Umuhimu wa Mfumo Dume (Ubaba)

nakubali pesa ndiyo kila kitu ila mbona hata wenye pesa ndoa zao ziko matatani?

mada haisemi kuwa pesa ndio kila kitu - inasema pesa ndio msingi mkuu wa kila kitu katika mapenzi/mahusiano

1. chakula kinanunuliwa kwa pesa (labda muwe mnafunga tu kila siku au kuomba chakula kwa majirani)
2. kitanda kinanunuliwa kwa pesa (labda mlale majanini vichakani ila siku hizi hata ardhi zina hatimiliki)
3. hata condom zinanunuliwa kwa pesa (labda muwe hamzitumii au muwe mnapewa bure zile za misaada)

na orodha ni ndefu inaendelea, ukiona huelewi mada rudi kwenye mfano wa gari - pesa ndio injini, ni lazima iwepo.
 
Msingi wako wa mapenzi/mahusiano ni mawe, simenti na udongo?

Kwa hiyo mtu akiija tani 2 za sement masukuma anaumia???

Wee ongeza tu vyenye unaona ndo vinafaa msingi wako...

Wapi tena nimekuchekesha aisee? Hapa kwenye msing?
 
Yafuatayo ni maoni jadidi ya Mwanafalsafa mahiri:

Naam Kaka, kwa kuwa ninandika jambo fulani kwa kirefu ili kuwakilisha humu JF siku sijazo, sitaingia humu kwenye mijadala ila ninavutiwa mara jingine na mijadala na mawaidha ya hapa na pale humu.

Uzi wako wenye jina sambamba na kichwa cha habari kwa ujumbe huu unahusu kidogo nishiriki na wewe na wengine wachache kuhusu Pesa na Mfumo baba...

Kwa kifupi ni hivi--uchumi ni kujikimu na kujitosheleza kwa kaya ili kukidhi mahitaji ya kimsingi yanayobainishwa hasa kuwa ni chakula, malazi na mavazi. Kikubwa ninapenda hili likuingie akilini kwa namna yake ya asili kabla halijaingiliana na mengine...

Kuhusu pesa kama kigezo cha mabadilishano--ninapenda kimsingi ikuingie akilini kuwa kazi na huduma huwa na asili ya kunasibu thamani ya chochote chenye kuweza kujakuweza kutumika kama kigezo/kizio cha mabadilishano katika jamii; hili tuliweke hivi kusudi tupate kudadavulia picha mbalimbali za mikunjuko ya kiustawi na ustaarabu kwa kadri hata historia inaweza kutupatia mifano ya ushahidi dhahiri.

Ingalikuwa vema sana kila mtu akajua vizuri pesa inakujaje hasa kuijipatia uthamani wake hata kutumika katika maisha ya watu--kwa kuwa nimeona kidogo mabadilishano yasiyo fasaha na kule kulenga mzizi wa hoja unayotaka kuendeshea maudhui ya uzi wako; mfano posti #15 ya NN--kimsingi ana hoja lakini wewe unashindwa kiufundi kuikabili kama unagwaya kwenye posti #17. Ukirudia tena kutojenga ya dhana kwa ufasaha wa hoja kwenye posti #22... Mtani wako wa jadi anakusakama vizuri, naona umshukuru huwa anakupa sehemu nzuri sana wewe kuweza kujenga hoja ama shauri japo kidogo huwa wote huwa mnapotoka mikondo na kuishia kwenye kucharurana vimaneno... NN anawaseti vizuri lakini wengi mnaonekana mpo juu juu--tazama posti #38, #39 na #44. Aidha, tazama na wewe unavyokosa kujitetea kwa umahiri kwa majibu yako mafupi mafupi katika posti #31, #32, #41, #43...

Basi tuzungumze kiufundi--Katika uchumi na mabadilishano vyote vilivyokuja kujitokeza kuwa ni vitu vya kutumika ili kukadirisha mabadilishano vimetokana na mazao fulani ya ardhi kufungamana na ugumu wa namna fulani kwa mshughuliko wa kufaulisha hayo. Nigawanye makundi mawili; vya kutoka ardhini kama madini, vito na chuma kwa namna zake. Kutoka majini ndiko huja vitu vya toka zamani kabisa kukadirisha biashara kama historia inavyofunua toka sehemu mbalimbali za dunia--Afrika ikiwa ni mojawapo; matumizi ya vitu kama makombe na masimbi yatokanayo viumbe bahari...

Kikubwa kilichonasibu matumizi ya makombe na masimbi kwa mfano ni masuala ya urembo, nakshi na mapambo. Jingine ni imani nyingi zilipata kufungamanishiwa na vitu hivyo kama vile faida ya hivyo kama dawa/kinga/vitu vya kuleta bahati hata kwa mambo kama uzazi... Na hapa nataka uwe na macho ya kuona ni jinsi gani mazao ya Mama Dunia yamenasibu moja kwa moja nasibu ya mikondo ya biashara--kuvutia mafungamano ya kaya, uzazi na mabadilishano. Uchumi ni nasibu ya kike na kheri inayokuja kwa namna ya kike--ndivyo imekuwa awali na basi hata inakuwa katika kuingia kwenye jitihada za uhandisi wa kijamii kwa miongozo, kanuni na misingi yenye kuleta usanisi wa ujasiriamali wa kijamii.

Muda wa wale wenye kukusanya makombe ama masimbi ki msingi ulifanya kizio cha tunu kwa wenye kuwatunza wenye kujishughulisha katika hilo. Ukiondoa shurti na migandamizano, toka zamani jamii nyingi zilikuwa zikijinasibu haki katika huduma na kazi kwa namna nyingi ikiwemo hiyo kutengenezea imani fulani juu ya jambo... Hili daima lilizaa taasisi za kibiashara na kuleta mifumo kwa mienendo na ustawi wa jamii. Mfano uliohai hata leo kwa mfano ni jinsi ambavyo vipusa, meno ya tembo, ngozi na vitu vingine kutoka kwa wanyama pori vinatumika katika magendo ya fedha na biashara na huku vikitafutwa kukomeshwa. Wenye kutaka vitu hivi wako radhi kutumia chochote kinakidhi mabadilishano kwa kuwa katika jamii husika mtu wa mwisho kumiliki hivyo huonekana ni mwenye heshima na utajiri ukiondoa imani kwa udawa wa asili--kama kawaida, siajabu huo ukichunguzwa utakuta kufungamanishiwa kheri ya uzazi ama utajiri zaidi.

Vivyo hivyo imekuwa kwa chuma. Ugumu wa upatikaji wa chuma na mbinu zake kufua hivyo vyuma umenasibu sura ya uchumi kulingana na umuhimu wa chuma yenye kwa matumizi mbalimbali kuanzia utengenezaji wa silaha, ujenzi mpaka nakshi. Na ndivyo hivi matumizi ya chuma yamekuwa na nguvu na hadhi bora kuliko makombe na masimbi--na kwa sasa ndiyo ninaandika mashauri fulani kuhusu kuibuka kwa ulimwengu wa sarafu, biashara, himaya na dola. Hii italeta mwangaza zaidi katika kuelewa vikomo vya ubepari na basi njia yakusuka upya miundo, tawala na mifumo kwa kaya katika karne ya 21 na kuwa ngazi kwa jamii sisi watu wa Afrika kuinuka upya na kujenga himaya ya namna yake.

Kutambua jinsi ambavyo sarafu inawekufangamanishiwa heshima/imani ya jadi/uthamani fulani ni jambo la msingi na kisayansi ambalo ni nadra kuona wengi kukikatishia ndani yake ili kujipatia maarifa. Kwa kuwa hili lingaliweza kutoa majibu na suluhu ya mengi yanayoisibu dunia yetu kwa misingi isiyohojiwa ya Benki Kuu ya Dunia na vyombo pacha vya fedha, Biashara, Thamani za Mabadilishano ya Sarafu na mengineyo mengi yenye kuja kuwa ni matokeo ya hivi kama vile mataifa yenye kuheshima kwa kutajwa yameendelea na hapo hapo kuna yaliyohohehahe mzungu wa reli bila ya matumaini ya kweli katika kujikwamua.

Kurahisisha haya yote katika sura rahisi ya kaya za wake, waume na watoto; ndivyo basi ni kwanini unazungumzia 'upatiaji', 'Ulinzi' na 'Heshima--katika muonekano na makuzi yake sifa'... Pesa ni kilainisho cha kunasibu mipangilio, miundo na uhitaji kwa yaliyo ya msingi na ya kupendelewa kuwezekana kupatikana maramoja kwa mwanakaya. Ila la muhimu ni kujua ni kitu gani kinachoitia hiyo sifa na hadhi? Kwa kuwa bila huu upeo hayo mengine ya katikati mtazungumza bila mwanzo wala mwisho... Kwa kuwa uthamani kwa mipangilio ya kaya, taasisi ikiwemo ya ndoa kwa mfano ni matunda ya mgandamizo wa miundo na mifumo ambayo nayo kwa namna ingine inajenga ushawishi kwa mapendeleo fulani, sifa kwa sura fulani ya mambo, mwenendo wa mishughuliko na pia tabia za wanakaya...

Ambalo basi kwa sasa sijazungumza ni ulalo wa kazi na huduma na athari zake kwa uthamani wa sarafu yoyotena jinsi gani mfume dume ambao ndiyo unapelekea 'ubaba' kushika hatamu... Kwa kuwa ukiweza kutanganisha kazi na huduma, basi nakuambia unayofunguo pia ya kuweza kutangamanisha ubaba na umama. Ila umama ni mungu katika sura halisi ya uhalisia wa maumbo; ndivyo hivi basi pamoja na fujo zote za kiume--mwanamke ni fumbo la mwisho kwa hekima ya mwanaume yeyote...

Ukiwa na hekima unaweza kuishi na mwanamke pasipo hofu kwa mikondo ya fedha--kwa kuwa wingi wale uchache si jibu hasa; ila jinsi unaweza kutia maana bidii ya kujenga paa juu ya kaya yako, watoto wapate kukua na kheri na baraka tele--wewe na mwenzako mkiwa mfalme na malkia kwa miliki yenu...

Haya mzazi, isome namba kimya kimya ;)
 
mwanamke hakuumbwa kumpa mumewe pesa kama hana au hata kusaidia. japo misaada tunawapa. utaona ni sahihi pale ambapo penzi limekolea. penzi likianza kuchujuka utaanza kuona ni mzigo. tofauti na mwanaume kwa vile ndio laana yake aliyopewa na muumba, hawezi kuona mzigo kamwe kulea familia yake.

mimi siamini haya mambo ya pesa.mkipendana,mnasaidiana,kwa aliekuwa nacho,anajaribu kumsaidiana mwenzake.mambo ya kuweka hela mbele,naona kama hakuna mapenzi hapo.mimi nikikupenda,haijalishi unacho au huna muhimu kuwa happy katika relationship.ukiwa happy,vyengine vinakuwa easy.mkiwa pamoja tu,nafsi yako inaburudika,hata katika ndoa,mkiwa na mapenzi,hata kama maisha ndio hivyo hivyo,mnaridhika tu.usione watu na majumba yao katika ndoa na mali zao,wengine huwa na stress tupu utajiuliza huyu kulikoni,mbona ana kila kitu.
 
Msingi wako wa mapenzi/mahusiano ni mawe, simenti na udongo?

Kwa hiyo mtu akiija tani 2 za sement masukuma anaumia???
Msingi wangu ukipekenyua kurasa za nyuma utauona....

Hizo tani za simenti tunazitaka sie? Akhaa !maana achilia mbali kuumizwa msukuma kwa huo mgandamizo, ni kwamba hazitafika kwenye huo msingi...
 
ki ukweli navutiwa zaidi na mwanaume mwenye hela plus awe na zile sifa zingine ninazotaka awe nazo, eti mimi nahudumie nyumba halafu ujifanye una kibesi dah patachimbika
 
Back
Top Bottom