Ule mgomo wa walimu wa nchi nzima upo?

MsakaGamba

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
392
141
Wakuu, mwaka jana mwezi Disemba mwanzoni rais wa chama cha walimu alitangaza mgogoro na serikali kutokana na danadana ya serikali kushindwa kulipa malimbikizo ya walimu.
Mgomo huo ulitajwa kuanza kuanzia tarehe 14 januari 2012 kipindi ambacho shule zitakuwa zinafunguliwa. Ukimya uliopo unapunguza joto kama ni kweli kuna dhamira ya dhati ya walimu hao kugoma na kusimamia madai na maslahi yao.

Je, wadau mgomo huo kwa hali ilivyo una dalili za kuwepo au ni yaleyale ya ukunguru wa walimu?
 
Ukunguru wa walimu una maana gani mkuu? Fafanua hapo kwanza,si zani kama ule mgomo utakuwepo kwani bwana Mkoba na Oloch walipiga serikali mkwara ili wapewe hela ya Xmass na Mwaka Mpya sasa walisharambishwa nao wamebakia kimyaaaaa
 
Soma The Guardian ya leo,Tumewaahidi upya.Sasa tutawalipa Mpaka February tutakuwa tumemaliza Deni lao lote-by Sio Kali ya JMT
 
CWT mna mpango gani kufungua matawi katika taasisi ambazo zimeajiri watumishi wenye taaluma ya ualimu kwa mfano vyuo vikuu, TIE n.k
 
Walimu... the most underprivileged group of workers ukilinganisha na kazi inayotakiwa wafanye. Mbaya zaidi wengi ni family people vitu kama kugoma ni ku-risk the whole family in case anything bad happens... Sijui hili kundi lipo vipi? Ni walimu wana umuhimu mno katika jamii kiasi kwamba mgomo tu bila kwenda kazini walimu woote Tanzania bila hata Maandamano yaweza sema loads.... Na kuonesha hasa umuhimu wao ni nini katika hio sector nyeti ya Elimu. No wonder Elimu imeshuka inchini like never before!
 
lakini kugoma si tu kubeba mabango na kutembea barabarani. kiwango cha elimu kinavyoshuka ni mgomo tosha
 
Migomo yaukweli haiandaliwi kwa muda mrefu.

True! Mfalme akichungulia dirishani asubuhi akiwa na "janaba" lake huku mrembo (malkia) akiwa bado anajiviringishaviringisha kitandani kutokana na majamboz ya usiku anakutana na umati wa wanaume umekwisha zingira jumba. Ama busara za hali ya juu zitumike au mfalme na malkia watolewe nduki uchi wa mnyama. Migomo haitangazwi kama harusi.
 
Jiulize matokeo yale mabovu ya kidato cha nne.

Jiulize juzi darasa la saba wamefaulu hawajui kusoma na kuandika.

Hii yote ni migomo bubu na ndio yenye madhara makubwa zaidi
 
Ni walimu waajiriwa wa private schools or government ndo watakaogoma au??
 
Viongozi wa CWT hawana lolote zaid ya kuwatumia walimu kama chumaulete. Hawana kazi nyingine zaiadi ya kuitishia serikali kwa migomo ili waonekane mbele ya walimu wanafanya kazi. Suala la malimbikizo ya mishahara haliwezi kwisha na hata hivyo serikali inajitahidi kulipa. Madeni mengine kama likizo na uhamisaho kwa sasa walimu wanalipwa ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Walimu wana matatizo mengi ambayo mengine yanaweza kupunguzawa na CWT kwani kwa sasa chama kina fedha ya kutosha na vitegaechumi. kwakweli walimu hawafaidiki na chama chao na fedha inaliwa na viogozi tu. Hivi kwanini CWT isipiganie mishahara ya walimu kupanda na marupurupu kwa walimu? Hapa naamini kuwa CWT in katawi ka CCM.

CWT acheni kuwadanganya walimu kwa migomo shughulikieni mishahara ya walimu iwe minono kama mnayojilipa hapo makao makuu.
 
CWT mna mpango gani kufungua matawi katika taasisi ambazo zimeajiri watumishi wenye taaluma ya ualimu kwa mfano vyuo vikuu, TIE n.k

Ndugu yangu kkitabu vyuo vikuu walisha jitoa chama cha walimu toka mwaka 1994. Ndio maana mishahara yao ni mikubwa.
 
Back
Top Bottom