mwandende
JF-Expert Member
- Feb 16, 2017
- 10,525
- 19,909
Lakini kiongozi,,,Mimi ni BAHARIA,,, na sio mvuvi ,,samahani kwa swali langu,,tunaposoma somo la PERSONAL SURVIVE TECHNIQUES... wanasema inapotokea ajali,,haswa mkiwa na life jackets,,mnapaswa kukaa eneo la ajali ili muweze kupatiwa msaada,,,tena muwe kikundi.,,kuliko kuogelea na kutoka eneo la ajali.....sasa naomba kukuuliza,,hao waliokufa umesema walijitakia,,je kwanini iwe walijitakia?
kuhusu wale jamaa wa boti waliopotea nakuzama na kufanikiwa kupona mtu mmoja wale jamaa kile kifo cha kujitakia sababu yule aliepona ndio aliwaambia baada ya kuzama wakati wanazama walibahatika kuvaa life jacket ile boti ikaenda chini sasa wao wakabaki wanaelea ndipo yule nahodha akawaambia itabidi tuogelee huku tukifata maji muelekeo wake wale jamaa wengine walikataa ikabidi kila mtu aogelee kivyake isipokuwa yule nahodha aliogelea kwa kufuata maji ndio pona yake yeye aliokotwa kisiwa cha koma akiwa mzima maana aliogelea mpaka ufukweni alipofika kalala hapo hapo mpaka maji yalipokuwa yanajaa ndo yakamuamsha ndo akapandisha juu ndio akapewa huduma ya kwanza nayo ni uji ila wale wengine wenziwe alozama nao hakuna alopona akiwemo mzungu ndio mwenye safari