Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,468
- 23,745
Nakumbuka moja za ahadi za mwana Tanu kuna moja ilikuwa inasema sitopokea wala kupokea Rushwa.miaka ile tunasoma elimu ilikuwa elimu kweli "when education was Education was Education"
Mwaka Jana liliibuka suala flan la Ardhi na mam mmoja alikuwa waziri wa ardhi n.k anafahmika kwa jina la Tibaijuka naye alijikuta anaropoka kuwa alipewa rushwa Million Kadhaa akakataa. na suala hilo likaishia hapo hapo pasipo vyombo vya dola kufuatilia kuwa ni akina nani hao wana ujasiri wa kwenda kumpa Rushwa waziri na wakaondoka salama kabisa pasipo shida zaidi ya yale maneno ya waziri kuwa alikataa rushwa.
Juzi juzi hapa ameibuka ndugu mwingine nimeambiwa ni mkuu wa Mkoa wa DSM naye anasema aliletewa Rushwa na watu mbalimbali za Tsh Mil 5 kila mmoja katika wale waliokuja akakataa na akawaacha waendoke nazo salama salimini.
Nikawaza ukiona mwanaume anakufuata na kukwambia anataka we na uhusiano na wewe mwanamke akakupa pesa kama kukulipa basi ujue amekudharau sana na ameshafaham udhaifu wako ni pesa au kuna watu wameshamwambia kuwa wewe huwa ukihongwa huna hiyana.
Je hawa walimofuata Bwana makonda kumpa rushwa walipata wapi ujasiri huu wa kwenda kumpa rushwa? walijuaje kuwa atahitaj zile pesa ana kama hatoridhika nazo basi atakataa tu?
Je tumejiuliza zaidi? kuwa pengine jamaa walikuwa na dau dogo mhusika akawaambia wakajipange walivyoondoka hawakurudi. alipoona mambo kama hayaeleweki yeye Mhusika akaona kama kuna watu wamemzunguka wamechukua lile dau ambalo yeye aliliona dogo na hapo akajifanya alikataa rushwa?
Kwanini hakuwashtaki siku ile ya kwanza? je haikuwezekana kuwasiliana na takukuru au polisi kuwadhibiti hawa watoa rushwa ikiwa makonda alikuwa na nia njema ya kukataa rushwa?
Hofu yake na ghadhabu za kuona kuwa jamaa hawakwenda kuongeza dau na badala yake pengine wameamua kucheza dili na polisi ndizo zilizomfanya makonda atakamke yale maneno mbele ya waziri mkuu .bila hivyo pengine asingetamka na tusingejua kuna watu walienda kumpa rushwa.
Nilikuwa nimekaa hapa chini kivulini ndo nikawa nawaza haya na mara nimeamshwa na sauti ya mtu anataka nisogee ili apitishe mkokoteni wake. naamka naendelea na safari ya kuokota makopo. sisi machizi tunazunguka jiji lote letu. tunakutana na omba omba wengi tu,machangudoa na makaka poa pia. sijui lini hawa wataondolewa jijini kama ilivyosemwa hapo mwanzo.
"HATUKUUANIKA, WACHA TUUTWANGE MBICHI"