coscated
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 2,919
- 1,968
Nyerere
nasikia alikuwa anaogopa sana challenge za wasomi na ndio maana kipindi
cha utawala wake wasomi wengi walikimbilia nje. Pia kuna tetesi kwamba
Nyerere alienda Makerere University kwa nia ya kusoma Udaktari lakini
alifeli sana masomo ya science, lakini kutokana na urafiki wa wakoloni
na familia ya Nyerere wakaona siyo busara wa kijan wao huyo kuja bila
degree, hivyo wakamwambia asome art yaani Education hasa kwenye masomo
ya historia. Sasa kuanzia aliwaogopa sana wasomi kwani shuleni walimzidi
akadhani na huku kwenye siasa watamfunika vilevile.
Historia ya Kambona siijui sana, kwani ilifichwafichwa aidha bahati mbaya au makusudi. Maoni ni subjective issue,kuna baadhi ya wanahistoria wanadai Kambona angelikuwa rais bora kuliko Nyerere, walichukuliaje swala hili?
Historia ya
Kambona siijui sana, kwani ilifichwafichwa aidha bahati mbaya au
makusudi. Maoni ni subjective issue,
Kila utawala na wahanga wake....nyerere na kambona ...karume na babu abdulrahman
Karume alimwogopa babu kwa elimu yake
inaonekana TANU iliharibu nyota ya Kambona maana ukiangalia kwa makini mapendekezo yake, yalikuwa ya kimsingi na yangepewa nafasi huenda hivi leo tungekuwa tunajadili historia tofauti.
hakika, sio tu Kambona wapo wengi sana kama akina Tuntemeke Sanga, Tumbo na wengineo wote waliopishana mawazo na watawala waliojiita waasisi.
Ziara mbili Ughaibuni zilivunja urafiki na Nyerere
KUNA wakati nilimsikia Hamad Rashid akitoa hoja
bungeni. Wakati huo mbunge huyo wa CUF
alikuwa kiongozi wa Upinzani bungeni. Hamad
Rashid aliomba kambi ya Upinzani bungeni
ibadilishwe jina na badala yake iitwe kambi ya
Ushindani bungeni. Ni kwa vile neno upinzani
linatafsiriwa vibaya na wananchi. Spika Samwel
Sitta alisimama na kutamka; Mtaendelea kuitwa
hivyo hivyo kambi ya Upinzani, kwa vile nyinyi ni
watu wa kupingapinga tu!
Na maneno haya ya Samwel Sitta yanatokana na
historia yetu. Maana; haya ni makosa ya kihistoria
yaliyofanywa na waliojenga msingi wa taifa letu.
Na ndio tunayoyaona hata katika mfarakano wa
miaka 50 iliyopita kati ya Julius Nyerere na Oscar
Kambona.
Na mara ile, mwaka 1965, TANU ilipoachana na
mfumo wa vyama vingi na kuasisi mfumo wa
chama kimoja, Kambona alipata kutamka: Kwa
nini tupige marufuku vyama vingine vya siasa
wakati tunajua wananchi walio wengi wanaipigia
kura TANU? Kambona akaongeza kusema: Bila
shaka, umaarufu wa TANU utabaki kwa muda
mrefu, lakini, je, pale umaarufu wa TANU
utakapopungua, ina maana tuwe madikteta?,
alihoji Kambona.
Nimepata kukumbushia mara kadhaa kuwa
historia ni mwalimu mzuri. Na wanadamu
hatupaswi kuwa vipofu wa historia yetu wenyewe.
Kuifumbia macho historia yako ni kujiandalia njia
ya kutumbukia korongoni kwa kujitakia.
Tunapoadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa
Tanganyika, tuna lazima ya kuipitia na kuitafakari
historia yetu. Kwa macho makavu na maangavu,
tuangalie nyuma tulikota. Tuangalie tulipo sasa.
Ndio, tufanye hivyo ili tuutafute mwelekeo
mwema wa nchi yetu hata kwa miaka mingine 50
ijayo.
Tuna maswali mengi ya kujiuliza, moja kuu ni hili;
Je, ni nchi ya namna gani tutayotaka kuijenga na
hata kuvirithisha vizazi vijavyo? Kwa maneno
mengine; ni jamii gani tunayotaka kuijenga? Sisi
wa kizazi cha Azimio tulikuwa wadogo sana katika
miaka kumi ya mwanzo ya uhuru, na hata
utekelezaji wa Azimio la Arusha. Nimezaliwa Ilala,
Dar es Salaam, Machi 11, 1966.
Ndio, kuna mema mengi tuliyoyaona, lakini
tukitafakari sasa, kuna mabaya mengi pia
tuliyoyashuhudia. Tuna wajibu wa kusimulia mema
na mabaya hayo kwa manufaa ya Watanzania wa
kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Kati ya kumbukumbu zangu mbaya za wakati huo
ni jinsi tulivyowaona wazazi wetu wakiishi kwa
hofu. Waliogopa kushutumu mamlaka hadharani
na kwa sauti. Waliishutumu Serikali na hata
kiongozi mkuu wa nchi kwa kunongona.
Wazazi wetu walimwogopa hata mjumbe wa
nyumba kumi. Ni ukweli kuwa kwa wakati ule,
Serikali na chama tawala havikuwa na uvumilivu
wa sauti za upinzani.
Na siku zote mamlaka bila upinzani huzaa kiburi
na majigambo. Huzaa hali ya kutokujali na kukosa
usikivu. Taratibu, huzaa hali ya kujisikia u-bwana
mkubwa. Hali hii ikiachwa ikaendelea, basi,
husababisha madhara makubwa kwa nchi. Huleta
hasara kubwa kwa nchi, kiuchumi na kijamii.
Juma la jana nilimalizia kwa kuandika kuwa makala
haya ni jaribio la kuvunja ukimya wa juu ya nini
kilitokea takribani miaka 50 iliyopita. Ni mmoja tu
wa mfano wa jinsi umma ulivyofichwa ukweli wa
juu ya nini hasa kilitokea kikasababisha mfarakano
wa waliopata kuwa viongozi wa mstari wa mbele
kwenye harakati za kuanzishwa kwa TANU na
kudai uhuru wa Tanganyika; Julius Kambarage
Nyerere na Oscar Salathiel Kambona.
Kuna aliyesoma makala yangu ya juma la jana na
kuniuliza; Maggid, hivi wewe huogopi? Ni kweli,
kama ningeandika haya mwaka 1976 nilipokuwa
mtoto wa umri wa miaka kumi tu, basi, vyombo
vya dola vingenishukia mithili ya mwewe
anayekishukia kifaranga cha kuku. Sio tu mimi
ningeswekwa rumande ya watoto, bali hata mama
na baba yangu wangetikiswa na dola kwa
dhambi ya kumzaa mtoto mwenye fikra za
kipinzanipinzani na kihainihaini.
Na hapa ndipo kwenye moja ya mapungufu
makubwa ya waliojenga msingi wa taifa letu;
kuchukia wenye kufikiri tofauti na watawala. Na
zaidi kuwachukia wenye akili ya kufikiri na
kuutumia vema welewa wao.
Si tunajua kuwa utotoni tulisikia kuna maadui wa
nchi wa aina mbili; maadui wa nje na wa ndani.
Wapinzani ama wenye kufikiri tofauti ndimo
walimowekwa wanaoitwa maadui wa ndani!
Niseme tu, mfulilizo wa makala haya ni moja ya
makala zangu muhimu tangu nianze kushika
kalamu na kuandika makala magazetini. Na
naandika nikiwa sina hata chembe ya hofu. Ni kwa
sababu moja kuu; kuwa yanahusu historia yetu na
mustakabali wa nchi yetu. Sote tuna wajibu wa
kuandika historia yetu.
Hii ni nchi yetu. Hatuna sababu za kuionea aibu
historia yetu, na badala yake tujivunie kuwa tuna
historia. Na ni unyonge na utumwa kusubiri
wasomi kutoka Marekani na Ulaya waje kutafiti na
kutuandikia historia yetu. Historia yako isimulie
mwenyewe.
Hivyo basi, tuna wajibu wa kuifanya kazi hiyo.
Historia itusaidie kutukumbusha machungu na
furaha ya tuliyoyapitia kama taifa. Si kwa kuandika
tu, hata kwa kusimulia machache
tuliyoyashuhudia.
Niliahidi kuchambua zaidi juu ya marafiki hawa
watatu; Kambona, Nyerere na Kawawa. Nitafanya
hivyo sasa.
Naam. Julius na Oscar walikuwa viongozi vijana
sana katika Tanganyika huru ya wakati huo.
Ikumbukwe wakati tukipata uhuru, Nyerere
alikuwa na miaka 39 na Oscar alikuwa na miaka
36. Hawa walikuwa ni vijana waliokabidhiwa
dhamana kubwa ya kuiongoza nchi kubwa ya
Tanganyika. Naamini walikuwa ni wenye dhamira
njema kwa taifa hili; Julius, Oscar, Rashid na
wenzao wengine katika TANU.
Ukweli unabaki kuwa Oscar Kambona hakuikimbia
nchi yake kwa kashfa ya kuiba fedha za Serikali au
ufisadi mwingine. Na kwa utafiti mdogo tu
niliofanya, nilichobaini ni ukweli kuwa marafiki
hawa wawili; Oscar na Julius walikuwa na
mgongano wa tofauti ya kimaono ya kisiasa
yaliyoathiri hata urafiki wao.
Maana; haiyumkini Kambona aliyeaminiwa na
Nyerere akaja kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa
TANU, akawa Waziri wa kwanza wa Elimu wa
Tanganyika huru, akaja kuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani na hata kwa wakati mmoja kushika wizara
mbili - Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya
Nje. Kwamba aje tena baadae kutuhumiwa
uhaini, na hata kushukiwa uraia wake!
Ndio, kwangu mimi ya Kambona na Nyerere
ilihusu zaidi mgongano wa tofauti za kimaono ya
kisiasa . Na ukiingia kwa undani kwenye maandiko
na simulizi utaupata ushahidi wa haya.
Na kwa hakika, ili siasa ya nchi istawi, basi,
inahitaji uwepo wa migongano ya kifikra. Hivyo
basi, siasa ni migongano ya kifikra yenye kuhitaji
majadiliano endelevu.
Tunaona kuwa migongano ya kifikra kati ya Oscar
na Julius ilianza kuonekana dhahiri katika ziara
mbili walizozifanya kwa pamoja katika mataifa
mawili tofauti. Ziara ya Marekani mwaka 1963 na
ziara ya Uchina mwaka 1965. Na hapo katikati
kuna jambo lililosababisha uwepo wa mahusiano
ya mashaka kati ya Julius na Oscar. Ni uasi wa
jeshi wa Janauri 20, 1964.
Uasi ule ulisababisha Nyerere na Kawawa waende
mafichoni. Inasimuliwa walijihifadhi eneo la
Kigamboni. Mjini alibaki Oscar Kambona
aliyeshiriki kikamilifu kuwatuliza wanajeshi wale.
Kimsingi, katika kipindi kile cha maasi, Kambona,
kama angetaka, alikuwa na fursa ya kutwaa
mamlaka ya nchi akisaidiwa na jeshi. Inasemwa
kuwa akiwa Waziri wa Ulinzi, Kambona alikubalika
sana jeshini.
Baada ya ziara ya Marekani akiwa na Oscar
Kambona mwaka 1963 ambako Rais John
Kennedy alimsifia sana Nyerere kwa kuonyesha
uwezo wa kiuongozi, miaka miwili baadae, mwaka
1965, Nyerere na msafara wake akiwamo Oscar
Kambona, walikwenda China kwa mara ya kwanza
na kulakiwa na Mwenyekiti Mao Tse Tung.
Nyerere akiwa kwenye gari la wazi na mwenyeji
wake Mao, alishangiliwa na Wachina wapatao
milioni moja waliojipanga barabarani.
Pale Ilala tulikoishi, nakumbuka nikiwa na umri wa
miaka sita tu, usiku mmoja pale viwanja vya shule
ya msingi Boma tuliangalia sinema ya ziara ya
Julius Nyerere Uchina .
Nyerere aliiona China na alivutiwa sana. What we
have seen in China is relevant to us, nimemsikia
Nyerere akiongea hayo kwenye kipande cha
filamu ya zamani kilichopo mtandaoni .
Alimaanisha walichokiona China kinaweza
kikafanyika kwetu.
Na Julius alianza kwa kubadilisha hata staili yake
ya mavazi, yakafanana na ya Mwenyekiti Mao, na
wengine katika TANU wakamwiga. Ni nini
kilitokea kwenye Mkutano wa TANU wa Januari,
1967 na kabla ya hapo? Mkutano huo ulisababisha
kumalizika kabisa kwa urafiki wa Nyerere na
Kambona. Fuatilia toleo lijalo.
Kifo cha sokoine nyerere alihusika asilimia 100 . Huyu mzee hakutaka mtu wa kutofautiana naye chochote . Alikuwa dikteta mmbaya sana.