Umewahi kupata mkasa gani barabarani?

Kubebwa na maji mafuriko ya Dar 2016. Gari ikazima ghafla afu ikaanza pelekwa upande. Nilipanik hatari
 
16/09/2016 tukiwa miongoni mwa abiria Mimi na mchumba wangu kwny basi la newforce kutoka DSM kuelekea songea,majira ya saa mbili usiku maeneo ya kifanya njombe basi lilipinduka na kutamatisha maisha ya mchumba wangu, sitakuja kusahau maneno ya mwisho mchumba wangu aliyonitamkia muda mfupi kabla hajakata roho,inauma sana
Pole sana mkuu kwa yote uliyopitia.....dereva wa ile basi nae alifariki mwakajuzi kama sikosei kutokana na madhara ya ile ajari
 
Kuna rafiki yangu mtu wa mitungi sana siku moja kapiga nyagi Yuko tungi balaa anaendesha anarudi home. Baada ya kuendesha kidogo akahisi uchovu na usingizi akajua atapiga mzinga.
Akajisalinisha kituo cha mafuta,akaacha gari wakamchukulia taxi akarudi home ili gari aifuate kesho. Kesho anaamka kama saa nne hakumbuki chochote. Kwenda nje gari haipo funguo anazo akajua kaibiwa gari ila hajui vipi na wapi. Ikabidi akatoe taarifa polisi.
Kama kawaida ya nyagi huwa inakukata memory Kwa muda fulani,jioni sana kumbukumbu zinamjia gari aliiacha kituo cha mafuta na alimlipa mlinzi ailinde ila hakumbuki wapi. Akafuatilia vituo vilivyopo njia anayotumia akaikuta gari salama salimini, ila bado haachi pombe
 
Kuna sehem moja inaitwa Mto Koga kama unatoka Tabora kwa gari unakwenda MPANDA....

Hio sehem ina Mbu sijawahi ona maishani mwangu, tulifika hapo saa nne usiku hivi, tukalala ndani ya Gari,
Asubuhi tunaamka Tyre Zote zina Pancha hazina Upepo.

Mbu wamenga'atanga'ta Tyre zote zimetoboka.
Kama sio chai basi nimekupa like mkuu
 
Ushimen,
Ni kitu cha kawaida sana kama unasafiri barabarani unatoka dar kwenda mwanza unaweza kukutana na mvua hata mara tano na jua pia unajikuta unaendaa kuna bonge la mvua mara kidogo unakuta imekata jua kaliii na mbele kukavuuu
 
Kuna watu wakorofi sana barabarani
Kuna siku tupo nyuma ya gari moja ndogo ghafla ikasimaa nasisi tukasimama eti huyo jamaa anasalimiana na watu walioko ngambo ya pili ya barabara...basi akatokea bodaboda mmoja akampiga ule mkono paaaaa boda akakimbia jamaa akaanza kumkimbiza.tukawakuta mbele wamekamatana sasa sijui yule jamaa askari au jesho maana hao ndo wanaongoza kuvunja sheria
Ila yule boda boda alinifirahisha sana
 
Kuna siku bana nimeenda kufunga bajaji toka dukani sasa tukachelewa sana kufunga fundi kaja kumaliza giza lishaingia dogo niliempanga aje aendeshe ikishafungwa kila nikimpigia simu haipokelewi.... Anakuja kupokea anaongea kilevi si mchezo nikajua huyu kashakula tungi nikamtel basi asije....

Mimi uzoefu wa bajaj sio kivile.... Ila pikipiki mara moja moja nakimbiza... Basi fundi akaniambia braza kama unaendesha pikipiki mbona na hii vile vile tu we amsha tu mwemyewe basi kidume nikajimwambafy pale nikaona sio kesi ngoja ntekenye mashine....

Ebana eeh nimechomoka nayo af naendesha sitaki nionekane sijui so kibati kikali af mashine nyepesiii baada ya kama dk 40 road mashine imeiva nimefika njiapanda moja sijangalia huku wala kule nataka ninyooke ebana eh sijui hata difenda ya polisi ilikotokea ni wapi nayo iko moto vibaya.... Nikawaza tu chap hapa nikifunga breki wananikuta kati na nakufa hapa hapa na nikisema niingie kushoto kwa spidi hii dude linapinduka damn nikaongeza mafuta tu mzee kama kukutana tukutane tu .... Tukakosana kidogo sana yani ... Sikuangalia nyuma ni gia tu nikasema kama wanakuja waje tu kitaeleweka ila jamaa hawakugeuza sijui walikua wanawahi wapi
 
Nakumbuka mwaka jana mwezi wa 10 pale kinondoni manyanya, nilikua na pick up double cabin (left hand) Natokea zangu sheli ya mwanamboka kujaza wese kisha nielekee mjini kupitia njia ya surrender. Sasa nikiwa kwenye mataa pale manyanya nipofika karibu na mataa taaa ikawaka rangi nyekundu ikabidi nisimame. Sasa baabda yakuwaka taa ya kijani nikafumuka speeed maana nilikua nawahi issue fulani, Basi ile kufika katikati ya mataaa bodaboda mmoja akajichomeka akivuka huku mimi nikiwa nimeshafika katikati na niko speed hapo... Basi nikawahi kukanyaga brake lakin hazikusaidia maana tyre zanyuma ziliserereka na wala siku jisumbua kumkwepa maana inhekua hatari kwangu, Nikaenda kumburuza jamaa na bodaboda yake. Yaani daaah jamaa aliumia vinaya sana. Na lile tukio lilitokea katikati ya mataa yaani kila mtu alijionea live pale. Sasa maaskari wakaanza kujisogeza sasa kuhoji, nikajikuta hio mishe yenyewe niliokua naiwahi imeingia doa. Yani sitasahau lile tukio
 
pole sana mkuu. ilishawahi kunikuta pia, taa zimeniruhusu ila boda sijui katokea wapi akanivaa, na alikuwa na abiria. ila kwa ajali inayohusu pikipiki siwezi kusubiri hapo, maana akili zao wanazijua wenyewe. kosa siyo lako ila wakija wengi wanafanya uharibifu. nilisepa kwa kweli na hadi leo sijui waliumiaje.
Nakumbuka mwaka jana mwezi wa 10 pale kinondoni manyanya, nilikua na pick up double cabin (left hand) Natokea zangu sheli ya mwanamboka kujaza wese kisha nielekee mjini kupitia njia ya surrender. Sasa nikiwa kwenye mataa pale manyanya nipofika karibu na mataa taaa ikawaka rangi nyekundu ikabidi nisimame. Sasa baabda yakuwaka taa ya kijani nikafumuka speeed maana nilikua nawahi issue fulani, Basi ile kufika katikati ya mataaa bodaboda mmoja akajichomeka akivuka huku mimi nikiwa nimeshafika katikati na niko speed hapo... Basi nikawahi kukanyaga brake lakin hazikusaidia maana tyre zanyuma ziliserereka na wala siku jisumbua kumkwepa maana inhekua hatari kwangu, Nikaenda kumburuza jamaa na bodaboda yake. Yaani daaah jamaa aliumia vinaya sana. Na lile tukio lilitokea katikati ya mataa yaani kila mtu alijionea live pale. Sasa maaskari wakaanza kujisogeza sasa kuhoji, nikajikuta hio mishe yenyewe niliokua naiwahi imeingia doa. Yani sitasahau lile tukio
 
pole sana mkuu. ilishawahi kunikuta pia, taa zimeniruhusu ila boda sijui katokea wapi akanivaa, na alikuwa na abiria. ila kwa ajali inayohusu pikipiki siwezi kusubiri hapo, maana akili zao wanazijua wenyewe. kosa siyo lako ila wakija wengi wanafanya uharibifu. nilisepa kwa kweli na hadi leo sijui kama waliumiaje.
Ni Mimi mkuu nilikua ntakutafuta sana
 
Kisa kingine, natoka Mwanga, kuna watu nilienda nao, narudi alone niko kwenye Noah, nikafika Mombo ilikua Jumamosi nikakuta vichwa kibao, sasa lile gari lilikua linakunywa mafuta hakuna mfano, nikaamua kupunguza gharama ngoja nile vichwa, sa kumi na moja jioni hio, destination ni Dar na gari haina Taa za Maana kwahio inabidi nikimbie niwahi kufika mjini kidogo.

Tukio la kwanza. ukipita kijiji cha mandera kabla ya kufika Wami, nikakutana na Fuso limeharibika na wameweka majani, kwakua nilikua speed kiasi nikayavaa yale mamiti wanayoweka, nusura niingie nyuma ya Fuso. Nikatoka hapo nikawa nalifuata basi la TYahmeed ili at least nioapte mwanga,

Tukio la pili, nikiwa nakaribia Bagamoyo saa tatu kasoro usiku, ghafla nikawaona punda watatu hivi wanakatiha barabara, wawili wanamalizia kuvuka halafu mmoja ndio amejaa kwenye site yangu, dah ilibidi nimvamie tu, gari iliyumba kiasi but ikusimama hadi pale Total Filling station Bagamoyo nikakuta gari imemumia kidoogo
Hahahhahha daaah we jamaa una majanga sana barabarani
 
Kuna traffic police mmoja kituo cha kivukoni pale ana tabia ya kuvizia uki park pale kwenye zile parking pembeni ya kituo .. hana kazi nyingine zaidi ya kubahatisha makosa pale kweny parking.. alinizuia kisa natembea na spare tairi wakati nimetoka kupata pancha nikabadili muda si mrf.. alichukua pesa yangu kwa kuwa nilikua na haraka sikutaka mambo yawe mengi.. huwa namuona sana anavizia watu pale kwenye parking
Yupo mmoja upande wa kigamboni wanamwita "wa mikanda" huyu akikufuma hujafunga mkanda kazi anayo.
 
Back
Top Bottom