Umri gani sahihi kumjulisha mtoto wa kuasili kuwa ulimuasili?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
5,132
6,931
Hii inawahusu watoto wanaoasiliwa wakiwa wadogo, kabla ya "kujitambua".

Ukiema usubiri mpaka awe mtu mzima ndipo umwambie ukweli, inaweza isiwe sahihi. Kunaweza kumwumiza nafsi kufahamu kuwa kipindi chote alichoishi na wewe hakuwa mwanao wa kumzaa.

Ukisema umjulishe angali akiwa mdogo, alu naona ina unafuu, lakini sina uhakika juu ya umri sahihi.

Unafikiri umri sahihi ni miaka mingapi?
 
Mimi nadhani (maoni yangu) ni vizuri umkuze huku anajua. Yaani mwambie tangu akiwa mdogo. Hii itasaidia kumfanya asipate shock kubwa baade, hasa baada ya kujenga bond na wazazi wake
 
mim wangu nilimwambia ukweli kdogo kidogo kama utan...leo kidogo....kesho kutwa kidogo mpaka ikawa
 
Huwa nashangaa kitu kimoja, kwa nini mtu ukimkuza kama mwanao na atakupenda perfectly kama mzazi wake Ila baada ya kujua kuwa hamuhusiani kwa damu. Inakuwa shida..

Uzazi ni malezi au damu, yote kwa yote, nadhani ni vibaya kumuambia akiwa mdogo sana maana utamnyima nafasi ya kuishi utoto wake akiwa na mzazi kihisia na kiakili. Maana kumjulisha sensitive information kama hiyo itamkomaza mapema na kuanza kufikiria mambo yaliyo juu ya level yake.. Akifika umri wa kujitambua, at least kama kuna umuhimu wa yeye kujua, utamjulisha

Mimi sikuwa adopted ila kuna sensitive information nilikuwa napewa about my past ziliniathiri kiasi japo watu walionizunguka walichukulia kawaida🙏🏽
 
Mimi nadhani (maoni yangu) ni vizuri umkuze huku anajua. Yaani mwambie tangu akiwa mdogo. Hii itasaidia kumfanya asipate shock kubwa baade, hasa baada ya kujenga bond na wazazi wake
kama hutambwambia wewe hakikisha mmoja kati ya ndugu zako watamwambia, au hata mfanyakazi wako atamwambia.
 
Hakuna haja ya kumwambia, unaweza kkuta hata watu unawatambua kam kaka zako na dada zao wala hamna uhusiano wa Damu... Hii dunia ina mengi sana hakuna haja ya kukipa stress kiumbe kilichokuja duniani kufurahia maisha,

Ishi nae kama mwanao utabarikiwa na muumba.
 
Back
Top Bottom