Ulanguzi wa Maji Dodoma: Waziri wa Maji Chukua Hatua

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,984
2,587
Hii nimepenyezewa na watani zangu wa kigogo

Wananchi wa Dodoma wanataabika kupata maji kutoa mamlaka yao ambayo ni Duwasa, huku Duwasa wenyewe wakiwapelekea wauza maji wenye matenki chini ya ardhi ili wauze

Imekua ni kawaida kwa Duwasa kutoa ratiba ya maji ambayo hawaitekelezi. Ikifika Siku ya kutoa maji mtaa husika wanasema wamepata dharula kwenye mitambo yao. Cha ajabu ni kwamba kuna watu wanauza maji mitaa hiyo hiyo amabao wanapelekewa maji na Duwasa moja kwa moja. Hawa watu hawaishiwi maji na wanauza masaa 24.

Kuna mitaaa kama vile Chidachi, Mkonze, Makulu na Kikuyu. Hawa ndio wamechaguliwa na Duwasa kuwa watakoseshwa maji makusudi ili wale walanguzi wa maji mitaa hiyo wauze vizuri. Unaambiwa mitaa hii maji yanaweza kutoa kwa dakika 20 tu na baada ya hapo unayasubiri wiki inayofuata kwa mtindo huo huo. Yaani kiufupi mwananchi wa mitaa hiyo hawezi pata maji hata lita 100 ndani ya wiki. Lakini cha ajabu wale wanaouza maji ya Duwasa wenye vituo katika mitaaa hiyo hiyo hawaishiwi maji. Hizi ni hujuma na uhuni wa waziwazi unaofanywa na duwasa.

Kinachoshangaza kingine ni ndani ya Dodoma hiyo hiyo kuna mitaa inapata maji kila siku si chini ya mass 9 na wengine wanapata maji hadi siku tatu mfululizo. Wanasema mitaa ya Chinangali, Iyumbu, Chamwino, Maili mbili, Chadulu, Area D, Area A n.k Hii mitaa haina shida ya maji kabisa na wanapata maji mass 24 au chini ya 24 lakini ni kila siku.

Wananchi wanamwomba waziri aingilie kati maana wameshaenda hadi Duwasa lakini hali ndio inazidi kuwa mbaya. Ni kama wanakomolewa sasa kwa kwenda kulalamika. Wanachojiuliza wananchi wa mitaa hiyo ni kwa nini wao tu ndio wakose maji? Kwanini watu wanaouza maji ya duwasa kwenye mitaa hiyohiyo wenyewe hawaishiwi?

Waziri chukua hatua. Duwasa inaangamiza watu Dodoma.
 
Yaani Makao Makuu maji ni ya tabu jumlisha na hili vumbi lake lililopamba moto sahii hali ni mbaya kinoma, huku ni jangwani typically walaqhi'..!!🙌
 
Hameni mrudi Dar
 
Back
Top Bottom