Ukweli wa kuzimika kwa taa za uwanja wa Benjamin Mkapa

Mbaga Jr

JF-Expert Member
May 28, 2018
19,132
41,689
Habari,

Kwa kawaida, mechi zote zinazochezwa muda wa usiku inatakiwa taa pamoja na miundombinu mingine ziendeshwe kwa jenereta. Hii ni kwa kila mechi bila kutegemea ni aina gani ya mechi.

Azam tv wanatoa milioni 300 kwa ajili ya kila mechi za usiku hii ni kwa sababu Azam Media ndio wanaofanya uzalishaji upande wa video, pia serikali nao kupitia wizara ya michezo nao pia wanatoa pesa kwa ajili ya kufanikisha mechi zote zinazochezwa muda wa usiku. Tukumbuke kwamba hizo pesa zote ni kwa mechi moja.

Kiasi chote hiki ni kwa ajili ya mafuta ya kwenye jenereta mana taa zinazotumika pale zinatumia umeme mkubwa.

Najua kuna watu hapa wataniuliza inakuaje Azam Media wanatoa pesa zote hizo kwa mechi moja 🤣 kabla hamjaniuliza naombeni na mimi niwaulize swali 'mnajua Azam Media wanaingiza pesa kiasi gani kwa mechi moja ya kimataifa?

Je, unajua ni kwanini baada ya taa kuzima tanesco walisema wao hawahusiki wakati inaeleweka kabisa kuwa muda wa usiku ni jenereta linatumika? 😂😂

Sasa kinachotokea huko uwanjani ni kwamba,
uongozi wa uwanja badala ya kutumia jenereta kwa ajili ya mechi za usiku, wao wanatumia umeme wa tanesco afu pesa kwa ajili ya mafuta ya jenereta wanaweka mfukoni. Hii wanafanya kwa karibu kila mechi ila ndio hivyo siku hazilingani na ndio kwa bahati nzuri wanapewa surprise taa kuzima kutokana na hitilafu au umeme kuwa mdogo kutoka Tanesco.

Eh em Ngoja niishie hapa 😂😂
Siku njema wakuu
 
Huo mpunga wa Azam mbona unanunua generator jipya brand yoyote ya 500kVA na mafuta ya saa 24 kwa mwezi mzima bila kulizima.

500kVA diesel generator ½ load ni 65l/h.

65×24×30×3100=145,080,000.

Mwezi mzima bila kulizima saa 24 ni 145M.
duh
 
Habari.!

Kwa kawaida, mechi zote zinazochezwa muda wa usiku inatakiwa taa pamoja na miundombinu mingine ziendeshwe kwa jenereta. Hii ni kwa kila mechi bila kutegemea ni aina gani ya mechi.

Azam tv wanatoa milioni 300 kwa ajili ya kila mechi za usiku hii ni kwa sababu Azam Media ndio wanaofanya uzalishaji upande wa video, pia serikali nao kupitia wizara ya michezo nao pia wanatoa pesa kwa ajili ya kufanikisha mechi zote zinazochezwa muda wa usiku. Tukumbuke kwamba hizo pesa zote ni kwa mechi moja.
Kiasi chote hiki ni kwa ajili ya mafuta ya kwenye jenereta mana taa zinazotumika pale zinatumia umeme mkubwa.

Najua kuna watu hapa wataniuliza inakuaje Azam Media wanatoa pesa zote hizo kwa mechi moja kabla hamjaniuliza naombeni na mimi niwaulize swali 'mnajua Azam Media wanaingiza pesa kiasi gani kwa mechi moja ya kimataifa.?

Je unajua ni kwann baada ya taa kuzima tanesco walisema wao hawahusiki wakati inaeleweka kabisa kuwa muda wa usiku ni jenereta linatumika.?

Sasa kinachotokea huko uwanjani ni kwamba,
uongozi wa uwanja badala ya kutumia jenereta kwa ajili ya mechi za usiku, wao wanatumia umeme wa tanesco afu pesa kwa ajili ya mafuta ya jenereta wanaweka mfukoni. Hii wanafanya kwa karibu kila mechi ila ndio hivyo siku hazilingani na ndio kwa bahati nzuri wanapewa surprise taa kuzima kutokana na hitilafu au umeme kuwa mdogo kutoka tanesco.

Eh em Ngoja niishie hapa
Siku njema wakuu
Sio kweli wale ni mbuzi wa kafara tu ila ukweli unajulikana ule uwanja upo chini ya serikali hapo wameamua tu kufa nao ili kupunguza hasira za wananchi ila ukweli unajulikana.
 
Mimi ninacho kujua
Simba ikicheza ule uwanja inatosha Lita 40 za mafuta.

Inatosa asilimia za uwanja. Kwenye get collection nknk.....

Hiyo ya Azam nae kama anatoa Hiyo Fedha Sina uhakika coz Azam haonyeshi Mechi za CAF...

ANYWAY NGOJA NIFANYE UTAFITI.
 
Labda kama Azam kapewa tenda ya kupiga picha mechi za caf zinazofanyika taifa
 
Back
Top Bottom