Ukweli kuhusu suala la deni Afrika waendelea kuwekwa wazi, nchi za Magharibi haziwezi kutwisha lawama kwa wengine

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
下载.jpg


Kwa muda wa karibu muongo mmoja sasa vyombo vya habari vya nchi za magharibi vimekuwa vikipata matope China kuwa ni chanzo cha mzigo wa madeni kwa nchi za Afrika, na kufanya baadhi ya watu waamini hivyo. Lakini baada ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na taasisi huru za nchi za magharibi, imeonekana wazi kuwa ni nchi za magharibi ndio zimeliingiza bara la Afrika kwenye msukosuko wa madeni.

Hivi karibu gazeti la The Guardian la Uingereza toleo la Julai 12, lilikuwa na makala yenye kichwa “Nchi za magharibi zinapaswa kuwalazimisha wakopeshaji binafsi kupunguza deni baya kwa nchi za Afrika” (West must force private lenders to ease Africa’s crippling debt). Kwa wasomaji wa kawaida wa gazeti hili, hiki kilikuwa ni kichwa cha habari cha kushangaza, kwani wamezoea kuona kuwa China ndio inabebeshwa lawama kwenye suala hilo.

Mwandishi wa makala hiyo ameinukuu taasisi ya Jubilee Debt Campaign, inayojihusisha na ufuatiliaji wa madeni duniani, akisema asilimia 30 ya deni la nusu ya nchi 22 za Afrika zenye mzigo mzito wa madeni ni la nchi za magharibi, na asilimia 6 tu ya deni hilo ni kutoka China. Deni hilo la China limejikita zaidi kwenye sekta ya miundombinu ambayo inaweza kurudisha hela zilizokopwa, na riba yake ni nafuu ikilinganishwa na deni la nchi za magharibi na muda wa kulipa ni muda mrefu.

Makala hiyo mbali na kuzikosoa serikali za nchi za magharibi kwa kutowasimamia kwa makini wakopeshaji binafsi wa nchi za magharibi, pia imetaka hatua ya China kusamehe deni kwa nchi za Afrika na hata kurefusha au kuahirisha muda wa kulipa deni kwa nchi za Afrika kutokana na janga la COVID-19, kuwa ni hatua chanya. Lakini imekosoa nchi za magharibi kwa kutochukua hatua kama hiyo, na kutaja kuwa hali hiyo imesababisha nchi za Afrika kujikuta zinakuwa na mzigo mkubwa wa madeni katika kipindi cha miaka 50.

Mkuu wa sera katika taasisi ya Jubilee Debt Campaign Bw. Tim Jones, amesema Uingereza na Marekani zinatakiwa kuwabana wakopeshaji wa nchi za magharibi kushughulikia tatizo la deni la nchi za Afrika. Sababu kubwa ni kwamba, kwa mujibu wa takwimu za taasisi hiyo ni asilimia 12 tu ya serikali za Afrika ndio zinadaiwa deni kubwa na China, na asilimia 35 ya serikali za Afrika zinadaiwa deni na makampuni ya nchi za magharibi.

Changamoto iliyopo kwa sasa imefichua zaidi sura ya msukosuko wa madeni kwa nchi za Afrika. Mgogoro wa Ukraine umefanya suala la usalama wa chakula na nishati, kutoa shinikizo kubwa kwa serikali za nchi za Afrika. Bahati mbaya ni kuwa msukosuko huo haujabadilisha muundo wa deni la nchi za magharibi kwa nchi za Afrika, na wala haujapunguza shinikizo lake. Badala yake ni kuwa shinikizo limeongezeka.

Kama makala hiyo ya gazeti la Guardian ingeandikwa na gazeti la China, licha ya kuwa na ukweli huo ingeitwa Propaganda. Hatua ya gazeti hilo kuandika habari hiyo na kunukuu vyanzo huru kutoka nchi za magharibi, inaonesha tena picha ambayo imekuwa ikisemwa kwa muda mrefu na China na nchi za Afrika kuwa “mzigo wa madeni” ni kauli ambayo ni janja ya kisiasa ya kuipaka matope China na yenye hila kwa nchi za Afrika.

Ni wazi kuwa kama nchi za Afrika zikikopa kutoka China kwa riba na masharti nafuu, wakopeshaji wa nchi za magharibi wenye nia ya kuzikamua serikali za nchi za Afrika wanakuwa wamepoteza chanzo kimoja cha mapato yao. Kwa hiyo ni wazi kuwa kelele zao zinatokana na kupungua kwa fursa ya kuzinyonya nchi za Afrika.
 
 
Tanzania hatumo mkuu Wala usiwe na wasiwasi..
Walengwa hapo ni kina Angola,Ghana Kenya,Zambia,Nigeria na Nchi zingine kama hizo
 
Back
Top Bottom