Umuhimu wa "Mentor" katika biashara

Huu uzi ndo resolutions zangu twenty twenty
1.quit social media..am nw a you tuber😊! Nimefanikiwa kwa jf kwa 90%
2.kusoma vitabu walau page 1daily..( Veronica must die)
3.my mentor nadhan ni centonomy na TEDx series!

...its not scary as it looks!√
YouTube is the future of online self development, ukipata muda pitia hizi accounts impact theory, john c maxwell, lewis Howes
 
Nyuzi kama hizi vijana wanazikimbia. Nimefika Senegal na Ghana. Hakika ndiyo maana n'na mahaba na watu wa West Africa.

Wametuacha mbali sana kimtazamo na fikra kwa jumla.
 
Andiko zuri ila napenda kujua kuwa - hivi ni kweli MENTOR lazima awe "mtu" yaani "physical person?". Je huyo MENTOR hawezi kuwa "kitabu" yaani upate kitabu au vitabu na usome mafanikio na njia mbalimbali alizopitia huyo mwandishi au waandishi na wakafanikiwa?

Nauliza hivyo kwani nimekuwa nikisoma vitabu vichache na kupata something humo. Kwa mfano kitabu - The Richest Man in Babylon na vingine vya aina hiyo, naviona kama ni MENTORS wazuri. Unasemaje on this Simbamteme!?
 
mukaruka mzee,

Good idea, vitabu ni best option but lazima awepo Mtu physically ambae yupo on the same environment na wewe.

Haiwezekani kuwa mentored na Mtu yupo USA wakati wewe upo Tanzania mtapishana sana
Books or online ni idea nzuri lakini mostly awepo Mtu physically ambae anajua exactly changamoto unazopitia na ameshapitia exactly
Nimewaza tuu mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Designated Savaiva,
Sawa Mkuu lakini tatizo linakuja kwenye kumpata Mentor, hapa Tanzania siyo rahisi sana kuwapata kwani ubinasfi umetamalaki sana.

Binafsi hivi sasa niko kwenye harakati za kumtafuta mentor wa kunipitisha kwenye biashara ya madini, hususan dhahabu; nataka kujua mengi kuhusu biashara hii ili niishike hii fursa aliyitoa Rais wetu mpendwa John Magufuli kwenye sekta ya madini.

Lakini imekuwa ngumu sana, kila ninayemfikiria kuwa anaweza kuni mentor kwenye sekta hii anakwepa tu. Sasa nisaidieni katika hili; nataka kuingia kama BROKER, kisha niingie kwenye DEALERSHIP. Nisaidieni kupata MENTOR.
 
mukaruka mzee, Ni kweli! Hata Mimi nilijaribu...nilimpata MTU mtaalam na mambo ya ice cream nikamfata anipe ushauri jinsi yakutengeneza ziwe nzuri zaidi,masoko na mambo menginemengine! In short ananizungusha Sana!

Hayupo tayari kunishika mkono...tupo ivo watanzania wengi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka jana nilikua napiga story na mama fulani na hiyo ilikua ni siku yetu ya kwanza kukutana, katikati ya maongezi nikamwambia mipango yangu na kwamba sijui sana kuhusu hiyo ishu ila nataka kujaribu.

Kumbe mme wake anafanya hizo ishu, yule mama akaniahidi kuniunganisha na mme wake kwa muongozo zaidi.

Week iliyofuata nikakutana na mme wake, nilishikwa na butwaa kwakweli, kwa bongo ni kama mtu akwambie nakuunganisha na mtu fulani kumbe huyo mtu ni Mo Dewji (anaweza asiwe na ukwasi kama Dewji ila ana mawe ya kutosha tu).

Yule mzee nawasiliana nae toka siku ile hadi leo kama navyowasiliana na masela tu, mtu poa sana. Hii sio bongo.

Kwa mazingira ya Bongo ni kazi sana mtu akuchukue under his/her wing kukufanyia mentorship tena bure.

Aidha Knowledge is NOT power. Knowledge is only POTENTIAL power. Action is power.

Unaweza kusoma vitabu vyote duniani ila kama hutofanyia kazi utakufa masikini.

Experience is the best teacher, wakati unasoma uwe field kufanyia kazi mawazo yako, usipoteze muda sana kusoma hayo mavitabu maana hakuna point itafika ambayo utaona umeiva na no two situations are the same. Njia aliyopitia mentor wako inaweza kuendana na yako ila haziwezi kufanana.
 
Sasa unawezaje kumpata huyo Mentor?
Si Mpaka akupende na kukukubali?

Tena kama yuko kwenye biashara ya aina unayofanya ndiyo kwanza atakuona kama hasimu wake wakati huo huo utegemee awe mshauri wa biashara yako?




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nazani kuna mambo ambayo yakiwepo unaweza kuhitaji kuwa na mentor mfano mnaofanyakazi kwenye taasisi moja n.k

Lakini eti mentor kwenye biashara hususa kwa hapa bongo sizani,

Labda mtu akushibe sana !

Nijuavyo mimi mentoring & coaching huwa inaweza kufanya kazi kwenye mazingira fulani yakiwepo na siyo kwenye biashara!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point namba 6 umekimbiakimbia tu, njoo uelezee hata Mentor aliishindwa.

Portfolio | 2020
Ameshindwa kuelezea ila ni kweli mtaji sio kizuizi cha kuanza. Ili ufanikiwe katika biashara lazima uwe na biashara na ili uwe na biashara lazima uanze. Kwa hiyo kuanza ni muhimu sana.

Mfano una wazo zuri la kuwa supplier wa mboga na matunda hoteli zote za Kinondoni. Tuseme utahitaji 500,000,000TZS, sawa!

Kuanza idea hauhitaji 500M. Anza na hiyo laki 5. Anzisha kigenge kidogo uanze kutafuta namna ya ku supply migahawa midogo. Kwenye mchakato utajifunza na kurekebisha makosa mengi sana. Utapata connections huko. Kama utakuwa na nidhamu na uvumilivu utajifunza mambo mengi ya msingi. Na utakua kutoka hatua mpaka hatua. Njiani katika hiyo safari utajua namna ya kuupata mtaji...

Just a little bit of summary
 
mukaruka mzee,
Mentor lazima awe ni mtu. Ukihitaji ushauri huwezi kukiendea kitabu na wala ukiwa unapotoka kitabu hakiwezi kukukemea na kukurekebisha, au kukutia moyo na kujadili suluhu
 
Akilinjema,
Mentor ni mwanadamu kwa hiyo inaanzia mahusiano yenu ya kawaida kabla hujamuomba akulee. Pili ni kama unaleleka. Huwezi kuomba kulelewa na wewe ni mbishi, mjivuni na mambo kama hayo. Lazima uwe unaleleka kabla ya kutafuta mlezi.

Kuwa biashara moja sio tatizo maana soko la Bongo ni kubwa. Kama ni biashara ya chakula anafanya na anauza mchele basi wewe nenda kauze magimbi au maharagwe ambayo yeye hauzi. Au kauze mbali na yeye mkoa mwingine au vyovyote vile mtakapoishi bila kugombania wateja. Au fanya biashara tofauti
 
Back
Top Bottom