Ulaya Yaomba Mkopo Kutoka China

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,605
6,080
Kiongozi wa hazina ya mkopo wa dhamana katika mataifa ya Ulaya yanayotumia sarafu ya Euro Klaus Regling amewasili mjini Beijing,Uchina katika harakati za kuishawishi Uchina kuwekeza fedha katika hazina hiyo.

111028033431_klaus_regling_304x171_reuters.jpg

Fedha hizo zitatumika kuzisaidia nchi wanachama wanaokabiliwa na tatizo la madeni.
China huenda ikaridhia ombi hili na kuwekeza dola bilioni mia moja katika hazina hiyo. Hata hivyo China imesisitiza kwamba lazima ihakikishiwe kuwa fedha hizi zitalindwa kabisa.
Viongozi wa mataifa hayo ya Ulaya tayari wameafikiana kuongeza hazina hiyo kwa dola trilioni moja nukta nne.
 
This is a Chinese century...

na sasa mafuta ya Libya watayanyonya kama yao

China is the superpower tayari.....Obama mwenyewe 'anafyata' mbele ya wachina lol
 
dankie kwa info,dah! WADHUNGU kwishney,haya tusubiri tuwaone hawa wacheza kung fu nao wataifanyaje Dunia.
 
This is a Chinese century...

na sasa mafuta ya Libya watayanyonya kama yao

China is the superpower tayari.....Obama mwenyewe 'anafyata' mbele ya wachina lol
Jamaa huwa wanazunguka kote lakini wakifika kwa wachina wanafyata kabisa na hivi sasa wanakabiliwa na madeni kweli
 
c ndilo taifa lilotabiriwa kwenye ufunuo na daniel juu ya kukuwa kwake kwa uchumi na kupinga juu ya marekani kutaka kuitawala dunia
 
watu wanatabiri kuwa mchina atamuovatake us kwenye 2020 but seriously kwa muonekano wangu ni chini ya hapo, hoping 5 years to come. Hata kijesh wako speedy sana hawa watu
 
dankie kwa info,dah! WADHUNGU kwishney,haya tusubiri tuwaone hawa wacheza kung fu nao wataifanyaje Dunia.

Ila hawa watu nao siwaamin kabisa wenyewe pesa mbele, hawana tofaut na ndugu zetu wachaga, hata sumu waweza kukupa
 
je wabongo tunajifunza nini katika hili?
Tutajifunza kitu gani wakati viongozi wako bbusy kufisadi rasilimali za nchi, shilingi kila siku inashuka Waziri wa Fedha anapiga porojo tu wala hawaji na alternative solution za kuokoa shilingi
 
watu wanatabiri kuwa mchina atamuovatake us kwenye 2020 but seriously kwa muonekano wangu ni chini ya hapo, hoping 5 years to come. Hata kijesh wako speedy sana hawa watu
Baada ya miaka 5 kutakuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye uchumi hasa wa nchi Asia
 
Huu sio mkopo, China wananunua Bonds za EFSF. Wanajua uchumi wa EU ukisimama kutakuwa hakuna wa kununua vitu vyao.
 
Acha wachina waendelee, ila nao vijijini ni choka mbaya!! Ama kweli maendeleo ni kitu tofauti kabisa na tunavyochukulia.
 
Back
Top Bottom