Ukweli Kuhusu Electronic Fiscal Devices ( EFDs)

Nilimsikia afisa mmoja wa TRA akihojiwa na BBC na VOA jana. Sababu alizozitoa zinadhihirisha kuwa hizo EFDs ni biashara ya mtu ndani ya TRA!

Kwa nini bei ipungue pungue kama vile ni biashara ya machinga; mara laki 8, 7, mara 6?

Wenyewe watoe vigezo vya mashine wanazihitaji na kuwaelimisha wafanyabiashara umuhimu wake ili kila mwenye nia ya kufanya biashara akanunue huko anakojua bei si ghali!

Jp
 
Wanasema na makato ni makubwa 18% ya kile uuzacho

Kwani hiyo 18% wanalipa wao wafanyabiashara au mtumiaji wa mwisho? Wao waweke bei yao wanayotaka alafu waongeze 18% kwenye hiyo bei ambayo ndo itakwenda TRA. Kutolipa kodi halali ndo kunawafanya waone kuwa nao wana stahiki kwenye hiyo 18%.
 
kwanza kabisa kama ilivyotanabahishwa kwenye website ya TRA(Tanzania Revenue Authority - E-Fiscal Devices (EFD))
kuna aina tatu za EFDs, TRA na Serikali wanatakiwa kuchambua wazi ni aina ipi ya hizo devices ambayo inafaa kwa kwa mazingira yetu ya Kitanzania , aina ipi ni kwa kundi lipi la wafanyabiashara? na ichambue bei ya kila divice(kwa mfano Nchi ya Republic of Georgia ni Georgian Lari GEL350 ( The price of the cash register and its maintenance), ambazo si zaidi ya TSH330,000/-)

Watueleze kwa wamejipanga vipi katika kuwaelimisha wafanyabiashara na wateja, ufuatiliaji, management and controlling ya kodi kwa kutumia hizo mashine.

watuambie kama mtu binafsi anaweza kujinunulia yake binafsi na TRA kuja kuinstall programme zao au kama makampuni binafsi wanaweza kusambaza tofauti na wao TRA kwani ni soko huria.

Anyway,
kama wewe unaujua ukweli wowote kuhusu manunuzi, usambazaji, upatikanaji, njia bora ya usimamizi wa kodi kupitia hizi mashine kulingana na mazingira yetu ya kitanzania( ki-Techolojia ,ki-hulka za wafanyabiashara na wateja na rushwa), tafadhali tuungane pamoja kuweka ukweli na ushawishi wetu hapa kuliko kuingia katika malumbano ya kuwalaumu wafanyabiashara au kuwalaumu TRA na serikali bali tujikite katika kuweka ukweli bayana na data sahihi kuhusu huu mradi wa TRA !

mimi naanza na link za upatikanaji wa EFDs

Daisy Technology - The fiscal devices your business needs

Cash Register Manufacturer, Retail Cash Registers, Restaurant Cash Registers, POS Systems

Home page

CASIO 140-CR ELECTRONIC CASH REGISTER RETAIL SHOP TILL | eBay

pt=LH_DefaultDomain_3&hash=item27c87bfaea

Bora tuwe wawazi na wakweli na tukosoe panapofaa kuliko kuingia katika malumbano kati ya hizi pande mbili

Aksante

Ndugu zangu,
Jambo hapa sio bei za mashine za EFDs ingawa kweli bei tajwa ni ghali sana ila tatizo wanalolihofia wafanyabiashara ni kuwa wakizikubali mashine TRA watapata mwanya mkubwa wa kuwagandamiza kwa visingizio vingivingi mfano kodi yako halali unayopaswa kulipa ni shs kadhaa kutokana na kumbukumbu za EFDs wakati ukweli halisi sio huo. Na hili tatizo ndio kiini hasa cha mapungufu ya ulipaji kodi Tanzania.

Serikali haina dhamira ya kweli ya kukusanya kodi ila wanayo dhamira ya kweli ya kuwagandamiza wanyonge. Kama serikali ingekuwa na dhamira ya kweli ya kukusanya kodi basi Rais wa nchi angeonyesha mfano kwa kulipa kodi mbona halipi? Mbona Rais alitangaza tatizo la ukimwi kama janga la kitaifa na akaonyesha mfano kwa kupima afya yeye na mkewe mbona hafanyi hivyo kwenye kodi? Kama Rais anaogopa kodi mbona tunawashangaa wafanyabiashara wa kariakoo wakiogopa kodi? Na kitendo hicho cha Rais kutolipa kodi kinalindwa na katiba je utasema serikali hiyo ina dhamira ya kweli ya kukusanya kodi? Mbona wanasiasa hawalipi kodi na mbona hatujawasikia TRA kwenda kuwafungia EFDs wanasiasa ili wasikwepe kodi? Mbona posho kibao za wafanyakazi wa serikali na taasisi zake hazikatwi kodi? Kwani TRA hawajui? Majumba ya Masaki yanapangishwa kwa bei gani na serikali inakusanya kodi kiasi gani kutoka huko? Je TRA hawajui mbona hawaendi huko?

Watu wengi wanasema wafanyabiashara wanakwepa sana kodi na kwamba wafanyakazi hawana nafasi hiyo ya kukwepa kodi. Ukweli ni kwamba wafanyabiashara wakubwa pekee ndio wenye uwezo wa kukwepa kodi kupitia connections zao na vigogo wa serikali pamoja na exemptions wanazopata lakini mfanyabiashara mdogo hana hiyo privilege ila anakung'utwa kodi vibaya sana. Tofauti inayojitokeza kwa mfanyabiashara mdogo ni kwamba anamhonga afisa wa TRA laki sita na analipa kodi 50,000. Asipofanya hivyo afisa wa TRA atam assess kodi ya milioni tatu bila kupungua. Na utakuta kodi halisi ni 650,000 lakini usipohonga utalipa 3m so sio kweli kwamba wafanyabiashara hawalipi kodi ila kodi wanayolipa inaliwa na maafisa wa TRA na serikali za mitaa badala ya kwenda kwenye mifuko ya serikali. So swali la serikali kujiuliza na kwamba kodi hii inakwenda wapi sio wafanyabiashara hawalipi kodi. Ndugu zangu mtaona tatizo la nchi yetu ni rushwa na kuwa na serkali dhaifu sio kwamba wafanyabiashara hawataki kulipa kodi.

Ukienda kariakoo bei za frame zote ni sawa tofauti tu itakuwa hii frame ya barabarani, hii frame ya ndani, frame za barabara hii ni bei fulani na kadhalika lakini sio hivyo kwa suala la kodi. Wewe mwenye biashara kidogo sana utalipa kodi kubwa na mwenzio mwenye biashara kubwa atalipa kodi ndogo sana kwa nini? Jibu ni RUSHWA. Hebu TRA waseme frame zote za mbele za mtaa wa kongo itakuwa 1m kwa mwaka au kodi yoyote watakayoona wao halafu waone kama wafanyabiashara hawatalipa? Lakini tatizo sio kodi ila wanazo hila zilizojificha na hicho ndicho wafanyabiashara wanachokiogopa. Mbona bei za leseni ni moja tu na kila mfanyabiashara ana leseni mbona hawakwepi? Jibu ni kuwa mfumo uko wazi na as a result una prompt voluntary compliance. TRA hawataki voluntary compliance kwa sababu ikiwa hivyo vitambi vyao vitanyauka. Mbona daladala wanalipa uniform tax mbona hawakwepi kwa nini frame za kariakoo isiwe hivyo on average serikali itapata kodi kubwa kuliko kuanza kuwalazimisha waingie gharama zisizo za msingi kama EFDs, audited accounts na kadhalika wakati biashara zile ni ndogo sana na zenye ushindani mkubwa sana na hata faida zake ni kidogo pia. Kwa nini serkali yetu inatesa wananchi wake kwa jina la uzalendo wa kulipa kodi wakati viongozi hawaonyeshi hata kidogo huo uzalendo?

Kama mfanyabiashara kamhonga afisa wa TRA 600,000 ataionyesha wapi kwenye mashine ya TRA? Kama kamlipa mwenye nyumba 30m na mwenye nyumba kamuandikia mkataba wa shs 3m atazionyesha wapi zile 27m ambazo hazijaandikwa kwenye mkataba? Kama mauzo ya mfanyabiashara kwa mwaka yatakuwa 100m as per EFD gharama za mfanyabiashara zitakuwa chini kwa 27m ya kodi, kwa 600,000 aliyomhonga afisa wa TRA halafu TRA watazihesabu kama profit na kumlima kodi tena mfanyabiashara je kwa mazingira haya utamtegemea mfanyabiashara wa kariakoo azikubali hizi mashine? Tuache unafiki na tuone tatizo liko wapi?
 
Pasco,

Sijui na wewe unaanza kuchanganya mambo. Issue hapa sio kukataa au kukwepa kodi, ila ni ulanguzi unaofanywa na TRA kwa kisingizio cha kufuatilia kodi. Na wafanyabiashara wa Kariakoo hawako peke yao kwenye hili. Ni hivi majuzi tu Mbeya nako kulikuwa na sintofahamu.

Tukumbuke hizi sio zama za RTD, kwamba taarifa zinapatikana kupitia RTD na wakina Uhuru/Dailynews. Zama za utandawazi zinampa raia wa kawaida uwezo wa kupata habari anayotaka na kwa muda anaoutaka yeye.

Bei ya hizi machine ni wizi mtupu na TRA wanataka kuleta maujanja kwenye huu ulanguzi. Hata hapo Kenya, pamoja na unyang'au wao, watu wanauziwa machine kwa bei nafuu. Hizi za TRA zina almasi ndani yake?

Kumbuka, kama kuna watu wanye uwezo wa kufuatilia bei za hizi machine basi wafanyabiashara wa Kariakoo watakuwa wa kwanza. Kila kukicha wanaenda China kununua bidhaa, wanajua hizi machine zinauzwa bei gani, leo hii mtu mzima anasimama na kuwaambia machine laki 8?

Na hata kama TRA watakuja na kisingizio kwamba wao wanatumia models za ghali, bado swali la msingi linabaki, kwanini wawachagulie watanzania machine za ghali? Hivi ni kweli machine zinazouzwa na TRA ni za viwango vya juu sana hivyo kufanya bei ya sasa kuwa sahihi?

Mh. Zambi ameongea bungeni baada ya kufanya uchunguzi binafsi, na anakubaliana na madai ya wafanya biashara kuwa bei za hizo machine si sawa. Kwanini TRA wanaendelea kungang'ania huu ulanguzi? Na kwanini waziri wa Fedha anakuwa bubu? Si ajabu huyu waziri na mawani yake wala hana habari ni kiasi cha fedha Tanzania imepoteza kwa kufunga maduka? Uchumi hauendeshwi kwa mtindo huo!
Mkuu FJM, Hiyo mashine, inalipiwa na TRA wenyewe kwa ku deduct kwenye kodi yako!.
Pasco.
 
Wabongo tumezoea sana wizi na kukwepa, wafanya biashara wamezoea super profit, kwa vile sasa mashine zitaonyesha kila kitu, nanataka kuzigomea!. Mbona wahindi wanazitumia na hawagomi?!.

Anayelipa kodi ni end user, hivyo anayepaswa kugoma ni mteja baada ya kupandishiwa bei kufuatia wafanya biashara kulipa kodi!, na sio wafanya biashara wagome kuuza, kisa kodi iko juu!. Huu sasa ni mwanzo mzuri wa hivi vibiashara mchoro mchoro vifungwe zibaki biashara halali tuu!.

Kwa upande wa EFD, nako ni wizi mtupu!, mashine inauzwa dola 100, hapa unauziwa dola 1000!.
Ukiamua kununua mwenywe, wale maajent wa TRA hawakubali ku install!.
Mijimashine yenyewe approved kwa Tanzania yote inatumia windows only kwa sisi tunaotumia mac, tunalazomika kununua computer ya window kwa ajili ya EFD tuu!.
Huu pia ni nyanyasaji!.
Pasco.
Pasco.

Nimekusoma Mkuu Pasco! Labda nichangie kidogo
Mosi wazo la TRA kuanzisha matumizi ya hizi machine ni vizuri na linapaswa kuungwa mkono japo jambo linapotambulishwa na kutumika kwa mara ya kwanza linakuwa na changamoto nyingi. katika hili nikubaliane na wewe kuwa kuna changamoto ambayo TRA wanatakiwa kuzifanyia kazi........
Ila kuna upotoshaji ambao unafanyika katika zoezi hili kwa mfano Kariakoo siyo kweli kuwa wafanyabiashara wa KKoo wote wanatakiwa kutumia hizi machine soko la kariakoo na viunga vyake vinawafanya biashara zaidi ya 60,000 lakini ambao wamelengwa kwenye zoezi hili ni 38,000 tu ambao Wamachinga,mama ntile hawahusiki na kwa maelezo ya TRA yeyote ambaye anaona kuwa pato lake halifiki 14mil kwa mwaka aseme ataondolewa kwenye zoezi na List ya hao wafanyabiashara ipo ila watu wameamua kugeneralize kuwa ni watu wote:

TRA wamelitanganza international tender kwa manufacturer wa mashine hizi na Jumla ya Kampuni 8 zilipita kwenye hii zabuni. na hizi machine zipo tailor kwa mazingira ya kitanzania kwa maana kwamba lugha Swahili/english na specification walizotumia ni kutoka TRA ambazo zitawesha zoezi hili kwenda smoothly. Kitu ambacho kinapelekea kuwa ukinunua machine kutoka kwa wazalishaji wengine mbali ya hao 8 machine yako itakuwa tofauti na haisomani na system ya TRA.

BEI YA MASHINE:
Gharama halisi ya Machine hizi kulingana na uwezo na aina ya biashara unayofanya zina range $245- 280 CIF + Distribution cost+Margin+ Other cost inaleta around $520 ukiconvert kwenye Tsh...unapata 800,000 ila wasambaji wamekuwa wakiuza mpaka laki 6 kwa kila machine.

Tatizo la Kkoo!
Mkuu Pasco tuwe wakweli na tuweke itikadi zetu pembeni hata kama CCM siwapendi! Issue ya EFDS ni Mtolea Ngoma tu ila kunasababu nyingine nyingi ambazo zimeambatana na hii. ila kwa muda mrefu wafanyabiashara wa kkoo wamekuwa cyo walipa kodi wazuri. na wengi wametajirika cyo kwasababu biashara inalipa bali ni kwamba hawalipi kodi.

Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi biashara kariakoo zimedorora sana wale wateja waliokuwa wanatoka Malawi,Zambia,Congo,Zimbabwe na Kwingineko kuja kujumua Kkko hawaji tena.
Mosi wengine wanakwenda wenye China,wengine wananulia Uganda ambako wako wanaruhusu nguo kuingia bure au kwa kodi nafuuu kushinda sisi na kubwa zaidi kuna wakinga wamefungua magodauni Mbeya wanaenda kuchukua mizigo china na maeneo mengine wanauzia mbeya so wazambia, congo na malawi wanaona ni bora wanunulie Mbeya.

Kitendo cha TRA kutambulisha huu mfumo wa machine ambayo kila bidhaa unayouza kodi inakatwa automaticaly inaonekana ni Mwiba mkali kwa wafanyabiashara ambao cyo wakweli.

Na kwa mujibu wa wafanyabiashara issue cyo Bei ya Machine ni kwamba hawataki machine ziwepo kabisa!

Tuendelee kuelimisha kwa vile vidogo tunavyovijua kuliko kupotosha!

Naomba kuwasilisha mkuu!
 
naomba kuuliza swali ambalo liliulizwa na mtu huko nyuma

Je nchi za Ulaya, usa, south africa wanatumia mashine zipi?

Kenya na Rwanda wanatumia mashine zipi?
EFD ni EFD, haijalishi ni mashine zipi kama zilivyo computers, ya kwangu ni Icotex imetengenezwa Bulgaria, haipokei computer za mac!.

Lengo la EFD zimewekewa GPRS hivyo kila transaction, TRA wanaiona na inaonyesha kodi ni kiasi gani!.

Kiukweli, hata kama TRA wanamonitor, kukwepa kodi ni tabia!, wenye mazoea hayo tayari wana risiti 2!, ya TRA na ya kwao!. Ukinunua usipodai risiti, wanaiba!, ili nchi isiendelee kuibiwa kodi na hawa wafanyabiashara wezi, kila mwananchi auelimishwe, ukinunua lazima mwenyeduka akupe risiti, na sipokupa, dai risiti!.
Pasco.
 
Hoja ya kwamba bei ni kubwa hata mimi nakubaliana nayo lakini tatizo wafanyabiashara wenyewe hawana kauli moja kuhusu ni kwanini hasa hawataki hizi mashine!!! Hizi kauli mbili mbili ndizo zinazotia shaka; kwamba mara huwezi kumpunguzia mteja coz' hata ukimpunguzia utalazimika kulipa kodi ya original price, ukiongea na mwingine anakuambia kodi kupitia hizi mashine ni nyingi; ukisogea upande wa pili wanakuambia wao hawakatai kulipa kodi na wapo tayari kulipa kodi kwa mfumo wa zamani....ukikutana na mwingine yeye ndo atakueleza suala la bei ya mashine kuwa kubwa!!!

BInafsi, nakubaliana na hoja kwamba hizi mashine bei yake kwa wengi ni kubwa especially kule mikoani lakini tutake tusitake; hizi mashine hata kama ingekuwa zinatolewa bure bado wafanyabiashara wengi wasingezipenda...wabongo tumeshazoea maisha ya ujanja ujanja! Hata wakati LUKU zinakuwa introduced, watu walikuwa wanazipinga ile mbaya coz' walifahamu ule ujanja ujanja wa bili imefikia laki 7 lakini msoma mita unampa elf 20 anakausha; ndo basi tena! Hapa ndipo ulipo msingi wa tatizo; hizi zingine zote ni kutafuta public sympathy!!
Hebu tuwe realistic hivi wafanyabiashara hasa tunaowazungumza au walio ktk kundi la waathirika zaidi ni wepi? Kwa wafanyabiashara wadogo wa mapato ya shilingi milioni 14 kwa mwaka gharama ya kununua EFD moja kwaTsh. 800,000-1,500,000 ni fedha nyingi na anayo haki ya kulalamika. Labda kwa wafanyabiashara wa mapato ya juu
 
Kwa taarifa yako wafanyabiashara wananouza Tshs 110,000 kwa siku au zaidi ndiyo wapasao kusajiliwa VAT
 
Something is behind this mgomo...but the bottom line is TRA ikicheka na wafanyabiashara hakuna kodi itakayokusanywa....hawa sio watu wa kuwachekea kabsa...pamoja na vipato vyetu vya chini wafanyakazi tumelipa kodi sana....tuanze kugawana maumivu sasa na kuongezwa tax base kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii.

Unasema kwa uchungu na wengi wansema kama wewe ikiwa ni pamoja na wabunge(hata mawaziri) ambao wenyewe wanauchungu sana na maendeleo ya nchi kiasi cha kukataa mishahara yao na marupurupu lukuki walionayo kukatwa kodi. Wanyonge mwaka huu wataipata

Ningefurahi kama angesimama waziri au mbunge mmoja jasiri akatuonesha TIN yake na mchango wake kwa mwaka kupitia kodi na hilo likawa chagizo kwa wengine kuiga
 
Hoja ya kwamba bei ni kubwa hata mimi nakubaliana nayo lakini tatizo wafanyabiashara wenyewe hawana kauli moja kuhusu ni kwanini hasa hawataki hizi mashine!!! Hizi kauli mbili mbili ndizo zinazotia shaka; kwamba mara huwezi kumpunguzia mteja coz' hata ukimpunguzia utalazimika kulipa kodi ya original price, ukiongea na mwingine anakuambia kodi kupitia hizi mashine ni nyingi; ukisogea upande wa pili wanakuambia wao hawakatai kulipa kodi na wapo tayari kulipa kodi kwa mfumo wa zamani....ukikutana na mwingine yeye ndo atakueleza suala la bei ya mashine kuwa kubwa!!!

BInafsi, nakubaliana na hoja kwamba hizi mashine bei yake kwa wengi ni kubwa especially kule mikoani lakini tutake tusitake; hizi mashine hata kama ingekuwa zinatolewa bure bado wafanyabiashara wengi wasingezipenda...wabongo tumeshazoea maisha ya ujanja ujanja! Hata wakati LUKU zinakuwa introduced, watu walikuwa wanazipinga ile mbaya coz' walifahamu ule ujanja ujanja wa bili imefikia laki 7 lakini msoma mita unampa elf 20 anakausha; ndo basi tena! Hapa ndipo ulipo msingi wa tatizo; hizi zingine zote ni kutafuta public sympathy!!

hayo majibu tofauti uliyopewa yote ni matatizo.Tatizo sio mashine kuwa ghali tu,bali na hayo mengine pia.Unajua Tanzania haina siku nyingi toka ilipobadili muelekeo wa wananchi wake kuacha kutegemea ajira za serikali hadi kujiajiri na hapo hapo leo hii tuna vyuo vingi vinazalisha watu wanaotaka ajira/kujiajiri wengi kuliko miaka ya nyuma.Kwa hiyo asilimia kubwa ya wale tunaowaita "wafanyabiashara" kiukweli bado ni small scale na medium scale na wengineo weengi waliobakia ni wajasiriamali.Kwa hiyo taifa hili lilihitaji kuwapa muda wa kutosha na msaada raia wake wafike mahali ambapo utakusanya kodi kubwa kutoka kwao bila malalamiko mengi.Lakini ukitazama rates za kodi na uhalisia wa uchumi wa mtu mmoja mmoja,utagundua hatuwasaidii wananchi bali tunawatreat kama vile tuliwapa misingi mizuri ya kiuchumi.Tunajenga gap kati ya maskini na matajiri,kwamba wachache wenye uwezo wa kulipa kodi hizo watahodhi njia za uchumi,wasioweza watabaki hawana la kufanya na huku serikali haina mpango na hawa walalahoi,then kitakachotokea hapo nakiogopa sana na dalili zinaanza kuonekana,kila kinachokuwa introduced na serikali watu wanalalamika tuu na wakubwa hawazingatii malalamiko hayo zaidi ya kuona wananchi wahuni,hii ni dalili kwamba tuendako si kwema,bora tuzuie mambo yasifike huko
 
Kaka hawa TRA hamna kitu kabisaaaa,hivi wana kitengo cha utafiti kweli????!!!!!
Huwa wanajifunza kutoka kwa wenzao kweli???!!!!
Wana nia ya kuikomboa hii nchi kupitia kodi kweli???!!!!
Waziri wa fedha na wataalamu wake wako aware kweli na uhitaji wa nchi hii katika suala hili??!!!

To hell with it, bora uchaguzi uje tujue la kufanya!!!!
Khaa!! Lipa kodi bana. Mbona mumeleweshwa kila kitu kwamba hiyo pesa mtarudishiwa kwenye mchakato wa kulipa kodi. nyie vipi hamuelewi? Au hamzitaki hizo machine? Au mlikuwa mnakwepa kulipa? Lipeni bana wafanyakazi wanaumia sana kwa sababu ya kukwepa kwenu:A S tongue:
 
Wabongo tumezoea sana wizi na kukwepa, wafanya biashara wamezoea super profit, kwa vile sasa mashine zitaonyesha kila kitu, nanataka kuzigomea!. Mbona wahindi wanazitumia na hawagomi?!.

Anayelipa kodi ni end user, hivyo anayepaswa kugoma ni mteja baada ya kupandishiwa bei kufuatia wafanya biashara kulipa kodi!, na sio wafanya biashara wagome kuuza, kisa kodi iko juu!. Huu sasa ni mwanzo mzuri wa hivi vibiashara mchoro mchoro vifungwe zibaki biashara halali tuu!.

Kwa upande wa EFD, nako ni wizi mtupu!, mashine inauzwa dola 100, hapa unauziwa dola 1000!.
Ukiamua kununua mwenywe, wale maajent wa TRA hawakubali ku install!.
Mijimashine yenyewe approved kwa Tanzania yote inatumia windows only kwa sisi tunaotumia mac, tunalazomika kununua computer ya window kwa ajili ya EFD tuu!.
Huu pia ni nyanyasaji!.
Pasco.
Pasco.

Pasco kulazimisha kutumia mashine wala si suluhu ya kuwafanya TRA kukusanya kodi,kumbuka ili
iweze kulipwa kodi ni lazima mnunuajia apewe risiti,je ni watanzania wangapi mpaka leo wakinunua
vitu wanaomba risiti?? je unafikiri mfanyabiashara anapenda kumpa mnunuzi risiti kama hajaiomba?
So kuna la muhimu zaidi tu ya kuwauzia wafanyabiashara mashine mbovu za EFD's'
 
Mkuu FJM, Hiyo mashine, inalipiwa na TRA wenyewe kwa ku deduct kwenye kodi yako!.
Pasco.

Pasco naona wengio mnaongelea kwa wale wanaolipa VAT tu,kumbukeni kuna wafanyabiashara ambao
hawalipi VAT na wametakiwa kuchukua mashine kwa ajili ya kutoa risiti tu,hii mnaiongeleaje?
 
Ndugu, unajadaili NJE ya mada.
Hapa mjadala ni mashine zenyewe, yaani EFD. Kwamba, bei hali ya mashine hizo ni mara 15 chini ya bei wanazouza kwenye maduka yaliyopendekezwa na TRA. Kwa nini hali iko hivyo? Kwa nini TRA wasiache biashara ya EFD iwe huru kama zilivyo calculators na laptop?
Mkuu there is a point you are missing,,,hizi mashine kwanza TRA haiuzi coz ni za TRA, na sio wafanyabiashara,,hela watakayotoa wafanyabiashara itakuwa setoff kwenye return zao za kodi,,,so literally mfanyabishara hapa hatoi pesa yake mkononi kozi hiyo pesa atarudishia,,so kama kuuzwa kwa bei ya juu,,TRA wenyewe ndo wangelalamika kuwa hizi mashine ni bei ghali.Kiini cha huu mgomo ni kukwepa kodi na gharama,,kwani hizi mashine hazidanganyi mapato mkuu.
 
Hii nchi hatuna muda mrefu tutashuhudia vita kali sana, nasema hivi kwa uchungu sana. Watu wanakwepa kulipa kodi kwani kodi yetu inatumika isivyostahili, sasa kama mwananchi haoni manufaa ya kodi anayotoa utamshawishi vipi kulipa? Mwananchi anaona wawekezaji wakiiba mali zetu za matrilioni mchana kweupe huku wakisamehewa kodi; huku mzalendo akiuza karanga TRA wanakula nae ligi alipe kodi wakati wawekezaji wanasepa na mali zetu? Mungu utusaidie sana. Pia kwenye hizo mashine lazima kuna udalali kama ule wa speed governor
 
Ndugu, unajadaili NJE ya mada.
Hapa mjadala ni mashine zenyewe, yaani EFD. Kwamba, bei hali ya mashine hizo ni mara 15 chini ya bei wanazouza kwenye maduka yaliyopendekezwa na TRA. Kwa nini hali iko hivyo? Kwa nini TRA wasiache biashara ya EFD iwe huru kama zilivyo calculators na laptop?

Nashukuru kwa mchango mzuri. Endeleeni kutoa elimu kwa wote wanaochangia hoja pasipo kuelewa. Hili nalo ni tatizo linalotukabili, yaani kusoma hoja na kuanza kuichangia pasipo kuielewa. Hata wabunge wetu wako hiviv hivi, ila tuwaelimishe na kuwasemehe.
 
hayo majibu tofauti uliyopewa yote ni matatizo.Tatizo sio mashine kuwa ghali tu,bali na hayo mengine pia.Unajua Tanzania haina siku nyingi toka ilipobadili muelekeo wa wananchi wake kuacha kutegemea ajira za serikali hadi kujiajiri na hapo hapo leo hii tuna vyuo vingi vinazalisha watu wanaotaka ajira/kujiajiri wengi kuliko miaka ya nyuma.Kwa hiyo asilimia kubwa ya wale tunaowaita "wafanyabiashara" kiukweli bado ni small scale na medium scale na wengineo weengi waliobakia ni wajasiriamali.Kwa hiyo taifa hili lilihitaji kuwapa muda wa kutosha na msaada raia wake wafike mahali ambapo utakusanya kodi kubwa kutoka kwao bila malalamiko mengi.Lakini ukitazama rates za kodi na uhalisia wa uchumi wa mtu mmoja mmoja,utagundua hatuwasaidii wananchi bali tunawatreat kama vile tuliwapa misingi mizuri ya kiuchumi.Tunajenga gap kati ya maskini na matajiri,kwamba wachache wenye uwezo wa kulipa kodi hizo watahodhi njia za uchumi,wasioweza watabaki hawana la kufanya na huku serikali haina mpango na hawa walalahoi,then kitakachotokea hapo nakiogopa sana na dalili zinaanza kuonekana,kila kinachokuwa introduced na serikali watu wanalalamika tuu na wakubwa hawazingatii malalamiko hayo zaidi ya kuona wananchi wahuni,hii ni dalili kwamba tuendako si kwema,bora tuzuie mambo yasifike huko
Ili kuwawezesha hao wananchi unaosema ni lazima serikali ikusanye kodi! Watu walio katika kundi hili ni wale wanaofikia mauzo ya TZS 14 million and above! Mfanyakazi anayepata gross salary TZS 250,000/- kwa mwezi ambapo ni sh.3,000,000/- kwa mwaka analipa kodi ya mapato lakini wewe unataka mfanyabishara anayefikisha mapato ya 14 million (karibu mara tano ya mfanyakazi) huyu asilipe kodi!! Come on, gimme a break! Hao wanaolalamika wengi wao wala hawamo ktk kundi la wale wanaolipa VAT ambao wao wameanza kutumia hizi mashine kwa muda mrefu sasa!
 
Khaa!! Lipa kodi bana. Mbona mumeleweshwa kila kitu kwamba hiyo pesa mtarudishiwa kwenye mchakato wa kulipa kodi. nyie vipi hamuelewi? Au hamzitaki hizo machine? Au mlikuwa mnakwepa kulipa? Lipeni bana wafanyakazi wanaumia sana kwa sababu ya kukwepa kwenu:A S tongue:

Pamojaaa na yoteeee mtu binafsi hatakiwi kuikopesha mamlaka kwa kigezo cha ukigoma ntakupeleka mahakamani!!!
 
Something is behind this mgomo...but the bottom line is TRA ikicheka na wafanyabiashara hakuna kodi itakayokusanywa....hawa sio watu wa kuwachekea kabsa...pamoja na vipato vyetu vya chini wafanyakazi tumelipa kodi sana....tuanze kugawana maumivu sasa na kuongezwa tax base kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii.

Siku zote, duniani pote mtu wa chini ndiye anayelipa kodi, kwa jina lingine anaitwa mlaji

Usidhani wafanyabiashara wakichukua hizo EFD wao ndio watalipia kodi, wafanyabiashara watachukua kutoka kwako "mlaji" kwa kukuongezea thamani ya VAT, na kwa upendeleo tu, unaweza kuulizwa 'ukitaka risiti bei ni hii na bila risiti bei ni hii' kwa umaskini wako wewe utakuwa wa kwanza kuionea aibu risiti ya EFD unless umetumwa na bosi wako na kakuambia leta risiti
 
Back
Top Bottom