UN yavunja ukimya Tanzania

tethering

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
331
139
Tafiti uchaguzi wa Urais Tanzania hazitoshi kumjua mshindi wa Urais Tanzania, hayo yamesemwa na mwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa Tanzania (UN)
Source ni Mwananchi ipandishe

UN: Tafiti za uchaguzi hazijaamua mshindi

By Julius Mathias, Mwananchi

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku 17 kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika nchini huku kampeni zikiendelea kupamba moto, Umoja wa Mataifa (UN) umesema tafiti zilizofanywa juu ya mbio za urais hazitoshi kutoa picha halisi ya atakayeibuka mshindi.

Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Balozi Alvaro Rodriguez alipotembelea ofisi za gazeti hili na kuzungumza na wahariri pamoja na waandishi.

Akiwa sambamba na Ofisa Mawasiliano wa UN, Hoyce Temu, mratibu huyo alisema kwa hali ya kisiasa ilivyo hivi sasa, kwa mtazamo wake anaona kulikuwa na mwanya wa kutosha kwa taasisi nyingi zaidi kujitokeza na kutoa taswira ya matokeo ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.

“Ukweli kwamba zaidi ya watu 23.7 milioni wameandikishwa kati ya 24 milioni waliokadiriwa na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) inadhirisha kulikuwa na maandalizi ya kutosha na elimu ya kutosha ilifika kwa wananchi. Lakini tafiti zilizotangazwa mpaka sasa siyo za kutosha kuweza kutoa picha ya nani anaweza kuibuka mshindi baada ya kura kupigwa,” alisema.

Pamoja na hali ya kisiasa iliyopo nchini, Rodriguez alisema upigaji kura ni hatua moja ya maendeleo ya taifa, lakini utawala bora ni kitu muhimu kitakachoiunganisha Tanzania na mataifa mengine duniani.

Aliwataka wadau wote kuzingatia suala hilo na kuliangalia kwa jicho la ziada.

Mratibu huyo alisema kwamba mara zote uchaguzi unahusisha vyama vingi vyenye itikadi tofauti za kiuchumi, akimaanisha ujamaa na ubepari na kutoa angalizo kwa wananchi kutambua wanachohitaji kwa miaka mitano ijayo.

“Yametokea mabadiliko katika siasa za ndani. Kinachoendelea hivi sasa kisingeweza kutabiriwa miezi mitano iliyopita. Kinachoonekana ni kama siasa za Tanzania zinategemea sana ushawishi wa mtu mmoja mmoja,” alisema. Rodriguez.
 
Tafiti uchaguzi wa Urais Tanzania hazitoshi kumjua mshindi wa Urais Tanzania, hayo yamesemwa na mwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa Tanzania (UN)

Sasa si walau ueleze alisemea wapi na source ni ipi ili tusome wenyewe na alitoa mfano upi ambao matokeo ya utafiti na reality ni tofauti? Mtu wa UN hawezi akadokeza kidogo hivi kama mtu anayemwambia mpenzi wake wakadinyane.
 
sasa si walau ueleze alisemea wapi na source ni ipi ili tusome wenyewe na alitoa mfano upi ambao matokeo ya utafiti na reality ni tofauti? Mtu wa un hawezi akadokeza kidogo hivi kama mtu anayemwambia mpenzi wake wakadinyane.

soma magazeti ya leo baadhi yameonyesha hiyo habari
 
Lowassa ndo Rais, kama hupendi we nenda kajinyonge, au ufanye chochote cha kukumaliza.
 
Kwahiyo hata yule babu mwenye mandevu ndevu anaitwa Hashimu Lungwe anaweza kuwa rais>>
Huu utakuwa utani kwa wapiga kura.
 
Tafiti uchaguzi wa Urais Tanzania hazitoshi kumjua mshindi wa Urais Tanzania, hayo yamesemwa na mwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa Tanzania (UN)

Acha uongo UN ya congo au?maana UN TANZANIA haijatoa tamko hilo!
 
Mimi nasubiri tu najua lowassa ndio rais hata kama Un wasingetoa angalizo hiyo jana mbona taarifa ya habari jana ilionesha azam TV
 
Back
Top Bottom