ulanguzi wa tiketi feri za ZNZ

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Hawa maswahiba bana, hawauzi tiketi dirishani. Wamepanga mawakala kuanzia posta mpya yaani wakikuona na kibegi utaandamana nao hadi kwenye gati. Na pale tiketi wanazo mkononi, tena zimeandikwa tayari, bei isiyo halali. Mie nina jina la kizungu na kihaya leo wanipa tiketi ninaitwa Mabruki! Ikitokea ajali si ndio historia yangu fupi inasahaulika kabisa? Kila tiketi cha juu 5,000/= sijui ndio mfumko wa bei au la............
 
July 2011 nilisafiri kikazi Dar-Zanzibar. Ticket dirishani zimekwisha ikabidi turushwe kwa kununua ticketi Shs 5000 zaidi ya bei iliyoandikwa. Mbaya zaidi jina jipya nikapewa-Ameir S Ameir. Ikabidi ni SMS nyumbani na kwa rafiki hilo jina jipya just in case. Ajali hizi zitokeapo ina maana orodha za wasafiri hazina maana kabisa.
 
kibongo bongo hiyo....magendo kila pahala, madili kila pahala...

viongozi wanapiga madili, wananchi madili....no wonder tunavuna matunda ya magendo na madili
 
July 2011 nilisafiri kikazi Dar-Zanzibar. Ticket dirishani zimekwisha ikabidi turushwe kwa kununua ticketi Shs 5000 zaidi ya bei iliyoandikwa. Mbaya zaidi jina jipya nikapewa-Ameir S Ameir. Ikabidi ni SMS nyumbani na kwa rafiki hilo jina jipya just in case. Ajali hizi zitokeapo ina maana orodha za wasafiri hazina maana kabisa.

No wonder hata hawajui idadi ya watu wanaosafiri kwenye vyombo!
 
July 2011 nilisafiri kikazi Dar-Zanzibar. Ticket dirishani zimekwisha ikabidi turushwe kwa kununua ticketi Shs 5000 zaidi ya bei iliyoandikwa. Mbaya zaidi jina jipya nikapewa-Ameir S Ameir. Ikabidi ni SMS nyumbani na kwa rafiki hilo jina jipya just in case. Ajali hizi zitokeapo ina maana orodha za wasafiri hazina maana kabisa.[/QUOTE]

Dah! Kazi kweli kweli!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom