Ukweli kuhusu laana (Curse)

Kwa mfano mtu anaposema anavunja chungu (analaani)familia nzima iteketee na inakuwa kweli.
Naomba kuelewesha mahusiano ya laana na watu kufa.
Mkuu hapo anaroga tu kwani hapo bila shaka msimamizi wa laana hiyo ni nguvu za giza.
 
Maana yangu ni kwamba ili umuone mtu kuwa kalaaniwa, ni lazima watu waseme ndipo nawewe akili yako ielekee huko. Kwani nikilaaniwa napatwa na nini specifically?!
Unapoambiwa ni adhabu unaelewa nini ? Laana ni adhabu kwahiyo anajua Allah atakavyokuadhibu kwani yeye ni mjuzi wa kuadhibu.
 
Hupatwi na kitu chocha amani tele....
Nimeisoma post yako kuhusu aliyempiga mama yake na mwishowe akawa kichaa. Ni hivi hapo siyo laana.! Pengine hata huko kumpiga mama yake ndiyo ilikuwa dalili ya kuugua akili. Pengine alishaanza kuugua akili kabla hata mama hajapigwa. Kumbe alikuwa tayari ana kichaa ambacho kilipanda siku hiyo na kumpiga mama yake. Si jambo dogo kumpiga mama, lazima akili iwe na matatizo kwanza ndipo umpige. Jingine ni hiyo imani ya kwamba umelaaniwa: hii inaweza kukuletea stress kali sana au depression na hasa pale mtoa laana anapokuwa ni marehemu. Matokeo ni kukufikisha kwenye ukichaa(mental illness). Kwa hiyo ni suala la kisaikolojia tu. Wapo wengi wamewapiga mama zao na wamepewa hiyo laana lakini wapo tu na wengine wana maisha mazuri kutuzidi hata sisi "wabarikiwa". Sisemi muwapige mama zenu.Kumpiga mzazi ni kitendo cha fedheha na kujidharirisha. Na hakisafishiki. Mimi nilishakataa kabisa kusikia mtu anasema ananibariki.
 
Kwa kuwa haya mambo yanategemea na kila mtu na mtazamao wake....ngoja tu tulimalize hili suala.....ili kila mtu abaki na upande wake......
 
Kwanza tujiulize neno laana latoka kwenye lugha gani? halafu ndio ulete huo ushahidi wako wa uongo latoka kwenye lugha ya kiarabu maana yake nikuwa mbali na kukubalika na Allah (Mwenyezimuungu) Hilo neno sisi wa swahili sio letu halafu hakuna dini itwayo sayansi kama hujui maana ya sayansi maana yake ni jitaahidi za uvumbuzi upo mkuu sio dini alio Kuja nayo Muhammad na Yesu isibitishe na sayansi hapana sayansi isibitishwe na vitabu vikatifu upo mzee cc waislamu na wakiristo hatuna dini itwayo sayansi upo
LLaana IPO na hauwezi kuizuia isipokuwa waweza punguza makali take.Binadamu hana uwezo wa kumlaani yeyote yule.
Maana ni njia ya asili ya kutoa adhabu kwa yale maovu ayafanyayo mtu hadharani ama gizani.
Ukifanya ubaya malipo yake ni ubaya Mara mbili ama zaidi hapahapa duniani.Vivyo hivyo ukifanya mema.
Njia rahisi ya kuzuia laana ni kufanya mema mara nyingi zaidi kuliko mabaya.
Hakuna binadamu anayeweza kumlaani mwingine bali njia ya asili hutoa haki kwa kila tendo.
 
Laana ipo ila mimi ufahamu wangu ni mdogo sana kuhusu hii kitu,ila simulizi zinaonyesha kuwa kupata laana sio tu lazima uwe wewe umekosa,ila inaweza kurithishwa tokea kizazi kimoja kwenda kingine.It is more spiritually than scientifically.
 
vitabu vya MUNGU vinasema uwazapo tu! unajiombea sembuse kutamka? hiyo huwa ipo kiimani zaidi.
 
revelation= ufunuo ni sahihi lakini naomba majibu ya hayo maswali japo umejibu hilo la sayansi vs laana,thanks but i need more

Tunaanza na definition.
Laana (curse) ni maombi mabaya ama tamko baya lenye kusudio la kuleta madhara (Rom. 3:14). Laana inaweza kutolewa na Mungu ama mtu. Laana inaweza kumpata mtu ama kitu. Mfano Mungu alilaani ardhi, Yesu alilaani mtini usizae matunda kesho yake ukakauka (Luka 6:28).

Baaraka ni nini? ni kinyume cha laana. Ni tamko, kunena vizuri, kutakia mafanikio (Luka 6:28).

Tujiulize kama leo maombi ya kweli (genuine) yanaweza kuleta matokeo chanya ama hasi. Kumbuka laana isiyo na sababu haitampata mtu wala kitu.

Huwezi kuepuka laana: Laana ambayo ni universal huwezi kuepuka mfano Mungu alipolaani creation kwa sababu ya dhambi.

Unaweza kuepuka laana: Toba ni njia mojawapo ya kuepuka laana.
 
watu wakishiba ugali wana matatizo sana, eti hakuna laana! nyie mnaishi jamii ipi? acheni kujifanya hamjui haya mambo, tumieni akili ya kawaida sio sigara bwege
Sasa mkuu unataka kufunga mjadala na ndio kwanza ni post #20, acha watu watiririke maana mtu akitoa ya moyoni kuna sehemu atafika atajifunza kitu kutoka kwako na wewe utajifunza kutoka kwake
 
Katika hali ya kawaida watu wa kale waliaminishwa vitu hivi yaani baraka na neema kuwa vipo alihali kiuhalisia ni kitu ambacho hakipo.. hii ni kwa upande wangu.
Umewahi kujiuliza kwann wanaotoa laana na baraka weng wao husemekana ni wazazi au wazee/walezi kuliko mtoto kutoa laana kwa mzazi?
Je hii laana ilipangwa kwa wakubwa tu wao ndo watoaji wa laana na baraka?

Jibu ni kwamba enzi za mababu zetu maneno haya laana na baraka yalitumika kujenga watoto kukaa katika malezi mazur yaan wasifanye vitu vibaya vya kuweza kuikwaza jamiii lasivyo walitishia watapata laana and vice vesa kwa baraka maneno haya yalitumika kama silaha tu na sikweli.
Na kama kuna ukweli uliwahi kumuona mtu kapata laana papo kwa papo? Hii imejengwa akilini mwa watu kuwa laana huja baadae...hakuna ukweli wowote na ili jambo ni imani tu tumejengewa kama ilivyo imani zingne.
Mkuu Mkuu hata kwenye Bible wapo waliolaniwa na waliopata baraka yuda eskariote alilaniwa "kikao chako kiwe ukiwa asijenge mtu. Mpaka lei pale ni pori.wewe u mwamba na juu yako ntalijenga kanisa baraka kwa petro
 
Maana yangu ni kwamba ili umuone mtu kuwa kalaaniwa, ni lazima watu waseme ndipo nawewe akili yako ielekee huko. Kwani nikilaaniwa napatwa na nini specifically?!
Mkuu RCM !! hivo kwa muktadha wako huu, wataka sema hujaona laana kumfika mlengwa???
au macho yako hayaoni!!!

Naomba, ntapendelea na nitaheshimu ukweli wako.... "Hebu niaambie kwa nini TANZANIA baada ya mwaka 1970 hadi hii leo ipo ktk ufakiri na umaskini wa kutupa tupo under $0.01 GNP ".......Juu ya kuwa Nchi hii imependelewa sana kwa kila neema alizotoa Mwenyeezi Mungu kwa Tanzania....

Saguda47 Hanitoni mattargsm abdulrahmana Dr.adams faida FYI, kabla ya mwaka 1970 Tanzania tulikuwa na kila aina ya huduma, miundombinu, Tz sh currency value GDP high/ GNP above standard Educations level ya kuridhisha , health bora, nk nk nk
 
Tunaanza na definition.
Laana (curse) ni maombi mabaya ama tamko baya lenye kusudio la kuleta madhara (Rom. 3:14). Laana inaweza kutolewa na Mungu ama mtu. Laana inaweza kumpata mtu ama kitu. Mfano Mungu alilaani ardhi, Yesu alilaani mtini usizae matunda kesho yake ukakauka (Luka 6:28).

Baaraka ni nini? ni kinyume cha laana. Ni tamko, kunena vizuri, kutakia mafanikio (Luka 6:28).

Tujiulize kama leo maombi ya kweli (genuine) yanaweza kuleta matokeo chanya ama hasi. Kumbuka laana isiyo na sababu haitampata mtu wala kitu.

Huwezi kuepuka laana: Laana ambayo ni universal huwezi kuepuka mfano Mungu alipolaani creation kwa sababu ya dhambi.

Unaweza kuepuka laana: Toba ni njia mojawapo ya kuepuka laana.
safi sana mkuu Mungu akubariki, ni sahihi kuwa laana inaweza kuletwa na Mungu lakini hapo kwa binadam bado nna dukuduku kwa maana siamini kama mwadam anaweza kuachia laana kwa nguvu zake tu( physical power) bila nguvu ya kiroho ( spiritual power) kuhusika, hiyo imekaaje mkuu
 
Mkuu RCM !! hivo kwa muktadha wako huu, wataka sema hujaona laana kumfika mlengwa???
au macho yako hayaoni!!!

Naomba, ntapendelea na nitaheshimu ukweli wako.... "Hebu niaambie kwa nini TANZANIA baada ya mwaka 1970 hadi hii leo ipo ktk ufakiri na umaskini wa kutupa tupo under $0.01 GNP ".......Juu ya kuwa Nchi hii imependelewa sana kwa kila neema alizotoa Mwenyeezi Mungu kwa Tanzania....

Saguda47 Hanitoni mattargsm abdulrahmana Dr.adams faida FYI, kabla ya mwaka 1970 Tanzania tulikuwa na kila aina ya huduma, miundombinu, Tz sh currency value GDP high/ GNP above standard Educations level ya kuridhisha , health bora, nk nk nk
Naunga mkono UKUTA lakini bado nasisitiza kuwa hapo hakuna laana. Kuna uchakavu wa kisera pamoja kasumba za hovyo za watawala. Hakuna laana wala baraka katika maisha halisi.
 
safi sana mkuu Mungu akubariki, ni sahihi kuwa laana inaweza kuletwa na Mungu lakini hapo kwa binadam bado nna dukuduku kwa maana siamini kama mwadam anaweza kuachia laana kwa nguvu zake tu( physical power) bila nguvu ya kiroho ( spiritual power) kuhusika, hiyo imekaaje mkuu

Angalia definition tena key word ni "maombi" hiyo ni physial power?
 
wakuu habari zenu
kama tujuavyo sote ya kwamba kuna uzoefu uliozoeleka na kukaa mawazoni na katika fahamu za watu yumkini hata mimi na wewe, hii ni LAANA ambayo inaweza kutokana ati na wazazi, mizimu, au Mwenyezi Mungu, katika kufikiria hili nikapata maswali yafuatayo:-
*Je laana ni imani tu au ni uhalisia umpatao mhusika na kumuathiri bila yeye kuwa na njia ya kuepuka?

* Je, sayansi inaweza kutoa ushahidi wowote juu ya hili suala au itathibitisha tu matokeo ya laana mfano maradhi, njaa, ukame, umasikini au vita?

*Je, ni namna gani laana husafiri kutoka kwenye chanzo (mtoa laana) hadi kwa mhanga (anaye laaniwa)?

Karibuni tujuzane wakuu
Dah natamani kujua hii kitu
 
Wao wanajuaje kama nimepata laanawanakipimo cha laana?
ulimwona mtu kalaniwa?
je iyo laana uwa inampataje muhusika kutoka kwa mtoa laana na anayelaniwa?
je unajua kutoa laana?
Ulimpa laana nani?
Maneno yapi unatumia kutoa laana?
Inachukua siku ngapi laana kumpata muhusika?
Naomba leo unipe laana nitoe ushuhuda jf.

Sipendagi ujinga mimi...
Nimeamini wewe si mtu wa mchezo mchezo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom