Umuhimu na hasara za kuwa Group 0 negative

Habari za usiku

Baada ya kupata magonjwa siku za karibuni ikanibi niende hospital ya Benjamin hapa Dodoma.

Nikacheki vipimo vyote ila nilipofika kwenye kipimo cha damu daktari alikuwa ananipa majibu huku Anatabasamu huku akiniambia kuwa nina bahati sana kuna kwenye kundi hili la damu(group 0 negative) na akaniandika jina kwenye White book na kuomba namba yangu.

Akaniambia nikihitajika na hospital nisisite kutoa msaada

Je, kuna umuhimu gani kuwa katika kundi hili(group 0 negative) na hasara zake ni nini hasaa?

Nb: Masomo ya India niliyakimbia yote nilibutua D
Wadau naomba kupata Elimu ya Jambo hili!
Ivi kati ya group O-Positive na O-Negative which is the best blood ambayo inanguvu zaid za kuhimili maradhi mbali mbali ikiwemo Ukimwi.
na ni ipi ambayo Cell zake hazina Rhesus-factor ya kupokea maradhi?
 
Faida:
Mwenye damu group O Negative anaweza kumpa mtu wa kundi lolote la damu.

Hasara:
  • Mtu mwenye damu O negative hawezi kupokea damu kwa kundi lingine lolote la damu isipokuwa kwa O negative mwenzake ( O negative anaweza kumgawia damu O positive ila hawezi kupokea damu kwa O positive)
  • Ndio kundi la damu ambalo wanalo watu wachache zaidi Duniani
Hakika, Pia sisi kuumwa ni aghalabu, ila ukijakuumwa unaweza kwenda 😂😅
 
Huku kusema positive na negative humaanisha nini. mfano: Group O positive, O negative.


JESUS IS CHRIST
 
Hapana asaiv kuna sindano wanachomwa kipindi wanahudhuria clinic ku supress immune reaction kwa mtoto alie tumboni ili asife, Muhimu ni kua watu hawa wanatakiwa wawe waudhuriaji wa clinic mzuri.
Yeah mkuu umemuelewesha vizuri sindano hiyo inaitwa anti-D mjamzito anachoma mimba ikifikisha miezi saba na pia ndani ya siku tatu baada ya kujifungua. cha muhimu ni kuwa muhudhuriaji mzuri wa clinic tu na iwe clinic ya hospitali inayoeleweka baada ya hiyo sindano mimba zinazofuata huchomi tena
 
Tulienda mgodini na jamaa zangu. mazingira yalikua magumu Sana. Wote waliugua na wengine walirudia kuumwa lakini Mimi sijawahi kuumwa mpaka tunaondoka.
 
Mara ya mwsho tulikua phlebotomy room nikapata mbususu kisa mdada alikua O- kama mimi yeye ndo alinitoa damu
Faida nyingine ni kuwatishia wagonjwa wasiende peku mana hata mimi nawaambiaga nna 0- ila nna ngwengwe
Waache kujiachia na imelipa nmeokoa wengi
 
Yeah mkuu umemuelewesha vizuri sindano hiyo inaitwa anti-D mjamzito anachoma mimba ikifikisha miezi saba na pia ndani ya siku tatu baada ya kujifungua. cha muhimu ni kuwa muhudhuriaji mzuri wa clinic tu na iwe clinic ya hospitali inayoeleweka baada ya hiyo sindano mimba zinazofuata huchomi tena
Sio kweli Mkuu kwamba akishachoma kwa ujauzito mmoja basi hachomi tena kwa mimba zinazofuata.

Baada ya ujauzito wa kwanza anachoma hiyo sindano na kila akipata ujauzito inatakiwa kuchoma hizo sindano kwa huo utaratibu uliousema hapo japo zinakuwaga mbili wakati wa ujauzito na akijifungua hiyo sindano ya kabla ya masaa 72 inakuwa ya tatu.
 
Back
Top Bottom