambao Mungu kaipa dunia (baada ya dhambi) ni miaka 6000, na miaka 1000 ni ya kupumzika mbinguni. Jumla miaka 7000, ndipo mbingu mpya na nchi mpya zinatengenezwa. Umeshawahi kusikia nadharia jii? kama ndiyo, hebu ongezea kuhusu ulivyosikia wewe.
cc: Ntuzu mshana jr TODAYS Eiyer na wadau wote, karibuni.
There is no recordation for aboriginal beings. Ever since consciousness existed we were HERE already.
Kitu kilichoongelewa kuhusu miaka 6000 ni existence of amalgamated creactures ambao ni WAZUNGU NA MAKABILA YAO. DUNIA YAO ITAISHIA MIAKA HIO 6000 TU. UWEPO WA TAWALA ZAO ZA KIUCHUMI, KISIASA NA KIMWILI (AMBAO NI UTAWALA WA KISHETANI ) UTAONDOKA MIKONONI MWAO. NA KUHAMIA KWA ABORIGINAL TENA (KUUMBWA KWA DUNIA MPYA NA MBINGU MPYA. AMBAO UTAKUWA UTAWALA WA UFALME WA MBINGU AMBAKO DUNIA ITAONGOZWA KIROHO NA SI KIDINI).
SIO DUNIA KAMA SAYARI KUWA ITAKUFA NA MAISHA KUFA HAIKUWA NA MAANA HIO.
NA MIAKA YAO IMEBAKI MICHACHE SANA NDIO MAANA WANAHANGAIKA MNO MAANA WENYEWE WANAFAHAMU.
WALE WANAOSOMA KITABU CHA BIBLIA KUNA UTABIRI WA YESU ALISEMA KUWA: WHEN YOU SEE A FIGUE TREE IS SPROUTING, BE AWARE THAT THE KINGDOM OF HEAVEN IS NEAR ( UKIONA MTI ULIOKAUKA UNAANZA KUCHIPUA UJUE NDIO ISHARA MOJAWAPO YA KUWA UFALME WA MBINGU UNAKARIBIA).
MTI ULIOKAUKA NI KIZAZI CHA WATU WEUSI WALIPOONDOSHWA NA KUNYANYASWA NA UTAWALA MPYA DHALIMU NA WAHOVYO WA WAZUNGU. WAKAFUTWA KABISA KATIKA USO WA MAARIFA DUNIANI. KWA VILE SIKU HIZI WATU WEUSI DUNIANI WANAANZA KUHOJI MAMLAKA HUSIKA JUU YA UOVU WALIOTENDEWA WAKATI WAO NDIO WALIOLETA USTAARABU WOTE DUNIANI NA KUTAKA KUANZA UPYA KUVESHA DUNIA NGUO TENA NI SAWA NA MTI UNAOCHIPUA.
MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA NA ALIE NA MASIKIO NA ASIKIE.