Umejifunza au ulijifunza jambo gani kipindi unapopitia au ulipopitia nyakati ngumu maishani mwako?

Baada ya kupitia nyakati kadhaa ngumu kwenye maisha, nimejifunza yafuatayo:-​
  1. Kila wakati mgumu unaoupitia, kuna funzo unalipata ambalo litakusaidia mbele ya safari. Funzo linalokuja in terms of maumivu linaeleweka kwa urahisi kwenye akili ya binadamu kuliko funzo kwa namna ya maelezo.​
  2. Nyakati ngumu hazidumu. Kuna wakati nilijua nitakufa. Niliona watu waliokufa huenda wamepumzika na mateso ya dunia na nilitaka nipumzike (it was too much). Lakini leo hii nikikumbuka, nabaki nacheka na kumshukuru Mungu kwa kunivusha.​
  3. Nyakati ngumu bado zitakuja. Kama ambavyo nilipambana nikavuka kwenye kile kisanga 2022, maisha yangu yakarudi katika hali ya kawaida, now nimekutana na kingine na huenda after hiki kinaweza kikaja na kingine. Hivyo namshukuru Mungu kwa kila kitu na kuendelea kuomba anipe nguvu, utulivu wa nafsi, amani, subira na moyo wa kuendelea kupambana bila kukata tamaa wala kumkufuru.​
  4. Haupo peke yako. Hii dunia kuna nyakati ngumu watu wanapitia. Watu wanapitia matatizo makubwa sana ya kifedha, ndoa na mahusiano, changamoto za kiafya, kupoteza mali na kufilisika, kukataliwa, kusalitiwa, kuibiwa, na kadhalika. Kama uko kwenye kipindi kigumu kwa sababu umefukuzwa kazi, kumbuka kuna mwanetu pale Muhimbili figo zimefeli na hakua mlevi wala nini. Kumbuka kuna jamaa kasalitiwa na mke wake mpenzi wa miaka 10. Kumbuka kuna jamaa duka limeungua moto na hakua na bima. Kumbuka kuna mangi kafilisiwa na benki baada ya kushindwa kurudisha mkopo. Watu wana matatizo mengi.​
  5. Hesabu baraka zako. Katika hayo hayo matatizo, bado kuna baraka fulani ambazo Mungu amekupa. Kuwa hai, kuwa mzima wa afya, kuwa na sehemu ya kuishi, kuweza kupata hicho kiasi kidogo cha fedha, kuwa na familia inayokusupport na kukutia moyo n.k.​
  6. Mtumainie sana Mungu. Kuna nyakati ngumu zinakuja lakini unakuta ulishafanya kila maandalizi, kuchukua kila tahadhari kwa weledi na umakini wa hali ya juu. Pamoja na yote, kitatokea kitu kidogo tu kitakwamisha kila kitu na mambo yote yataharibika. Hapa tunafunzwa, pamoja na uwezo mkubwa wa kiakili tulionao, mambo mengine yako nje ya uwezo wetu wa kucontrol. Hivyo, mtumainie sana Mungu unapoianza safari yako upya. Bila ridhaa yake, nothing will ever get done.​

 
1. Hakuna anaekujali zaidi yako wewe mwenyewe.

2. Kila mtu anapitia magumu kwa nyakati tofauti tofauti kwahiyo pambana hauko peke yako.

3. Kuna mambo ukipitia hayakuachi bure(yanakufundisha).

4. Jipe muda na usijiumize kwa vitu ambavyo kamwe haviwezi kuwa ndani ya uwezo wako.

5. Samehe na sahau.

6. Ishi maisha yako hakuna atakaekusaidia kuyaishi.
 
Me nilikula msoto kipindi flani..ila ndugu zangu na jamaa angu mmoja hivi ndio walisimama na mimi..the rest tumebaki kufahamiana tu ila ukaribu sina tena na wao
 
Habari za muda huu wapendwa.

Maisha ni safari ndefu sana yenye milima na mabonde.

Kuna nyakati unapitia Raha mpaka unajiona hapa duniani upo peke yako.

Kuna nyakati unapitia msoto mkali mpaka unajuta kuzaliwa, lakini kila nyakati tunazopitia kwenye maisha zinabeba ujumbe na mafunzo ambayo unaweza kunufaika kwayo siku za mbeleni.

Si vibaya kama uta share baadhi matukio ya nyakati hizo zilizokufanya ujifunze mambo mengine ya msingi.

NB;
Mimi binafsi nilipofukuzwa na kazi na kuishi maisha ya dhiki ndio nilijifunza kuwa thamani ya mwanamume kwenye jamii, ndoa au hata familia ipo kwenye kutoa.
Ukianguka kiuchumi ndo utajua ulikua na ndugu au na mafisi, marafik au mashetani, mke au malaya, then after hapo sasa utamtafuta Mungu na utatubu kisha atakurudisha sehemu ulipokua mwanzo, ACHA MUNGU AITWE MUNGU........
 
Habari za muda huu wapendwa.

Maisha ni safari ndefu sana yenye milima na mabonde.

Kuna nyakati unapitia Raha mpaka unajiona hapa duniani upo peke yako.

Kuna nyakati unapitia msoto mkali mpaka unajuta kuzaliwa, lakini kila nyakati tunazopitia kwenye maisha zinabeba ujumbe na mafunzo ambayo unaweza kunufaika kwayo siku za mbeleni.

Si vibaya kama uta share baadhi matukio ya nyakati hizo zilizokufanya ujifunze mambo mengine ya msingi.

NB;
Mimi binafsi nilipofukuzwa na kazi na kuishi maisha ya dhiki ndio nilijifunza kuwa thamani ya mwanamume kwenye jamii, ndoa au hata familia ipo kwenye kutoa.
Nimejifunza kuwa unapopita kipindi kigumu kwanza jua kuwa hayo ni mapito tu na sio makazi ya kudumu. Pili usitetereke na kujikuta unafanya mambo ya kujidhalilisha au kuharibu malengo yako ya awali. Tatu nimejua kuwa mapito magumu ni majaribu na kuna faida endapo utayashinda utakuwa bora zaidi kuliko hapo mwanzo. Na nne mapito ni sehemu muhimu kabisa ya maisha kama ilivyo furaha na mafanikio.
 
Back
Top Bottom