Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
.Hivyo kama wewe unaamini muundo wa canon law ktk Ukatoliki sioni sababu ya wewe kutaka kuniuzia mimi ambaye nimeukataa na kutokuwa Mkristu wa kanisa hilo la Katoliki..
Sijajaribu kukuuzia; nilikuwa naonesha ulinganifu na tofauti ya sheria za kanisa na sheria nchi kwamba siyo moja na hazihusiani.
Kisha basi, malelezo yako yote hapo juu unazungumzia Canon law ktk kanisa la Kikatoliki wakati hizi sheria zimeanza toka wakati wa Costantine akitawala Roma.
Hapana muundo wa sheria za Kirumi unatangulia Utawala wa Constantine wa Roma. Na Kanon Law siyo sawa na sheria za Kirumi.
Mkusanyiko wa sheria na kuachagua kile kinachkubalika ktk dhehebu moja sio Canon Law ya Ukristu ila ni ya dhehebu unalozungumzia.
Kuna Canon Law ya Kanisa Katoliki tu.
Labda kwa kukusahihisha vizuri ni kwamba Canon Law zimetumika kuunda mfumo, utaratibu na sheria za nchi nyingi za Magharibi na sisi kama tuloifga na kuchukua mengi toka kwa Watawala wetu (Muingereza) basi bila shaka sheria nyingi zimetokana na Canon law.
Kuna ukweli humo kama vile mfumo wa falsafa za Kirumi na kigiriki zina mchango wa wana Falsafa wa Kiarabu na mafundisho ya Kifalsafa ya mtu kama Mt. Thomas yana msingi mkubwa katika wanazuonni wa Kiislamu ambao walijifunza Aristotle. Sasa hilo siyo jambo geni, jamii mbalimbali duniani zimechangiana katika kuchangia ujuzi wa dunia. Hivyo, katika mifumo yetu sisi leo hii tuna michango ya elimu ya Kiislamu, Kikristu, Kigiriki n.k
Kwa hiyo unaposema sisi wakatoliki tunafanbya hivi na vile ni tafsiri ya Canon law according to Romans Catholic ambayo sii lazima ikubalike kwa Anglican..
Kuna Canon Law moja nayo ni Kanisa Katoliki. Makanisa mengine yanasheria na taratibu zao. Kumbuka kuwa makanisa mengine yote mengi yamekuja baada ya 1600 (kabla ya hapo kulikuwa na Kanisa Moja tu upande wa Magharibi)) na upande wa Mashariki kulikuwa na Kanisa moja la Orthodox (baada ya utengano wa 1054). Kabla ya hapo kulikuwa na kanisa moja tu.
Na madhehebu hayo mengine ya Kikristu yana taratibu zao za kuendesha makanisa yao na haviitwi Canon Law.
na haikuwekwa muhuri kufanyiwa marekebisho na madhebeu mengineyo ambayo yalijitenga na kanisa hilo.
Ndiyo maana zinaitwa Kanuni za Kanisa Katoliki.. siyo Kanuni za Ukristu.
Ni hizi taratibu za uongozi, sheria na tafsiri ya mambo mengi ndizo zimetugawanya katika dini na madhehebu mbalimbali..
Tofauti zetu zinaletwa na mambo mengi zaidi kuliko Sheria za Kanisa.
Hivyo kuwepo kwa mahakama ya kanisa Katoliki na nguvu alopewa Padre au Vatica huwezi kuijengea hema ikawa mfano bora kwa madhehebu mengine ya Kikristu au hata Waislaam,.
Kwanini isiwe wakati Ukatoliki nao ni dini, na mambo yanayohusu mahakama hizo yanayuhusu Ibada, ndoa na mambo ya utawala wa Kanisa hilo?
.kwani waislaam hata yule sheikh Mkubwa wa msikiti wa Mecca bado ni binadamu ambaye hana madaraka makubwa kwa Waislaam wote duniani, hata yeyey anafuata kitabu hicho hicho nachokifuata mimi na anafuata sheria sawa na mimi Mkandara ambaye hata kusalisha watu wawili ni jambo kubwa kwangu.
Na hapo ndipo matatizo yalipo; na ndio sababu wanahitaji serikali kuingilia kati kwani hakuna chombo cha juu cha kusimamia maslahi yote.
Na nazidi kusema ndio maana sote hapa tunaamini dini tofauti kutokana na mifumo kama hii laa sivyo sisi sote tunaamini Mungu mmoja, tungekuwa dini..
labda.
Halafu tazama basi unavyozi8di kujipiteza kwa madai kwamba kama Bakwata sio chombo cha Waislaam je chombo chao ni kipi?..
Siyo madai yangu hayo, hayo ni madai ya baadhi ya Waislamu ambao wameikataa Bakwata kuwa si chombo chao.
Mkuu huwezi kuelewa kwa sababu wewe sii Muislaam. Huwezi kupima uzito wa wa kitu kwa ujazo wa hekima ndani ya Uislaam.. Kifupi Waislaama hawana chombo isipokuwa wanaweza kuunda chombo kinachowakilisha waislaam ktk maswala ya uatwala nma sii dini kama unavyoijua KKK au chombo cha Kikristu..
Sasa huoni hapo ndio tatizo? Kwamba, kama hakuna chombo cha kusimamia maslahi yenu ni vigumu kuweza kujadili na kuwa na msimamo mmoja. Hapa ndipo haja ya serikali inaingia. Lakini sasa ni nani atakayezungumza na serikali kwa niaba ya Waislamu?
Bakwata sii chombo cha Waislaam ila ni chombo kilichoundwa na serikali kwa waislaam..
Je ipo haja ya kuwa na chombo cha Waislamu na nani akiunde?
Ni imani yangu kwamba bakwata iliundwa kwa mpango wa Kisiasa zaidi kukidhi mahitaji ya waislaam kisiasa hasa baada ya kuona nguvu ya KKK ktk Utawala ikabidi wawape Waislaam nao chombo chao ngoma ionekane draw
Na hao Waislamu wanajua hili tangu 1969?, miaka 40 iliyopita? Sasa wafanye nini ili kuondokana na Bakwata?
Bakwata wapo kama NGO zinazoundwa inayojidhughulisha zaidi na Uislaam ktk misaada, kukitangaza chama na kadhalika.. Kesho Bakwata inaweza kunyimwa kibali na ikafa lakini Uislaam hautaondoka kutokana na kufa kwa Bakwata.
Hilo ni kweli, na nisawa na TEC na CCT zinaweza kufutwa lakini Ukristu utaendelea kuwepo. ama?
Huwezi kulinganisha wala kufananisha Bakwata na KKK au chombo kinginecho cha kidini..
Naamini inawezekana tu.