Una mipango gani kwa miaka 10-20 ijayo?

Habari wana-JF. Kama tunavyojua mpango kazi kwenye maisha ndiyo dira itakayokuongoza katika maisha yako na kufikia malengo yako.

Kwangu nahisi safari ndiyo kwanza inaanza na maamuzi yangu ya leo yatakuwa na mchango mkubwa kwa maisha ya baadaye.

Nikiwa kwenye early 20s (23) tayari nipo kwenye first phase ya mpango kazi wangu. Mimi shule nilikuwa siipendi kabisa kwa miaka 11 yote niliyosoma elimu ya msingi mpaka sekondari ila mtazamo wangu ulibadilika baada ya kujiunga chuo nikiwa na 18 na kuanza kusoma kile ninachokipenda.

Toka nikiwa mdogo nilikuwa ni mtu ninayependa kutumia teknolojia ya computer ni kwasababu ilikuwepo nyumbani na mzee wangu alinifundisha nilipokuwa mdogo sana. Nilipenda kucheza games na kufanya simple tasks mbalimbali. Mimi ni mmoja wa Gen Z niliyetumia Windows XP miaka hiyo.

So baada ya kumaliza sekondari nilijua nataka kusomea nini basi moja kwa moja nikainza safari yangu kwenye field ya Information Technology, miaka yote niliifurahia mpaka nilipohitimu kwa ngazi ya Diploma.

Sasa ukiachana na hiyo historia (intro) fupi mpango kazi wangu umegawanyika katika phase 2.

1st phase: 10 years
2nd phase: 10 years

So huu ni mpango kazi wa miaka 20 ijayo. Kwenye first phase ndiyo msingi unapoanzia, kitakachofanyika hapa ndiyo kitaleta picha ya kitakachotokea baada ya miaka 20.

1. Natumaini nitakuwa hai kwa miaka 20 ijayo.

2. Nataka niweze kufanya vitu ninavyovifanya kwenye early 20s kwa uwezo uleule au kwa ufanisi zaidi ya sasa. Hapa ni afya kuwa bora zaidi.

3. Nataka kuamua namna maisha yangu ya baadaye yatakuwa, na siyo magonjwa kuamua muda wangu wa kuishi duniani. Hapa ni kwa kuwa makini zaidi na afya yangu ya akili mpaka mwili.

4. Nataka kuishi kwa miaka 20 ijayo.

1st phase:

1. Career Building. Hapa nataka kujenga career yangu kwenye Web Development & Graphic Design (Freelancer) ndiyo kitu ninachifanya kwa sasa ila ninapotaka kufika ni safari ndefu ambayo siwezi kufika kwa usiku mmoja ndiyo maana ujenzi wa career yangu upo kwenye first phase. Malengo ni kuwa bora kwenye hizo field: bora kweli.

2. Education. Kwenye first phase ya mpango kazi wangu nataka kujiendeleza kielimu mpaka level ya Bachelor Degree. Hii naitaka ikiwa ni mwanzo wa safari nyingine kwenye second phase ya mpango kazi wangu.

3. Health. Afya ndiyo kila kitu, afya ndiyo uzima. Bila afya imara huu mpango kazi si kitu. Hivyo jambo la muhimu zaidi ni kulinda na kuimarisha afya yangu ya akili na mwili kwa miaka 20 ijayo. Hapa ni kwa kupata mlo kamili, mazoezi, kuwa na bima ya afya, kuupa mwili na akili mapumziko panapohitajika, kuyapa vipaumbele mambo yatakayonijenga na kunipa furaha zaidi.

4. Family & relationships. Nataka kuwa karibu zaidi na familia yangu: hao ndiyo watu wangu niliokuwa nao toka siku ya kwanza naletwa Duniani na ndiyo watakaokuwa na mimi katika safari ya maisha yangu. Mahusiano ni jambo la muhimu, hii ni safari nyingine kuelekea kujenga familia bora. Lakini sitaki mahusiano yaharibu mpango kazi wangu kabisa, hivyo ni kazi nyingine ya kutafuta mtu sahihi wa kuwa naye.

5. Personal development. Hapa nataka kuwa bora zaidi kwenye Technology na ndiyo njia ya kuijenga career yangu. Nataka kuachana na addiction zote zinazozuia mpango kazi wangu kufanyika kwa 100%.

6. Finance. Hili jambo la muhimu, mwanzo na mwisho wa mpango kazi huu. Nataka kujenga career itakayonipa fursa za kufanya Duniani popote na kunipa kipato kinachoendena na thamani ya kazi nitakayoifanya. Nataka kuweza zaidi kwenye Cryptocurrency & Stocks: elimu hapa ni muhimu zaidi. Nataka kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji wa kisasa, hii ndiyo back-up plan yangu japokuwa sitaki kuwa na back-up ni njia ya kwanza kujiona nimefeli kwenye mpango kazi wangu mkuu. Nataka kutafuta fursa nyingi zaidi za uwekezaji, sitaki kujipa limit, kujifunza zaidi ndiyo kufanikiwa zaidi.

7. Adventure. Malengo yangu kwa miaka 10 ijayo ni kusafiri zaidi, hasa nje ya nchi: kujifunza zaidi. Kupanda Mlima Kilimanjaro ni jambo lingine nataka kulufanya katika miaka 10, nilishatembelea Mbuga ya Wanyama ya Serengeti, hivyo kwa utalii Kilimanjaro ni my next target.

#: Kufurahia ujana ni jambo la muhimu zaidi kwasababu unakuja mara moja tu kwenye maisha. Kazi ni lazima ifanyike kwelikweli ila kufurahia maisha kila siku ni kushukuru kwa baraka hii tuliyonayo.

2nd Phase:

1. Education. Lengo kubwa kwenye second phase ya mpango kazi wangu itakuwa ni kujiendeleza kielimu kwa ngazi ya Masters. Hapa nataka kufuata nyayo za mzee wangu aliyehitimu masomo yake ya Masters nchini Netherlands. Nje ya nchi ndiyo lengo langu kuu kupata elimu huko, naamini fursa nyingi zaidi zitapatikana.

2. Family. Hapa sasa naamini ndiyo utakuwa wakati mzuri wa mimi kujenga familia bora baada ya msingi kutengenezwa kwenye first phase.

3. Work career. Hapa sasa ndiyo natarajia kazi kubwa zaidi itafanyika: kufanya kazi, uwekezaji kwa ajili ya kizazi changu.

4. Retirement. Baada ya miaka 20 ijayo natarajia kustaafu nikiwa na miaka 45-50. Ni muda ambao naamini ukifika napaswa kufurahia zaidi maisha na familia yangu bila kuwaza kufanya kazi tena. Lakini hili halitawezekana kama kazi bora na ya uhakika haitafanyika kwenye hii miaka 20 ya mpango kazi wangu.

5. Off-grid. Hapa naaminisha kuishi nje ya mji kabisa na familia yangu, mahali ambako nitafurahia maisha yangu baada ya kuikamilisha kazi kubwa iliyonileta Duniani. Kuwa na farm house ndiyo ndoto yangu kubwa. Kwa Tanzania tayari lipo eneo linalonivutia zaidi kuishi kwenye miaka 20 ijayo.

Yapo mengi ila hapa ni kwa kifupi tu. Ningependa kujua mipango yako kwa miaka 5, 10, 15 au 20 ijayo maana hapa tayari tunatofautiana umri, elimu, vipato.

Nataka kuishi kwa miaka 20 ijayo.
It seems like you have life sorted, Kila la kheri.

Karibu sana kwenye mapambano.
 
We b

Wege kweli nikuambie ili mniroge? Muanze kunionea kijicho na hasidi watu wa jamii forum?
 
Ni vizuri kuwa na mipango ila mpango wako hautakupatia financial freedom.
Bado kuna mengi najifunza. Financial freedom najua ni safari nyingine ambayo inahitaji umakini zaidi.

Nadhani financial freedom inaweza kuwa determined zaidi na vipaumbele vya mtu. Jinsi safari ya maisha inavyoendelea ni nafasi nyingine ya kujifunza zaidi.

Asante kwa maoni yako.
 
Asante sana mkuu. Kila safari inaanzia kwenye kilometre 0. Najua kabisa siyo kazi rahisi, kuna mstari mwembamba unaotenganisha kufaulu na kufeli.

Tunaishi tukiwa na matumauni ya kuamka kesho ila hata pumzi ya sekunde 1 ijayo hatuna uhakika nayo.
upo sahihi kikubwa uwe na malengo na mpango kazi wa kuyafanya yatimie.
 
Nimesikia sauti tu ya mtu aliye nyikani ikinambia..."amkaaa wewe.You nearly "wetted" the mattress.Those are pipe-dreams"...!🤔
😂😂😂

Hizi ni ndoto za kawaida kabisa kwasababu hata vizazi vilivyopita wengi wamejenga career zao kupitia elimu, biashara na wengi wanastaafu kwenye 60s. Kipi cha ajabu nilichoandika?

Kuogopa kufeli ni hatari zaidi kuliko kufeli kwenyewe.
 
Labda kama uko nje ya Tanzania, ila kama upo hapa bongo Land.

Safari bado mbichiiii....
Ndiyo maana nahitaji miaka 20 na inaweza kuchukua hata miaka 30 maana unachokipanga siyo kuwa kitanyooka tu.

Yes! Tanzania ni moja ya disadvantage kwenye mpango wangu. Career yangu naijenga zaidi kwenye freelance na kuna vitu kama serikali inafanya viwe vigumu.
 
Nina mipango ya kufunguwa kilinge cha uganga wa kienyeji.
Nimegunduwa ukitaka kupata pesa na Kula kuku , mbuzi na mbususu za bure bure uwe mganga wa kienyeji..

Hii ni mipango yangu ya miaka 10 ijayo..
 
Kabla sijachangia naomba kufahamu
1. Unafanya kazi masaa mangapi kwa siku /wiki kulekea hizo ndoto zako.
2. Gharama ya mlo wako mmoja hua ni kiasi gani lets say lunch au breakfast.

Ndani ya mada . Sina mpango wowote ule hua naishi kwa kunata na beat, yaan freestyle life.
 
nikiwa sec.school niliapa kutoenda migodini kuchimba, no matter what will happen..hii ni baada ya kumuona jirani yetu kavunjika hovyo hovyo mguu wake,..na ukizingatia tena kwetu mzee na mama wote ni wasomi na wafanyakazi wa SERIKALI...miaka sita baadae nikajikuta niko migodini nikigonga nyundo balaaa😂😂, ..wachimbaji wenzangu walikuwa hawajui kuwa hata kitabu nimepiga, maana nilibadilika na kuamua tu sasa liwalo na liwe......so nakutakia safari njema bwana mdogo, ila fahamu changamoto za maisha halisi ni kubwa mno kuliko hizo za kwenye karatasi....
 
Attachments

  • FB_IMG_1686296807033.jpg
    FB_IMG_1686296807033.jpg
    17.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom