UMEME: Tanesco, Ngeleja OMBENI MSAMAHA Kwa KAKOBE

Ngeleja ndiye anajua nini kinaendelea pale na Mkurungez TANESCO anafahamu ndio maana wanahaha kufanya matengenezo.Serikali haiamini Uchawi lakini Kikwete akianguka anakimbilia Bagamoyo badala ya kuwaona viongozi wa dini!

mkuu hapa sijaelewa naomba unifahamishe. Ina maana umeme umeshindwa kuvuka pale kwa Askofu Kakobe au ni issue nyingine?
 
[h=2]Ngeleja ameanza Uchunguz umeme 132kv kwa Kakobe[/h]
Tafakuri Yangu Ya Leo: Ya Kakobe na TANESCO mwogopeni Mungu tujaribu kwa Mafisadi




KAMA kuna jambo linalowakera watanzania basi ni hili la Ufisadi miongoni mwa baadhi ya viongozi wetu. Watanzania wanajiuliza, iweje wao waendelee kuwa masikini ilihali wachache wanazidi kuneemeka huku wakikodi ndege kwenda kutumbuliwa vipele huko Berlin Ujerumani? Sasa mimi nina pendekezo binafsi mkiona linafaa tulifanyie kazi wadau.

Hivi mnakumbuka enzi zile za mgogoro kati ya Askofu Zakaria Kakobe na TANESCO? , Kakobe aliendesha harakati zisizo na umwagaji damu akazipachika jina la "TANESCO Mwogopeni Mungu !!" na fulana za njano alichapa tunazikumbuka, Sasa kwa nini na sisi tusitumie mbinu hii kuwashughulikia Mafisadi?

Na hii iwe Tafakuri yangu ya leo jamani……

Nova Kambota Mwanaharakati
"Kitendawili sio deni ukishindwa nipe mji"
0717-709618 au 0766-730256
novakambota@gmail.com
novadream.blog.com
10 Machi 2011
Njombe , Tanzania.
 
[h=2]Friday, March 19, 2010[/h]
MABANGO YA KANISA LA KAKOBE YAONDOLEWA
Sasa hivi katika pita yangu mitaa ya Mlimani city huku Mwenge nimekuta mafundi wa TANESCO na kampuni moja toka JAPAN wanayaondoa mabango ya kanisa la FULL GOSPEL FELLOW SHIP ambalo linaongozwa na Mchungaji Zacharia Kakobe chini ya ulinzi mkali wa polisi bila shaka kuruhusu kupitishwa kwa waya za umeme.


Juu na chini ni mabango ya kanisa la Kakobe yakiondolewa kwa winchi
-------------------------
HABARI KAMILI
Hatua hii inakuja baada ya serikali kuliruhusu Shirika la Umeme (Tanesco) kuendelea na mradi wa kupitisha nyaya za umeme wa msongo wa 132KV juu ya eneo hilo, baada ya ya waumini kulinda majengo ya Kanisa hilo la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) kwa takribani miezi mitatu

Waumini hao walikuwa wakikesha usiku na mchana kwa lengo la kuzuia wafanyakazi wa Tanesco kupitisha nyaya hizo juu ya kiwanja cha kanisa hilo lililo jirani na eneo la Mwenge wilayani Kinondoni baada ya mkuu wa FGBF, Askofu Zacharia Kakobe kupinga mradi huo na kutangaza eneo hilo kuwa la hatari kwa wafanyakazi wa shirika hilo la ugavi wa umeme.

Askofu Kakobe anadai kuwa mradi huo wa thamani ya Sh34 bilioni kutoka serikali ya Japan haufai kupitishwa juu ya eneo la kanisa hilo kwa kuwa ni hatari kwa afya za waumini wake na unaweza kuharibu mawasiliano ya ndani wakati wa ibada, ambazo alisema hurekodiwa wakati zikiendelea na pia kudai kuwa utavuruga mawimbi ya televisheni kwa kuwa kanisa hilo lina mpango wa kujenga studio ya runinga.

Askofu huyo alidai mradi huo ulipingwa na wakazi wa maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndio maana ukakwepeshwa hivyo anataka Tanesco pia ikwepeshe nyaya zinazotakiwa kupita juu ya kanisa lake lililo kando ya Barabara ya Sam Nujoma.

Lakini Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja jana alisema kuwa serikali imejiridhisha kuwa mradi huo hautakuwa na athari za kimazingira na afya ya binadamu na hivyo kutupilia mbali ombi la Askofu Kakobe la kutaka nyaya hizo zipitishwe katikati ya Barabara ya Sam Nujoma.

Ngeleja, ambaye wizara yake ilifanya vikao kadhaa na uongozi wa FGBF, alisema eneo la katikati ya barabara hiyo haliwezi kutumika kwa ajili ya nyaya hizo kwa kuwa tayari lina nguzo za taa za barabarani na kuongeza kuwa eneo hilo la kati linakusudiwa kutumika kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.
 
Angel Mungu hulani kizazi hata cha tatu kwa dhambi ambazo babu zao walikosa. Kwani kizazi cha tatu kina kosa gani? Mungu hulaani nchi kwa dhambi wanazofanya watu. Ilitakiwa waTanzania tukemee kile kitendo lakini wengi wetu tulikaa kimya ina maana tulikubaliana na serikali. Tena wengine walikebehi sana. Sasa usishangae Mungu kulaani nchi nzima. Na laana hii itaendelea watu wasipotubu dhambi hii. Kakobe ni mtumishi wa Mungu na Mungu huwa hapendi watumishi wake wakitukanwa na kusumbuliwa. Alimpa ugonjwa wa ukoma Miriam dada yake Musa kwa kosa la kumsema kaka yake. Huyo ni Mungu wetu Angel. Ni Mungu mwenye enzi na mawazo yake yako juu sana tofauti na sisi tunavyodhani. Nchi kupata umeme piga goti tubu kwa dhambi waliyoifanya Tanesco na Serikali dhidi ya kakobe. Unajua Angel Mungu wetu ni wa Upendo. Jibu la hii ni kuvunja hii laana kwa kutubu na kuomba rehema kwa Mungu kisha kuikataa. Mungu atatenda.
Ngeleja na ccm ni wabaya sana ila siungi mkono hoja ya kuamini kuwa MUNGU ANAWAHUKUMU WATANZANIA WOOTE WAKE KWA WAUME, YATIMA KWA WAJANE, WALEMAVU NA VICHANGA, MAASKOFU, MAPADRI, MASHEHE NA WAUMINI WAO KWA KUWAPA ADHABU YA KUKAA GIZANI NA KUBEBA MATATIZO MENGI YATOKANAYO NA MGAO ETI KISA NGELEJA KAKOSANA NA KAKOBE, NAWASI HI MSIFIKIRI HILO KWANI MUNGU NI WETU SOTE NA HAWEZI KU2ADHIBU WOOTE KWA KOSA LA NGELEJA, KM KAKOBE ALILAAN KUWE NA STATIZO LA UMEME WATZ WATESEKE BAS NAAMINI NAYY AMELAANIWA KWANI IMEANDIKWA USILAANI USIJE UKALAANIWA, NAOMBA MSIMSINGIZIE MUNGU UZEMBE NI WA JK, NGELEJA NA SERIKALI YA CCM
 
Angel yule ni mtumishi wa Mungu. Nasikia alikuwa na mpango wa kuanzisha television. Na huo umeme hawezi tena kufanya kitu tena na hizi ni njama za shetani kuzuia injili isienee. Angel soma biblia vizuri na uombe Roho Mtakatifu akufahamishe maana ya kile unachosoma. Mungu aliwalaani wana wa Israel wote waliotoka Misri wasifike Kanani kwa sababu ya dhambi isipokuwa Caleb na wenzake na wale waliozaliwa jangwani. Mungu huangamiza watu wote kwa ajili ya dhambi za wachache. Lakini Angel tukipiga magoti sawasawa Mungu huyu ni wa rehema. Ataiokoa nchi kwa sababu ya wachache wanomtumikia. Ukitubu kwa dhambi hii Angel Mungu ataiokoa nchi hii na adha hii kwa ajili yako. Simama tu hapo palipobomoka.
sijawah na wala siwezi kuthubutu kusema kuwa biblia imeandika kuwa tanesko wapitishe umeme kwenye kanisa la kakobe kwani imeandikwa usiongeze wala kupunguza neno nami siwezi kupinga neno la mungu, kwanini mnasema kakobe alilaani umeme usiwake kwa watz wote? Je yy ni nani mbele ya mungu awezaye kulaani taifa zima liteseke?
 
Am tired talking about da same ****** ngereja and his goverment. kikwete is da worse, i expect nothing frm hm.
 
sijawah na wala siwezi kuthubutu kusema kuwa biblia imeandika kuwa tanesko wapitishe umeme kwenye kanisa la kakobe kwani imeandikwa usiongeze wala kupunguza neno nami siwezi kupinga neno la mungu, kwanini mnasema kakobe alilaani umeme usiwake kwa watz wote? Je yy ni nani mbele ya mungu awezaye kulaani taifa zima liteseke?



Mbona Elia aliomba na Mvua haikunyesha katika Israel Nzima kwa Miaka 3,Elia alikuwa nani na Kakobe ni nani? Au unadhani kizazi hiki hakina wakina Elia?!! "Wenye Haki wangu wataishi kwa Imani"
Nenda Full Gospel kajifunze Neno la Mungu!!
 
Hivi relate vitu unavyoongea! Hivi BABU yupo juu tena baada ya Kupigwa chini na Kakobe? Babu ni Kushney.

ninavofahamu ni kwamba Mungu anaweza kuangamiza hata dunia nzima kwa makosa ya wachache.

Mi naona hamjaelewa. Ngeleja haadhibiwi yeye kama Ngeleja, anaadhibiwa kama WAZIRI WA NISHATI NA MADINI. hivyo laana ikiwepo kwa waziri maana yake ni pamoja na Wizara na taasisi ndani yake.


Umesema Vyema,Kwa dhambi aliyofanya Adamu na Hawa,Wanawake wote na wanaume wote tunalipia mpaka leo until mtu ampokee Bwana Yesu!!
Tatizo watu wanayaangalia mambo katika akili za kibinadamu!!!
 
Tafsiri rahisi ya Biblia inasema kile usichopenda utendewe, usiwatendee watu wengine, pia inasema kama kitu ni sumu kwako usimpe mtu mwingine. vilevile Biblia inasema mpende jirani yako kama nafsi yako(habakuki 2.15, mathayo 7:12, 1-12) kila amchukiaye ndugu yake ni muuaji(1yoh3:13-16). Je jiulize ngeleja na jk wangepitisha ummeme huo juu ya nyumba zao au mbele ya nyumba zao wangekubaliana. Halafu kwann walidanganya umma wakidai umeme huo hauna madhara halafu walipofunga nguzo wakaandika mabango hatari. Hivyo, Mungu akaamua kujibu maombi ya Kakobe ya kutopitisha umeme katika nguzo hizo pamoja na kuleta upunguuf mkubwa wa umeme nchini. Kama ngeleja na jk hawatatubu hadharani umeme utaendelea kuwa tatizo hata kama Mabwawa yote yatajaa maji.

kwa maandiko haya inatosha kuthibitisha kuwa Biblia inakataza umeme huo kupitishwa mbele ya kanisa hilo kwa jinsi serikali ilivyofanya huku ikijua umeme huo una madhara hata tu kwa mtu anayepita chini ya nguzo hizo

nisiwachoshe mm napita mwenye masikio ayasikie maneno haya kama kuna anyebisha aendelee kufuatilia sakata la umeme nchini tangu wamdhulumu haki yake kakobe, yametokea yafuatayo
1. Gesi iliyodaiwa inaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 30 ijayo inadaiwa imekauka hakuna gesi ya kuchimba mda mrefu hivyo
2. baadhi ya makampuni ya gesi yamefunga biashara hiyo na kuondoka
3. transforma na miundombinu mingi ya Tanesco kila kukicha imekuwa ikiharibika na kuleta hasara ya mamilioni ya shilingi
4. bwawa la mtera na mengineyo yamekauka kwa gahfla hata ulifikia wakati jk akadhani watendaji wake wanamdanganya au yule anayefungulia maji anafungulia kwa ajili ya kilimo, akaenda mwenyewe kujiona, kamuulizeni alichokiona hajawahi kukiona
5. umaarufu wa ngeleja na wizara yake vimesambaratika kabisa, kila ngleja akiinuka kujitutumua kashfa za aibu kama akina Jairo zinaibuka na kumzamisha chini kilindini, hafurukuti, bila kubebwa na rais wa magamba, angekuwa amefukuzwa kazi ya uwaziri siku nyingi
6. hakuna mradi wa umeme unaobuniwa na kufanikiwa,

jamani eee fanyeni utafiti mtaona

cha kusikitisha majanga mengine mengi yameendelea kama
1. hali ngumu ya maisha imeongezeka kuliko wakati wowote ule
2. mafuriko ambayo kila mtu anashangaa jinsi yalivyotokea na hakuna anaweza kukuelezea maji hayo yalikotoka na kusomba nyumba n.k

haya ni mapigo ya hasira ya Mungu kwa watu kutokana na dharau za jk na ngeleja wake kwa mtumishi wa mungu Kakobe
 
muulizen jk kuna kipindi aliwtuma usalama wa taifa kutafuta ku- dito kakobe, waulizeni usalama wa taifa walichokiona na hata jk muulizeni alichoambiwa

ccm hawana adabu kwa watumishi wa Mungu kama aina Kakobe wanadhani ni mashehe wa Bakwata, ngoja Mungu awaipge kama ilivyokuwa enzi za Farao hadi kieleweke na washike adabu yao
 
Mwenye updates atupie.. Huo wa 132 kv unapita? Maana mwanzo ulikuwa wa 180kv,sina kumbukumbu kamili..
 
kama kweli NGELEJA alipitisha umeme kanisani kwa kakobe bila kufata haki na KAKOBE akaudhika na hilo bas ni vyema NGELEJA akaombe KAKOBE msamaha ambaye ni binadamu mwenzake na si nabii na atoe mawaya yake.
 
kama kweli NGELEJA alipitisha umeme kanisani kwa kakobe bila kufata haki na KAKOBE akaudhika na hilo bas ni vyema NGELEJA akaombe KAKOBE msamaha ambaye ni binadamu mwenzake na "si nabii" na atoe mawaya yake kwani imeandikwa unapomkosea mtu usiendae msikitin/kanisani kumwomba MUNGU akusamehe rudi kamwombe uliyemkosea msamaha na Mungu atakusamehe.*~*~* WA KUABUDIWA, WA KUHESHIMIWA NI WEWE MUNGU,
 
Nabii Eliya alisema kwa mfalme Ahabu kuwa mvua haitanyesha katika nchi kwa miaka mitatu na nusu na ikawa hivyo. Watu wote wa nchi ile waliteseka bila kuchagua mtoto, mkubwa, mzee na hata mfalme mwenyewe. Hadi hapo Eliya alipoomba tena na kutoa sadaka na hapo mvua ikanyesha. Mambo ya rohoni si ya kubishania maana kama Neno lilishajidhihirisha ni vizuri hatua ikachukuliwa ili kunusuru madhara zaidi.
 
Back
Top Bottom